Kuna jamaa yangu alinunua magomeni, incubator na inayoweza kuhatch mayai elfu tisa (9,000) hapo magomeni, cost ilikuwa arround milioni 20 za kitz, inafanya kazi mpaka leo. Yeye biashara yake ni kutotolesha vifaranga tu, unaenda na mayai yako anakucharge 300 kwa kila yai. Yakitoka yasitoke that's the cost. Nikavutiwa na biashara nikatafuta vendor china nikapata kwa dola 2900 kila kitu, hiyo iliikuwa ni hatcher ya mayai 5000 na incubator ya mayai 6000, bei ya hatcher ilikuwa dola 700, na incubator 1100, na hizo 1100 zilikuwa ni contena la futi ishirini kuja tz. Sasa hizi habari ni za mwaka 2010 mwanzoni, sijui sasa zikoje.pia kumbuka kuna tra na customs mzigo ukishafika, fanya utafiti wa gharama za kutoa mzigo. Kama uko interested ingia alibaba.com, jiridhishe mwenyewe na wauzaji kwa kusearch kama unavyofanya google. Halaf malizana nao. Ila kuwa makini, matapeli wengi. Ingekuwa vema ukawatumia watz wanaoenda kununua bidhaa zao huko japo wakachungulie kama jamaa wana kiwanda na wahakikishe usalama wa pesa zako kwa kuthibitisha mzigo unapakiwa melini.
Nb: hata hao watz usiwaamini sana, sanaa zimezidi nchini hapa.
Wadau naomba msaada wenu. Mimi ni mjasiliamali anayejishugulisha na ufugaji wa kuku wa kienyeji. Shida yangu ni Incubator mashini ya kuangulia mayai. Sijawa na mtaji wa kununulia incubator halisi ila nataka nianze kwa jinsi ya kiasili kabisa ya kuangua mayai japo kati ya 25 hadi 40 ili kuokoa mayai mengi yanayoharibika kwa kuachwa na kuku mwenyewe na pia ili kupata vifaranga wengi kwa wakati mmoja. Sasa niliambiwa kuna njia fulani ya kutotolesha mayai bila kutumia incubator. Naomba msaada kwa anayefahamu.
Naomba kutoa hoja
Sasa hizi dharau!
Mzee kama hufahamu kitu ni vema ukanyamaza.Dharau ziko wapi hapo?
Nawafahamu vijana wanatengeza hizo incubator hapahala Dar kwa gharama hizo.Zinafanya kazi vizuri tu.Zinatumia umeme na kerosine incase umeme hamna.Zinaweza ku-incubate hadi mayai 120 kwa mpigo(hii ninayotumia ina uwezo huo pia)
Unajua bei ya imported incubator wewe?
Hasira za nini mkuu.
We tayari amesema anamtaji kidogo laki 7 si utakuwa unamuumiza.
Yeye mwenyewe hata hajarespond/kubaliana kwa hyo pesa. Amekaa kimya
Halafu ameomba njia nyingine ya kienyeji tofauti na Incubator. Sasa nashangaa wewe kumbanjikia bei
Kaka incubator inataka umeme wa kutosha kama umeme ukikatika hata 30 min tu umeharibu mayai mkuu ss wengine wakiihitaji wanakuwa na back up ya umeme (Generator) ushauri wangu angalia hao vifaranga unaowataka ni wa kwako wa kufuga achana na hii maneno na kama ni wa kuuza plz anza kutafuta Generator kwanza maana umeme wa ki bongo unaujua usijerudi hapa jamnvini unalia lia tu!