Mashindano ya Miss Totoz?

Yo Yo

JF-Expert Member
May 31, 2008
11,217
1,702
attachment.php

attachment.php

Mbunge wa Viti Maalum Al-Shymaa Kwegiar akiwa na washiriki wa Miss Totoz

attachment.php

Fatuma Issa (7) ameibuka kidedea katika shindano la kumpata Malkia wa Watoto, Miss Totoz Temeke 2009 katika Ukumbi wa Equator Grill baada ya kuwashinda warembo wenzake 11 katika shindano lililokuwa gumu na la aina yake wakati majaji Mariam Chaheli, Jowalipokuwa wakichuja nafasi ili kumpata mrembo wa Ukweli kwa Watoto wa Wilaya ya Temeke.

Shindano hilo ambalo lengo lake ni kukuza na kuendeleza Sanaa kuanzia ngazi za chini lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa kutokana na watoto kuchuana vikali kila mmoja akiitaji kuibuka na ushindi na kuweka rekodi ya kwanza katika maisha yake katika shindano hilo, warembo waliobahatika kupanda jukwaani ni pamoja na Janey Anthony, Fatuma Issa, Zaituni Hassan, Neema Ally, Ester Frenk, Ashura Omary,Mariam Karama,Nasra Ally, Yunis Anthony, Angela Silayu,Happy Peter, na Eda Damian.

..........

"shindano hili kusema kweli ni la kipekee, ukiwatazama watoto unagundua kuwa pia wanaitaji kupatiwa mafunzo haya ikiwa mapema ili ifikapo wakati wa mshiriki anakuwa apati tabu na pia anakuwa ana tena aibu kama tunavyowashuhudia baadhi ya washiriki wanashindwa hata kujielezea, kujibu swali hata kama siyo gumu, ukweli wengi wao wanakuwa na aibu, hivyo watoto wakianza kufunzwa angali wadogo bila shaka siku zijazo tutakuwa na washiriki wengi wa Urembo"alisema Al-Shymaa
.......

kikubwa ninawaomba watu mbalimbali kujitokeza kusaidia kufanikisha shindano hili ambalo ni changamoto kwa watoto wetu, ili pia waweze kujitambua umuhimu wao juu ya masuala ya Urembo wakiwa bado wadogo kama ilivyom katika masuala mengine kama mpira wa miguu, na kikapu watoto wanaanza kuelimishwa wakiwa wadogo na hivyo kukua wakijua namna ya kuvitumia Vipaji vyao"alisema Jack

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo alizawadiwa TV na Cheni, wa pili na wa tatu Radio na Cheni wa nne na tano walipatiwa cheni kila mmoja, sambamba na washiriki wote kupatiwa vifaa vya shule ikiwamo vitabu, peni, na madaftari ambavyo vyote vilikabidhiwa na mgeni Rasmi Mh. Mbunge Viti Maalum, Al-Shymaa Kwegiar.

http://michuzijr.blogspot.com/2009/08/fatuma-issa-7-ameibuka-kidedea-katika.html#comments
 
Attachments

  • ujinga.jpg
    ujinga.jpg
    47.1 KB · Views: 625
  • ujinga2.JPG
    ujinga2.JPG
    39 KB · Views: 599
  • ujinga3.jpg
    ujinga3.jpg
    38.6 KB · Views: 609
Last edited:
jamani wazazi wenzangu ndo upuuzi gani huu?unafikiri urembo ni future?una kikomo jama..baada ya ziwa kua gotini,sura kuanza kukunjika,atafanya nini huyu binti na hamkumuandaa ki elimu zaidi?maskini hawa watoto wamekosa wazazi bora poleni sana...mdau,greece

someone needs to stop this madness.Tunaiga @thing mpaka nonsense.Please watanzania wenzangu kemeeni this stupidity.Kids can complete on sports but beuty peagent is a big no no
wapi uzalendo wetu.i WISH Nyerere angerise huko aliko akemee this bs
Mitanzania bado saaaaana.......
 
Mitanzania bado saaaaana.......

Nashangaa na huyo Mbunge na akili zake anafrahia shindano kama hilo jamani Mitanzania bado ipo ovyo ovyo badala ya kuanzisha mashindano ya kuandika Insha, kukokotoa hisabati wao urembo huu urembo utawasaidia nini watoto hawa kama si kuwadumaza kiakili na kuanza kuwaza zawadi za Vogue,Escudo na kisha kukatisha masomo yao si tumeshuhudia wanyange kibao wakisha pata umaarufu na Elimu hawataki tena lakini walio chuja sasa wamefulia wanajuuta kwa nini hawakujiendeleza kielimu. Mitanzania bado
 
Sishangai mitanzania inafulia kwa kila kitu......huyo mbunge nae ni zero tu.....sasa hivyo vitoto vinafundishwa nini? tunaona mtaani mamisss walivyo busy kusaka mapedejee baabda ya kuukwaa umiss na watoto wa siku hizi huwafichi kitu nao akili zao zinaandaliwa kuelekea huko huko......

