Mashine ya kupalilia imegoma kuwaka nahitaji msaada wa maelekezo

Herbert Nkuluzi

JF-Expert Member
Aug 10, 2015
2,431
2,436
Kama mnavyofahamu wakulima tunapaswa kuongeza ufanisi wa kazi yetu hii kwa kuongeza matumzi ya zana bora za kisasa ,mimi mwenzenu nimeagiza mashine ya kupalilia inaitwa BRUSH CUTTER japo ina majembe ya kulima ,kupalilia na kufyeka sasa leo nimeamua niiwashe .Nikatia petrol kwenye tank nikaweka oili kwenye port ya oil ila kuwasha mashine haiwaki na tatizo ni kwamba sijajua kijiswichi fulani hivi kinatakiwa kuwa wapi wakati nawasha na zaidi nimekuja kutazama mafuta yake naambiwa eti huwa ni mchanganyiko wa petrol na oili sasa naomba msaada hapo kwa wenye mashine ya aina hii au utaalamu mnisaidie nifanye nini mashine iwake.

Ni Honda GX35 ,4 stroke
Kwa mwenye uzoefu ni vema tupeane namba hapa nimpigie anielekeze vizuri

My number 0755346718/0625911797
 
Picha zake ni hizi
IMG_20210221_164214_3.jpg
JPEG_20210221_164717_1141866139371440275.jpg
 
Ya kwako ikoje na mimi nimeagiza ya 52cc yenye jembe la kupalilia na kulimia.
Niloagiza iko sawa na #10 yako ikoje maana umepiga close up sana haieleweki.

Ila bila shaka ina spark plug na carburetor hivyo vitu lazim ni kawaida kurekebisha baada ya muda. Sijui mfumo wa oil. Inatunia engine oil nadhani.

Naomba mrejesho Bro tupeane akili
 
hiyo mashine inatakiwa iwashwe na fundi wa chain saw au motor pump na mwisho ukikosa hao ni wa pikipiki. Kuna sehemu ya kuweka oil, oil chafu na petrol, petrol inatakiwa ichanganywe na 2T/4T stroke engine (zipo maduka ya kuuza oil).

Kawaida mchanganyiko ni nusu lita kwa lita 5 za petrol au wengine wanaweka vizibo 2 kwa tank inategemea. Ukibugi kuua mashine ni sekunde tu
 
Ya kwako ikoje na mimi nimeagiza ya 52cc yenye jembe la kupalilia na kulimia.
Niloagiza iko sawa na #10 yako ikoje maana umepiga close up sana haieleweki.

Ila bila shaka ina spark plug na carburetor hivyo vitu lazim ni kawaida kurekebisha baada ya muda. Sijui mfumo wa oil. Inatunia engine oil nadhani.

Naomba mrejesho Bro tupeane akili
Ni ya kubeba mgongoni , ni 4 Stroke engine , ina majembe ya kulima (2) ,kupalilia 1 kufyeka nyembe 4
Nitaiphotoa kesho nikutumie ilivyo kwa uzima wake wote
 
Haka tukitu kakijaa oil ikizidi kwenye tank lake huwa hakawaki....
Kama Bado kanazingua na upo Dar, nenda kamata Kuna wakala wa Honda atakuwashia
 
4 stroke haichanganywi oil na petrol kwa pamoja. Kila fluid unaiweka sehemu yake. Angalia plug yake kama ni nzima, kagua hiyo plug, ukiifungua na ukakuta imelowana ujue kuna tatizo lazima fundi ahusike hapo. Kabla ya kuiwasha, kuna switch ambayo mara nyingi ina rangi nyekundu, hakikisha ipo on. Pia kuna switch ya kuset speed, hakikisha speed ipo juu. Kujua speed kama ipo juu, wamechora mnyama sungura na kobe, ikiwa kwenye sungura ipo juu na kobe speed ipo chini, ikigoma kuwaka na hapo, pandisha choke au shusha. Ikigoma kuwaka kama unaweza fungua carburator, ifungue na uhakikishe ni safi, funga na ujaribu kuiwasha tena na yenyewe kama ni nzima, huwa kuna mtego upo maene hayo ya carburator utakua umefyatuka ni wa kuutega tena na uwashe. Kama huna ufahamu wa hivyo vitu nilivyokuelekeza, nasisitiza peleka kwa fundi hata hao wa pikipiki watakurekebishia.

Nb: mimi sio fundi ila nina pump za petrol kwa muda mrefu na changomoto ya kutokuwaka imenikuta mara nyingi
 
Mi nimeiwasha ya kwangu 2T au 2 stroke.

Wengi wanajisahau unapojaza mafuta carburator inakuwa tupu haina petrol kabisa. Pikipiki yanaingia yenyewe.

Kwenye 2T ukishachanganya mafuta kwa vipimo una pump kwa kutumia kubonyeza kipira au pale chini air cleaner kujaza mafuta kwenye carbutor inawaka. Ikishawaka chock inabidi iwe off.

Pia aliyeuza wengi hawajui tofauti ya 2T na 4T sasa baadala ya kusoma manual wanamwamini muuzaji na kuuwa mashine.
 
Mashine mpya lakini mpaka utie tie vidole kuiwasha... Inasikitisha sana...
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom