Mashindano ya waandishi wa habari SADC 2021

Analogia Malenga

JF-Expert Member
Feb 24, 2012
2,910
2,000
MASHINDANO YA SADC KWA WAANDISHI WA HABARI KWA MWAKA 2021

Dodoma, 15 Oktoba 2020


Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki inapenda kuufahamisha umma kuwa Sekretariati ya Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) imetangaza kuanza rasmi kwa mashindano ya waandishi wa habari kwa mwaka 2021 (2021 SADC Media Awards Competition). Shindano hili litakuwa katika Makundi manne (4) yafuatayo; picha, uchapishaji, runinga na radio.

Washindi wa shindano hili, linalohusisha washiriki kutoka Nchi zote Wanachama wa SADC watatangazwa kwenye Mkutano wa 41 wa Wakuu wa Nchi na Serikali wa SADC utakaofanyika mwezi Agosti, 2021 ambapo watapewa zawadi na vyeti.

Wizara inapenda kuwahimiza Waandishi wa Habari watakaokidhi vigezo kujaza na kuwasilisha fomu za maombi ya kushiriki katika shindano hili, Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kabla ya tarehe 28 Februari 2021. Kwa taarifa zaidi na kupata fomu za maombi za kushiriki shindano, taratibu na masharti ya kuzingatia, tafadhali tembelea Southern African Development Community :: Media Awards

1602835416281.png
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom