Mashine za kunyolea ndevu n.k zinaitwa Al Shabab | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine za kunyolea ndevu n.k zinaitwa Al Shabab

Discussion in 'JF Chit-Chat' started by mhondo, Oct 29, 2011.

 1. m

  mhondo JF-Expert Member

  #1
  Oct 29, 2011
  Joined: Apr 23, 2011
  Messages: 970
  Likes Received: 33
  Trophy Points: 45
  Nilienda dukani kwa ajili ya kununua vitu mbalimbali vya dukani na kuona mashine ya kunyolea kama zile za Bic au gillete inaitwa Al Shabab ipo dukani. Ninajiuliza swali je zinatengenezwa na kundi la Al shabab la Somalia au imetokea tu majina kufanana?. Na kama zinatengenezwa na kundi hilo kwanini zimeruhusiwa kuingizwa TZ?.
   
 2. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #2
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  al shabab ni kijana mahiri,rijali, aliyekomaa(aliyebalehe na kuota ndevu) nk ndo maana halisi na ndio maana watengenezaji wa vinyoleo hivyo walichagua jina hilo lakini wale jamaa wamejibatiza tu na kwa kuwa ule msahafu haujaandikwa kizungu wala kiswahili lazima uone chenga
   
 3. BADILI TABIA

  BADILI TABIA JF-Expert Member

  #3
  Oct 29, 2011
  Joined: Jun 13, 2011
  Messages: 30,873
  Likes Received: 6,224
  Trophy Points: 280
  ungeipiga picha utuwekee mkuu...
   
 4. Inkoskaz

  Inkoskaz JF-Expert Member

  #4
  Oct 29, 2011
  Joined: Nov 6, 2010
  Messages: 6,318
  Likes Received: 438
  Trophy Points: 180
  usingoje kutafuniwa mkuu.labda hana kamera au mwenye duka asingemuelewa.wewe nenda dukani ulizia mashine au nyembe ya al shabab.pia salon za kiume zipo kibao zinatumika
   
 5. v

  valid statement JF-Expert Member

  #5
  Oct 30, 2011
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 176
  Trophy Points: 160
  nadhani ni jina tu.
   
 6. u

  uporoto01 JF-Expert Member

  #6
  Oct 30, 2011
  Joined: May 23, 2008
  Messages: 4,741
  Likes Received: 21
  Trophy Points: 135
  Shabaab kiarabu inamaanisha kijana,hili kundi lilikuwa la vijana(kama UVCCM au Bavicha) katika Islamic court union kilichokua kikitawala eneo kubwa la Somalia kwa amani kwa miaka mitatu kabla ya uvamizi wa Ethiopia kwa shinikizo la Marekani(waliolipia kila kitu) na kuirudisha tena nchi kwenye vita.<br>Kundi hili lilibadilika na kuwa la kijeshi kuwaondoa Ethiopia.
   
Loading...