Mashindano ya African Football League (AFL) hatihati kutokuwepo msimu huu

Jul 15, 2024
19
15
Kama mnayakumbuka yale mashindano ya AFL ,yaliofanyika msimu uliopita apa na yalizinduliwa hapa hapa Tanzania kwa mechi kati ya Simba sc dhidi ya Al ahly sc na mchezo kutamatika kwa sare ya goli 2 kwa 2 .Na bingwa wa mashindano hayo hadi mwisho walikua ni Mamelodi Sundows ya Afrika kusini.
Sasa inasemekana kua huenda mashindano hayo kwa msimu huu yasiwepo!. Na sababu mojawapo kubwa inayozungumzwa ni ufinyu wa ratiba za mashindano yaliyopo kwa msimu huu.
Je wewe ukiwa kama mwanasoka yapi ni maoni yako kulingana na hizi tetesi zilizopo kuhusu haya mashindano ?? Comment yako ni muhimu hapa .
 
Mashindano mengi na FIFA CLUB WORLD CUP imeharibia club za Africa so lazima waebde huko
 
Hayo mashinano yamefutwa sababu ni bonanza ambalo linaharibu ratiba za timu kwenye kucheza mashindano serious.

Pia vigezo vya kupatikana washiriki vina utata.

Na hatua za mbele za bingwa wa hayo mashindano hazieleweki.

Mfano bingwa wa caf champions league anaenda hatua ya mbele ya ku qualify kucheza fifa club world cup. Ila bingwa wa AFL haeleweki anaenda wapi

Bingwa wa shirikisho anaenda kucheza Caf super cup. Ila bingwa wa AFL hana anapoenda zaidi ya kushoshana tu
 
Back
Top Bottom