Mashindano katika Jumuiya ya Afrika Mashariki

mwengeso

JF-Expert Member
Nov 27, 2014
9,227
6,666
Hili nilibandikalo hapo ni wazo tu, kama serikali ya awamu ya tano ya Magufuli, ambaye kwa sasa ndiye m/kiti wa Jumuia, italifanyia kazi.

Kuna mashindano mengi yanayoendeshwa kwenye Jumuia ya Afrika Mashariki japo yaliyo juu sana ni ya mpira wa mguu. Napendekeza kuongeza mashindano yafuatayo, zaidi ya kuweka ukaribu wetu, kutambua na kukuza vipaji kijumuia:
1) Elimu: mtihani wa darasa la saba, sekondari na chuo kikuu.
2) Uchumi: kubuni na kutekeleza miradi ya ujasiriamali ngazi yaTaifa.
3) Uzalishaji: bidhaa bora za kilimo na viwandani
4) Sanaa: kwaya, mziki wa dansi, uandishi, na filamu.

Nawasilisha.
 
wewe unataka tuaibikee "Magufuli usitekeleze aliyoyasema huyu raia wako nakusihi hatutaki aibu!"
 
Hahahaaaa, mbona humu JF huwa tunashuka majamboz ya kujiamini!!
 
kwenye "elimu+uchumi" hapo utasababisha TUPATE AIBU YA KARNE mbele ya wakenya, tutaaibika sana coz wakenya wametuzidi, kataa kubali ukweli ndo huo.
 
Tukubali kuabika kwa nia ya kuboresha pale tulipolegea, au! "Life is but learning".
 
kwenye "elimu+uchumi" hapo utasababisha TUPATE AIBU YA KARNE mbele ya wakenya, tutaaibika sana coz wakenya wametuzidi, kataa kubali ukweli ndo huo.

Elimu kabla na mara baada ya uhuru kulikuwa na mitigani ya CAMBRIDGE kwa nchi zote za Jumuia ya Nadola. Ibawezekana kabisa kuanzisha mitihani ya Jumuia ya Afrika Mashariki kuelekea Taifa moja.
 
Back
Top Bottom