Mashine tatu za kusafisha damu Muhimbili zaharibika | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashine tatu za kusafisha damu Muhimbili zaharibika

Discussion in 'JF Doctor' started by MziziMkavu, Dec 21, 2011.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Dec 21, 2011
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,616
  Likes Received: 4,617
  Trophy Points: 280
  [h=2][/h]  Mashine tatu za kusafisha damu katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam, zimeharibika.

  Hata hivyo, uongozi wa hospitali hiyo umewataka wananchi wenye matatizo ya kibofu cha mkojo, kutokuwa na hofu ya kusitishwa kwa utoaji wa huduma kutokana na kuharibika kwa mashine hizo.

  Afisa Habari wa Hospitali hiyo, Aminiel Eligaesha, alisema kitengo cha kutoa huduma kwa wenye matatizo ya kibofu kinaendelea kufanya kazi kama kawaida na hakuna haja ya kuwa na hofu hiyo.

  Eligaesha alitoa kauli hiyo kufuatia kuwepo kwa taarifa kusambaa hospitalini hapo kuwa huduma ya usafishaji damu

  katika kitengo hicho imesimamishwa kutokana na kuharibika kwa mashine hizo.

  Alisema mpaka sasa kitengo hicho kinatoa huduma kwa kutumia mashine nne kati ya saba zilizokuwa zikitoa huduma awali.

  Alisema licha ya kuharibika mashine tatu kazi ya kuwahudumia wagonjwa haijatetereka kutokana na kuchukua hatua za haraka za kuweka zamu kwa wagonjwa wanaotakiwa kupatiwa huduma hiyo.

  Eligaesha alieleza hatua nyingine waliyochukua ni pamoja na kuwaelekeza wagonjwa wenye kadi za Bima ya Afya

  kwenda katika hospitali nyingine zinazotoa matibabu ya aina hiyo ili pasiwepo na mrundikano wa wagonjwa.

  Aidha, Muuguzi Mkuu wa Kitengo hicho, Morris Ngonyani alisema kwa ujumla kitengo hicho hupokea wagonjwa 10 kila siku na mpaka sasa hakuna mgonjwa aliyekosa matibabu.

  Ngonyani alisema mashine zilizoharibika zinafanyiwa uchunguzi na wataalamu wa kizalendo waliopelekwa nje kujifunza jinsi ya utunzaji wa mashine hizo.
  CHANZO: NIPASHE

  Hata Hospitali ya muhimbili kuna Mafisadi wa kuharibu mashine ya kusafishia Damu ? Kazi kweli Wagonjwa watakufa wengi basi kasheshe bongo yetu   
Loading...