Mashindano ya kuhifadhi Quran ni moja ya vielelezo vya jinsi dunia ilivyojaa mfumo wa kibaguzi usiokubalika!

The Phylosopher

JF-Expert Member
Mar 11, 2015
1,804
2,721
Mimi ninaamini katika ushindani lakini kuna mambo yanani fanya nione kuna watu kwenye hii dunia mifumo iliyopo imewatenga kabisa.

Ninachoelewa mimi suala la imani kwa Mungu ni la moyo wa mtu binafsi. Ni ngumu sana kubainisha mcha Mungu ama laa.

Kwa habari ya kuhifadhi kurani jambo kubwa linalotawala ni uwezo wa mtu kukaririshwa vitu kichwani jambo ambalo ni matokeo ya uumbaji wa Mungu.

Kwa nini uwashindanishe watu tena jambo lenyewe la dini lakini uwezo wa kuperfom unategemea Mungu majaliwa ya mola!!?

Why ufurahie kwamba nimeshinda wakati akili uliyotumia kushinda ulipewa na aliyewapa uliowashunda!?

Huu mfumo ni wa kibaguzi
Napendekeza watu washindanishwe kwenye vitu ambavyo wana fursa navyo sawa.

Soma: News Alert: - Rais Samia akishiriki tamasha la Mashindano ya Kuhifadhi Quran kwa Wanawake
 
Mimi ninaamini katika ushindani lakini kuna mambo yanani fanya nione kuna watu kwenye hii dunia mifumo iliyopo imewatenga kabisa.

Ninachoelewa mimi suala la imani kwa Mungu ni la moyo wa mtu binafsi. Ni ngumu sana kubainisha mcha Mungu ama laa.

Kwa habari ya kuhifadhi kurani jambo kubwa linalotawala ni uwezo wa mtu kukaririshwa vitu kichwani jambo ambalo ni matokeo ya uumbaji wa Mungu.

Kwa nini uwashindanishe watu tena jambo lenyewe la dini lakini uwezo wa kuperfom unategemea Mungu majaliwa ya mola!!?

Why ufurahie kwamba nimeshinda wakati akili uliyotumia kushinda ulipewa na aliyewapa uliowashunda!?

Huu mfumo ni wa kibaguzi
Napendekeza watu washindanishwe kwenye vitu ambavyo wana fursa navyo sawa.
Nenda kwenye mashindano ya biblia ya waislaam waachie waislaam
 
Japo suala lenyewe la mashindano ya Quran limezungumzwa na baadhi ya wanachuoni wa kiislamu kuwa halifai lakini hoja ya haina mashiko.

Kwa sababu kuhifadhi Quran ni juhudi ambazo mtu anatakiwa kuzifanya ili hiyo Quran ikae kifuani mwake, usidhani ni jambo rahisi bali kuna juhudi kubwa imefanyika.

Ishu sio kuihifadhi, ishu ni kuifanya iendelee kubaki kifuani mwako baada ya kuihifadhi maana inamponyoka mtu kirahisi sana.
 
Kuwa na akili na kutumia akili ni vitu viwili tofauti.
Ni UPUMBAVU kutaka watu wasishindane kwasababu tu aliyeshinda na aliyeshindwa wote wamepewa akili na Mungu yuleyule.
 
Mimi ninaamini katika ushindani lakini kuna mambo yanani fanya nione kuna watu kwenye hii dunia mifumo iliyopo imewatenga kabisa.

Ninachoelewa mimi suala la imani kwa Mungu ni la moyo wa mtu binafsi. Ni ngumu sana kubainisha mcha Mungu ama laa.

Kwa habari ya kuhifadhi kurani jambo kubwa linalotawala ni uwezo wa mtu kukaririshwa vitu kichwani jambo ambalo ni matokeo ya uumbaji wa Mungu.

Kwa nini uwashindanishe watu tena jambo lenyewe la dini lakini uwezo wa kuperfom unategemea Mungu majaliwa ya mola!!?

Why ufurahie kwamba nimeshinda wakati akili uliyotumia kushinda ulipewa na aliyewapa uliowashunda!?

Huu mfumo ni wa kibaguzi
Napendekeza watu washindanishwe kwenye vitu ambavyo wana fursa navyo sawa.
Post ya ajabu...

Shuleni tunashindanishwa kwa kupewa mitihani kwani AKILI HIZO SI ZA UUMBAJI WA MUNGU?!!

Biasharani tunashindana kwani AKILI ZA KUFANYA HAYO SI UWEZO WA UUMBAJI WA MUNGU ?!!

Dada zetu na wake zetu wanashindana USAFI ,UZURI ,WEMA ,MAHONDOMOLO* kwani humo hakuna UWEZO WA UUMBAJI WA MUNGU ?!!

Tunashindana kila eneo....CHADEMA wanashindana na CCM....

Mawazo yako yanatokana na mtazamo wa malezi yasiyonyooka(astray without guidance) ???!!

Mawazo yako yanatokana na uduni wa kutafakari ikiwa unao uwezo wa kutafakari ?!!

Je ni 'IQ" ndogo na kujitutumua mbele za watu kutafuta "kajamba nani ?!!!

Waislamu wasishindane Quran kwa rejea ya fikra zako ?!!

Majumbani tusishindane utunzaji mwema kwa sababu ya fikra zako ?!!

Alijisemea mwanafalsafa Ibn Farabi " Ukinipa kazi ya kuhesabu nyota angani wakati wa usiku mpevu nitakupa idadi yake ndani ya sekunde 1 ila ukinipa kazi ya kuhesabu WENDAWAZIMU katika mgongo wa ardhi ,SIIWEZI...".

NEVER GIVE WISDOM TO UNWORTHY AS IT IS UNJUST TO THE KNOWLEDGEABLE

#Napenda kusoma Quran
 
Kwa sababu kuhifadhi Quran ni juhudi ambazo mtu anatakiwa kuzifanya ili hiyo Quran ikae kifuani mwake, usidhani ni jambo rahisi bali kuna juhudi kubwa imefanyika.

Ishu sio kuihifadhi, ishu ni kuifanya iendelee kubaki kifuani mwako baada ya kuihifadhi maana inamponyoka mtu kirahisi sana.
Kifuani au kichwani??
 
Kifuani au kichwani??
"I do what I do based on how I feel"...MOYO...

Kwa sababu kupenda kuisoma Qur'an kuirudirudia ni mapenzi ya mtu binafsi....hukaririka na ubongo kwa sababu kwanza ulianza MOYO kupenda....

Karibu Al Kasus hapa "dokoa punje umwachie na mwenzio"!!
 
Back
Top Bottom