Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania (TPA) inaujulisha Umma kuwa Jumapili tarehe 23 Mei 2021, Majira ya saa 8 Mchana katika Bandari ya Dar es Salaam, mashine ya kunyanyua vitu vizito (crane) iliyokuwa ikishushwa kutoka kwenye meli ya LCT AJE 1 ilipata ajali ya kutumbukia baharini.
Mashine hiyo yenye uzito wa takribani tani 70 iliwasili kwa meli katika Bandari ya Dar es Salaam ikitokea visiwa vya Songosongo na ilikuwa ikishushwa katika eneo la Gati la Malindi. Zoezi la kuiopoa mashine hiyo linaendelea.
Credit: Le Mutuz TV