Mashine ya Kiotomotela ya Benki Stanbic Shoppers Plaza Mikocheni mbovu, watumiaji muwe makini

mwanamwana

JF-Expert Member
Aug 1, 2011
1,076
4,113
Habari wakuu,

Kiotomotela cha Benki ya Stanbic jengo la Shoppers Mikocheni ni kibovu ambapo hupelekea wateja kusumbuka sana, hivyo kutoa mwanya kwa mlinzi kutoa msaada.

Ubovu wake ni kwamba screen yake mwanga ni hafifu sana kiasi kwamba huwezi kutumia wakati jua likiwepo, kwa usiku sijui inakuwaje. Nadhani ubovu ule ni kutokana na kupigwa jua kwa muda mrefu hivyo kufifilisha mwanga.

Mimi leo nimeenda kutoa mpunga ila baada ya kuchomeka kiotomotela nilishindwa kuona chochote hata baada ya kuhangaika kwa takribani dakika 1 mpaka mashine ikaanza kutoa mlio fulani.

Akaja mlinzi kutoa msaada akiwa kavaa kapelo na kitambaa anachojifunika ili aweze kuona kwenye display. Kweli alinisaidia nikafanikiwa lakini sijapenda maana unafanya muhamala ikiwa pamoja na kuweka nywila yeye akiwa hapo hapo.

Ajabu baada ya kutoa pesa ikawa kama kasita kunirudishia kiotomotela changu mpaka nilipomwambia anipatie, huenda alikuwa kasahau.

Baada ya kuchukua mpunga nikaenda kwenye egesho la gari, kwa muda ule mpaka naondoka mlinzi alikuwa kasaidia watu wanne.

Ombi langu kwa Benki husika: Naomba sana mfuatilie na kurekebisha tatizo hili, Benki muhimu kama hii kuendekeza tatizo dogo kama hili ni ajabu sana.

Walinzi mnaowaweka pale ni kwa ajili ya kuangalia usalama wa wateja na pesa zao na sio kuwasaidia wateja kutoa pesa. Mbona viotomotela vingine vinavyozunguka pale havina tatizo kama lenu?

Nawatakia utekelezaji mwema.
 
Aisee siku ukijisahau tu ukawaachia atm card yako utakuta uniform na bunduki kaacha hapo hapo.

Hali ni tete Sana mtaani.nadhani bank zinabidi ziganye Kila namna kupreserve wateja ikiwemo hyo ya usalama wa pesa pamoja na mazingira Bora ya kibenki.
 
Aisee siku ukijisahau tu ukawaachia atm card yako utakuta uniform na bunduki kaacha hapo hapo.

Hali ni tete Sana mtaani.nadhani bank zinabidi ziganye Kila namna kupreserve wateja ikiwemo hyo ya usalama wa pesa pamoja na mazingira Bora ya kibenki.
Kweli mkuu, inabidi tuwe makini sana. Pia hawa walinzi wasikae karibu na mashine za kutolea pesa.
 
Hilo neno 'Kiotomotela' limenifanya nijisikie nimechacha ghafla
Asante mkuu kwa tahadhari.
 
Note;ATM-Kiotomotela
.. .Mbona sasa pale amesema 'nilipomtaka mlinzi anirudishie Kiotomotela changu akawa kama anasita'!
....Amrudishie Kiotomotela, ATM, yake ama amrudishie KADI yake ya Kitomotela???
Mkuu naona Kachanganya somo ama ndio kwanza amelisikia hilo neno 'Kiotomotela' kwa hiyo analitumia kikamilifu!!
...just joking, Mkuu!! Heh heh he....
 
Back
Top Bottom