nchi zenye mamiss wakali kutokea duniani kama Venezuela na india hawafanyi upupu huu....Venezuela wana chuo cha mafuzno ya umiss lakini sio kwa makinda kama hawa.....most wanakuwa ni vigori wametoka vyuoni....

again huu ni upuuzi nikiwa kama mwanajamii mpenda maendeleo nalaani kitendo hiki
 
Sishangai mitanzania inafulia kwa kila kitu......huyo mbunge nae ni zero tu.....sasa hivyo vitoto vinafundishwa nini? tunaona mtaani mamisss walivyo busy kusaka mapedejee baabda ya kuukwaa umiss na watoto wa siku hizi huwafichi kitu nao akili zao zinaandaliwa kuelekea huko huko......

Mpwa hivi waziri wa Watoto ni nani vile tu mtafute anazungumziaje swala hili?
Ndo maana tunako elekea tutakuwa na taifa lenye vilaza wengi badala ya kuchochea Elimu wao wanachochea umiss huu umiss utamsaidia nini mtoto jamani??????? Na wazazi wenye watoto hao wanapaswa kuchukulia hatua za kisheria kwa kuwaruhusu watoto kushuriki hata huyo mbunge nae anapaswa kuwajibika....
 
Mpwa hamna haja ya waziri hapo wala CCM......hapo ni ile mitanzania mivivu kichwani....wazazi vichwani sijui kama watakuwa wazima.....
 
Mpwa hamna haja ya waziri hapo wala CCM......hapo ni ile mitanzania mivivu kichwani....wazazi vichwani sijui kama watakuwa wazima.....

Nimegundua Mitanzania mingi inapenda vitu cheap sana hata mizazi nayo hivyo hivyo inawaza mtoto wangu ukue uwe mrembo au ugombee umiss TZ ili aonekane kwenye media za Bongo ndo ujiko wao.
 
ni kitu cheme kabisa kama tumeshindwa kuwaua mafisadi na bado tunawachagua kuwa viongozi si ni bora tuendelee na taaluma zingine kama hii ya urembo kwa watoo bravoo waandaaji kip it higher.
 
Fatuma Issa (7) ameibuka kidedea katika shindano la kumpata Malkia wa Watoto, Miss Totoz Temeke 2009 katika Ukumbi wa Equator Grill baada ya kuwashinda warembo wenzake 11 katika shindano lililokuwa gumu na la aina yake wakati majaji Mariam Chaheli, Jowalipokuwa wakichuja nafasi ili kumpata mrembo wa Ukweli kwa Watoto wa Wilaya ya Temeke.

Duh!Hii kali..!Kwa hiyo huyo ni miss,kimiss au tumuiteje?

Shindano hilo ambalo lengo lake ni kukuza na kuendeleza Sanaa kuanzia ngazi za chini lilikuwa na mvuto na msisimko mkubwa kutokana na watoto kuchuana vikali kila mmoja akiitaji kuibuka na ushindi na kuweka rekodi ya kwanza katika maisha yake katika shindano hilo, warembo waliobahatika kupanda jukwaani ni pamoja na Janey Anthony, Fatuma Issa, Zaituni Hassan, Neema Ally, Ester Frenk, Ashura Omary,Mariam Karama,Nasra Ally, Yunis Anthony, Angela Silayu,Happy Peter, na Eda Damian.

Yani kabisa wazazi wanakubali kuwaruhusu watoto wao waende kushiriki hayo mashindano?!Its nonesense..Badala wakuze elimu wanakuza urembo,wa kazi gani?Kwani huo urembo ndio ufunguo wa maisha?!
..........

"shindano hili kusema kweli ni la kipekee, ukiwatazama watoto unagundua kuwa pia wanaitaji kupatiwa mafunzo haya ikiwa mapema ili ifikapo wakati wa mshiriki anakuwa apati tabu na pia anakuwa ana tena aibu kama tunavyowashuhudia baadhi ya washiriki wanashindwa hata kujielezea, kujibu swali hata kama siyo gumu, ukweli wengi wao wanakuwa na aibu, hivyo watoto wakianza kufunzwa angali wadogo bila shaka siku zijazo tutakuwa na washiriki wengi wa Urembo"alisema Al-Shymaa

Hamna lolote kwani hao walioshiriki ndo watakuja kushiriki tena badae?Wengine watakuwa vibonge,wengine wafupi na sababu nyinginezo...!This is totally crazy!!!
.......

kikubwa ninawaomba watu mbalimbali kujitokeza kusaidia kufanikisha shindano hili ambalo ni changamoto kwa watoto wetu, ili pia waweze kujitambua umuhimu wao juu ya masuala ya Urembo wakiwa bado wadogo kama ilivyom katika masuala mengine kama mpira wa miguu, na kikapu watoto wanaanza kuelimishwa wakiwa wadogo na hivyo kukua wakijua namna ya kuvitumia Vipaji vyao"alisema Jack

Yani watu waache kuwasaidia watu wasiojiweza wenye matatizo mbalimbali waanze kutoa michango kwa ajili ya hivyo vimiss "its stupidity"

Mshindi wa kwanza katika shindano hilo alizawadiwa TV na Cheni, wa pili na wa tatu Radio na Cheni wa nne na tano walipatiwa cheni kila mmoja, sambamba na washiriki wote kupatiwa vifaa vya shule ikiwamo vitabu, peni, na madaftari ambavyo vyote vilikabidhiwa na mgeni Rasmi Mh. Mbunge Viti Maalum, Al-Shymaa Kwegiar.

