Mashine za kisasa zaibwa Muhimbili zina thamani ya Sh150 milioni | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine za kisasa zaibwa Muhimbili zina thamani ya Sh150 milioni

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by Mazingira, Jun 3, 2009.

 1. Mazingira

  Mazingira JF-Expert Member

  #1
  Jun 3, 2009
  Joined: May 31, 2009
  Messages: 1,837
  Likes Received: 23
  Trophy Points: 135
  Na Sadick Mtulya


  VIFAA na mashine kubwa tatu kwa ajili ya kupimia na kufanya utafiti wa magonjwa mbalimbali na mashine zingine ndogo ndogo zilizopo katika maabara maalum (SPL) ya kisasa kwenye jengo jipya lililokarabatiwa na Shirika la misaada la Japan (JICA) kwenye Hospitali ya Taifa Muhimbili vimeibwa.

  Upotevu wa vifaa muhimu kwenye hospitali hiyo umekuwa wa kawaida kwani ni mara kadhaa imeripotiwa kuibwa kwa mashine mbalimnbali bila ya hatua za waziwazi kuchukuliwa

  Afisa uhusiano masaidizi wa hospitali hiyo Jeza Waziri jana aliithibitishia Mwananchi kutokea kwa tukio hilo.

  Thamani ya mashine hizo tatu ni zaidi ya Sh 150 milioni kutokana na kila moja kuwa na gharama zaidi ya Sh 54 milioni.

  Jengo hilo la mradi uliofadhiliwa na serikali ya Japan kupitia shirika lake la misaada ya kiufundi la JICA limetelekezwa tangu Machi 2 mwaka huu.

  Hata hivyo Waziri alisema tayari uongozi umechukua hatua za awali za kufanya uchuguzi kubaini aliyehusika na wizi huo.

  Wizi huo unadaiwa kufanyika kati ya Mei 11 na 25 mwaka huu ambapo viyoyozi viwili viliibwa Mei 11.

  Waziri alipoulizwa kama tukio hilo liliripotiwa polisi, alisema bado hawajafanya hivyo na kwamba wanatarajia kuripoti wakati wowote kuanzia sasa katika katika kituo cha polisi Sarender Bridge jijini Dar es Salaam.

  Lakini habari ilizolifikia Mwananchi jana zilisema wizi huo umesababishwa na uzembe wa hospitali hiyo kutokuweka ulinzi tofauti na ilivyokuwa kabla hawajakabidhiwa jengo hilo.

  Maabara hiyo iliyopo karibu na wodi A na B maalum ya watoto ilianzishwa nchini kwa lengo maalum la kutoa huduma kwa watoto ikiwa ni sehemu ya mpango wa taifa wa kupunguza vifo vya mama na mtoto.

  Kwa mujibu wa chanzo chetu ambacho hakikutaka kuandikwa gazetini hali hiyo imetokana na uongozi wa Muhimbili kutolifutilia jengo hilo ambalo linasimamiwa na idara ya watoto na utawala

  Chanzo hicho kikasema kutokana na kutothaminiwa kwa maabara hiyo ndio sababu ya kutokuwepo walinzi kwenye jengo hilo ambalo limepakana na ukuta unaotazama eneo la jangwani.

  “Tangu walipokabidhiwa hili jengo la maabara maalumu ‘special laboratory’ (SPL) Machi mwaka huu hapajawekwa walinzi, hali hii ndiyo imesababisha viyoyozi vitatu aina ya ‘Spirit unit’ kuibwa na kuna hatari ya vifaa mbalimbali vikapotea katika mazingira ya kutatanisha,” kilisema chanzo hicho.

  Maabara hiyo ina uwezo wa kufanya vipimo vyote vinavyoweza kuleta majibu ya magonjwa mbalimbali ikiwemo magonjwa ya ini, figo, moyo, kansa ya kizazi na kiume, uvimbe tofauti mwilini na magonjwa mengine.
  Pia katika maabara hiyo wataalam mbalimbali huitumia kwa ajili ya kufanyia utafiti wa magonjwa tofauti. Baadhi ya vitu vilivyoibwa ni viyoyozi vitatu aina ya ‘spirit unit’.

  Source:Mwananchi

  Jamani huu wizi wa vifaa mahospitalini ni mradi wa mtu au? Maana juzi juzi tu Ocean Road Hospital nao waliibiwa machine ya mamilioni na sijui kama kuna watu waliwajibishwa. Sasa Muhimbili, Lol!
   
 2. Mbu

  Mbu JF-Expert Member

  #2
  Jun 3, 2009
  Joined: Jan 11, 2007
  Messages: 12,729
  Likes Received: 187
  Trophy Points: 160

  ...uzembe huo, au ndio kwakuwa mali ya Umma?

  ...mwandishi kachapia, 'Spirit Unit' au Split Unit bana ? :)

  wizi utakoma vipi wakati uozo na uzembe unaanzia kwa Mkuu wa Ulinzi na Usalama hospitalini hapo, Mkuu wa Idara, Mkurugenzi Mkuu wa hospitali na waziri mwenyewe wa Afya (aliyewahi kuwa Mkurugenzi wa Tiba hospitalini hapo)...
   
 3. rmashauri

  rmashauri JF-Expert Member

  #3
  Jun 3, 2009
  Joined: Jan 29, 2009
  Messages: 3,008
  Likes Received: 14
  Trophy Points: 135
   
Loading...