Mashindano ya urembo yazidi kupamba moto tanzania - sasa kuna miss totoz!

Herbalist Dr MziziMkavu

JF-Expert Member
Feb 3, 2009
42,316
33,125
MASHINDANO YA UREMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO TANZANIA - SASA KUNA MISS TOTOZ!



Haya unaambiwa ni mashindano ya Miss Totoz Temeke . Ina maana kuna Miss Totoz Ilala, Kinondoni, na wilaya zingine Tanzania au yanafanyika kitaifa? Picha na post nzima nimevidokoa kutoka blogu ya Father Kidevu (samahani Father Kidevu). Ni kazi kwelikweli!



Miss Totoz 2009, Fatuma Issa

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Dully Sykys, akiimba na watoto, wakati wa kutumbuiza onyesho la Miss Totoz Temeke 2009.


Miss Totoz Tmk 2009, Fatuma Issa(kati) akiwa na mshindi wa pili Jane Anthonyn na mshindi wa tatu Yunis Anthon wakati wa onyesho.

Mbunge wa Viti Maalum Al-Shymaa Kwegiar akiwa na washiriki wa Miss Totoz katika ukumbi wa Equator Grill Dar es Salam


 
MASHINDANO YA UREMBO YAZIDI KUPAMBA MOTO TANZANIA - SASA KUNA MISS TOTOZ!



Haya unaambiwa ni mashindano ya Miss Totoz Temeke . Ina maana kuna Miss Totoz Ilala, Kinondoni, na wilaya zingine Tanzania au yanafanyika kitaifa? Picha na post nzima nimevidokoa kutoka blogu ya Father Kidevu (samahani Father Kidevu). Ni kazi kwelikweli!



Miss Totoz 2009, Fatuma Issa

Msanii wa Muziki wa Kizazi Kipya, Dully Sykys, akiimba na watoto, wakati wa kutumbuiza onyesho la Miss Totoz Temeke 2009.


Miss Totoz Tmk 2009, Fatuma Issa(kati) akiwa na mshindi wa pili Jane Anthonyn na mshindi wa tatu Yunis Anthon wakati wa onyesho.

Mbunge wa Viti Maalum Al-Shymaa Kwegiar akiwa na washiriki wa Miss Totoz katika ukumbi wa Equator Grill Dar es Salam



Hii ni child abuse na inaonekana wazi katika sura ya huyu Fatuma jinsi alivyo panic.

Ni vigumu kuamini kama mzazi yeyote wa halali, hasa baba wa halali anaweza kumuuza binti yake kama hivi. Kama huyu Issa ni muislamu na huyu Fatuma ni binti wake wa halali basi aanbidi afahamu yafuatayo: Wasiokuwa waislamu wanaweza kuchagua wayatakayo wakiona yanafaa.

1. Hii ni haramu na ni masuala (accountability) kubwa mbele ya Mwenyezi Mungu amabayo adhabu yake ni kali sana.
2. Hii ni ukandamizaji wa kijinsia dhidi ya wasichana/wanawake kwa kuwafanya kama bidhaa badala ya watu/binaadamu wenye hadhi na heshima katika jamii.
3. Atumie muda kuchunguza na kuchambua undani wa haya anayoyaiga. Afahamu ya kwamba, kinyume na wanavyojaribu kuonyesha hadharani (kwa kutumia vyombo vya habari kama TV na magazeti) eti kwamba wanafaidi maisha yenye raha na starehe, ukweli ni kwamba, wanaadhibika kwa maisha yenye dhiki na mashinikizo ya aina mbalimbali na katu roho zao hazitulii na wakati wote huwa zimejaa wahka na wasiwasi. Si hivyo tu, lakini baada ya kurubuniwa kote huku na shaitani, shaitani huwa hawaachi kamwe bali ili kutaka kuuondokana na madhila yaliyo ndani ya nyoyo zao humgeukia tena shaitani kuomba msaada, naye shaitani huwarubuni tena kwa kuwadanganya ya kuwa ni katika vilevi, madawa,zinaa, nk, kwamba watapata mapumziko. Huko tena huingia katika matatizo mengine na makubwa na yenye kujirudia rudia (recycled). Kwa kifupi wana maisha "muflisi"
3. Hii katu haitamuondoshea umasikini bali itaaongeza kwa maana itamzidishia moyo wa kutotosheka na kutokinai.
4. Anahitaji asome alama na dalili za ulimwengu unavyokwenda na ajifunze somo la "subira" kwa maana haya yanayotokea hivi sasa ya ulimwengu kulazimishwa kufuata mifumo ya kikafiri ni ya kipindi cha mpito, yanafikia kileleni na sio muda mrefu yataanza kuporomoka(sijasema kikristo, kiyahudi, kibudha nk), nimesema kikafiri,kama tutafahamiana. Sifikirii kama ukristo ndio unaopush mamabo kama haya au kwa mfano kutia msukumo wa kulazimisha kuzitambua ndoa za mabaradhuli, ni makafiri.
 
Hii ni kuwaandaa hawa watoto kuwa MARAYA NA MAKAHABA SIKU ZA USONI. TUTEGEMEE KUWA NA WAKINA LULU WENGI SANA HIVI KARIBUNI. TUNAJENGA TAIFA GANI JAMANI.

IMEFIKIA WAKATI TANZANIA HATA UKIANZISHA MASHINDANO YA KUJISAIDIA HAJA KUBWA. UKIMUALIKA THE SO CALLED MHESHIMIWA ATAKUJA.

IF YOU THINK YOU CANNOT CHANGE TANZANIA, CHANGE YOUR FAMILY,
 
Duh! Hii dunia sijui inaelekea wapi. Laiti wangelijua kama wanawaharibu hao watoto kwa kuwafundisha mambo makubwa wakati bado ni wadogo wasingelifanya huo upuuzi.
 
Hivi ndivo walivo Wengi waishio Tanganyika! Wamekosa kitu kiitwacho "heshima na ustaarabu". Ni watu wa starehe zaidi na upuuzi
 
wabongo wanapenda sana starehe kuliko kazi,
na mbaya zaidi sasa tumeanza kuwatrumia watoto ili kukamilisha burudani zetu. jamani tuwapeleke hawa watoto wasome si kuwatumia kama vyiombo vya burudani
 
Watoto Hawa hawatendewi haki kabisa

Ni Laana hii tunaitafuta

Tunawajengea watoto misingi gani ktk Maisha yao??????????????!!!!!!!!
 
Ndo urithi walioona unawafaa hao watoto na si vinginevyo
 
Watanzania tumelaaniwa kuiga culture ya wenzetu wa magharibi na tumeshndwa kuboresha ya kw2,mwenyezi Mungu a2samehe kwa maana hatujui tulitendalo! Ww mzazi wa mtoto huyu,kama kwl una hekima na busara,wawezaje mtoto kumuuzia sura yke badald ya kumjaza maadili na kumfanya amtambue aliyempa huo urembo? Jiandaeni kwnda kumjibu Mungu cku ikifika!
 
Huyo atakuwa mbunge wa ccm wa viti maalum maana hatambui hata haki za watoto na hicho cheo alipewa na mabwana zake nasema kila siku viti maalumu wafutea maana vitakuja kutuletea wendawazimu ndani ya bunge haya yameanza kujitokeza
 
Back
Top Bottom