Atleast walikumbuka kama kuna vitu vinaitwa vitabu ,madaftari na peni...
Huyo waziri amefulia,yani anaalikwa kwenye mashindano kama hayo na yeye anahudhuria?!
Mbona hao mawaziri hawawi mstari wa mbele kuwasaidia watu wenye shida?!
Watanzania tunazidi kupotea...!
 
Last edited:
Lazima hata wazazi wa watoto walioshiriki oblangata zao zimebunguliwa siyo hivi hivi!!! halafu mtunga sheria ndiye anayekuwa mgeni rasmi!!! hivi huku si kubaka future yao hawa watoto. mawaziri wa utamaduni na michezo na wa jinsia na maendeleo ya watoto wanatakiwa kuwajibika.
kila siku tunalalamika mmomonyoko wa maadili halafu mheshimiwa (mdharauliwa) anakuwa mstari wa mbele kumong'onyoa. uchafu usiomithilika!!!
 
nafikiri lazima tuwe na mtizamo chanya wa mambo haya, hiyo ni sanaa kama nyingine tuu, zamani muziki wa bongo flavour ulikuwa unaonekana uhuni mtupu, lakini sasa huitaji PhD kutambua kama ni ajira inayolipa tuu, what about comedy art, ilpoanza mliwachukulia kuwa ni wehu sasa hivi wanalipa mpaka mameneja wao mishahara.Sanaa ya urembo haimzuii mtoto kusoma na kuelimika, actually in future elimu itakuwa one of the qualifications za kushiriki, hapa sioni tatizo labda kama mna mitazamo ya kizamani
 
Jamani tubadilike, mtoto kuhudhuria mashindano hayo ni sawa na kwenda kuimba kwaya. Cha msingi hapo ni kuyaandaa mashindano hayo yahusishe mambo mazuri, mfano kitu ambacho mimi sija penda ni kutoa zawadi ya TV. Hawa bado ni watoto, TV ya nini badala ya kumzawadia kompyuta au ada ya shule ktk shule fulani nzuri.
 
Ukiwa miss ni marufuku kusoma?

Mara nyingi hawajali elimu. Wengi wa hao so called ma miss kichwani hamnazo kabisa! Ukitaka kugundua kuwa hamnazo, jaribu ku carry conversation na baadhi yao kuhusu mambo mbalimbali ya kidunia kuanzia jiografia, masuala ya afya, uchumi, siasa, michezo na kadhalika. Utagundua kwamba wao wanachojua zaidi ni nani anam date nani na nini kiko in vogue. Zaidi ya hapo zilch, nada, zero.
 
Last edited:
Kitendo hiki cha wazazi kukubali mtoto wako achukuliwe kwenye miss ni ujinga usipimika hata kwa mzani wa aina yoyote.

Hivi kwa hawa watoto kigezo cha ushindi ilikuwa nini mapengo au? Imeniuma sana mimi hata kwa kufulia akili na pesa, siwezi kumtoa mwanangu afanya ujinga kama huu. Tupige vita mawazo ya kijiang kama haya na ikifikia sehemu watuwashitakiwe kwa kosa la kudhalilisha watoto.

Huyu amejifunza nini kutoka kwenye umiss wa kijinga kama huu?? Hapa ndiyo nagundua kuwa wazazi wengi hatutumii akili.
 
Yaani kwa kweli hii nchi sijui tunakwenda wapi, kweli UPEO ni kitu muhimu sana kwa binadamu aliyekamili na mwenye wivu wa maendeleo lakini tulio wengi vichwa vyetu vimeinama kuyaelekeza macho ardhini!! tutasema macho yameona mbali kweli? Hawa watoto masikini wanaongozwa na watu walioelekeza macho yao ardhini!! MUNGU awaokoe na awalaani hao wanaowapotosha, tutaondoa umasikini kwa mashindano ya urembo au shule? Huyu mbunge vipi jamani?
 
kwanza yo yo asante kwa kuweka hii ishu
jamani haya mashindano ya ma miss kwa watoto ni uwendawazimu
hivi hao wazazi wanafikiria nini
je na mmbunge kweli anaona ni sawa kweli kwenda kwenye vitu kama hivyo, basi kazi tanzania tunayo
kwa watu wa nje ya nchi je huko kwenu mliko kuna mashindano ya umisss kama yalivyo tz ????
 
Yapo lakini siyo kila mtu anaya endorse. Watu wengi, kwa makisio yangu wanayalaani.
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom