Mashimo ya Choo yasiyojaa ni kama yako Over-Charged hivi

Shark

JF-Expert Member
Jan 25, 2010
29,423
29,084
Wakuu Kwema?

Kuna haya mashimo ya choo wanayosema hayajai. Inawezekana kweli hayajai au yanajaa kwa kuchelewa lakini naona kama yanakuzwa sana Gharama zake. Yaani nikijaribu kuangalia materials yanayotumika kujenga haya mashimo sioni kabisa system moja ya mashimo mawili kugharimu 2Mil +.

Inawezekana kabisa labda sababu yanapendwa sana ndio maana bei zake ziko juu ili wajenzi wapige hela ndefu, lakini kwenye materials halisi ki ukweli nyinyi wajenzi mnakuza sana.

Au kuna mwenye kuelewa why bei za haya mshimo (system) ziko juu wakati bei za mchanga, cement, kokoto, pipes vinajulikana?
 
Kama wanaweza ku-defy logic (yaani unajaza kitu alafu hakijai) basi hata hio pesa wanayochaji ni ndogo... nawashauri waongeze maradufu ili waamie kwenye madampo yasiyojaa... Hapo mwisho wa siku tutaokoa mazingira
Kama utaalamu huo wanao na haugarimu sana wangeweka tu bei ya kawaida
 
Kama utaalamu huo wanao na haugarimu sana wangeweka tu bei ya kawaida
Hapana Mkuu knowledge is Power..., na pesa ni nini zaidi ya kufacilitate kile unachotaka..., kwahio mpaka pale supply itakapokuwa kubwa kuliko demand..., wenyewe watashusha tu.

Ila hakuna kitu ambacho hakijai labda kama kinavuja, hata kama kinayeyuka ukiongeza matumizi (mfano labda ukibadilishe nyumba yako kuwa kanisa au iwe choo cha stendi) nina uhakika kitajaa, unless otherwise wakupe matumizi yasizidi kiasi fulani kwa siku.

Hawa wakikutana na wakorofi wanaweza wakadaiwa fidia kwamba uliniambia hakijai mbona kimejaa.
 
Mimi nilichokifanya, kwanza nilisoma kwa makini na kuangalia video mbalimbali Youtube na kwenye baadhi ya account za instagram za wanaofanya kazi hii.

Ni kweli ukiangalia material wanazotumia na ghalama wanayokupa ni vitu viwili tofauti kabisa. So nilichokifanya mimi ni kumwita fundi anifanyie nnachokitaka (kama nilivyokua nasoma mitandaoni). Na kazi aliimaliza vizuri kwa ghalama isiyozidi laki 8.

Hata hivyo hiyo gharama bado ni kubwa sana kwa kazi wanazozitangaza hao jamaa. Mimi nilijenga mashimo makubwa kidogo ndio maana ikafikia gharama hiyo
 
Sasa kama Utaalamu tayar anao, si angefanya tu kwa hata 200,000 + materials 400,000 ili apate wateja wengi sababu wengi watamudu gharama?
Ndio shida ya wabongo wengi, ni sawa na yule anaeuza kiatu dukani kwa 100,000 wakati anakaa nacho dukani mwaka hakijanunuliwa, wakati mwenzake anauza kwa 60,000 viatu vilevile vinatoka na kwa mwaka anaingiza mzigo dukani mpaka mara 5 au zaidi...
 
Binafsi siamini ile system thou kuna nanmna wananishawishi kwa sasa nataka mwenye ushahidi alietumia ile system kwa miaka walau mitano bila kujaa anirecommend niweke kwenye project yangu.
Its all about physics wala sio uchawi au mazingaombwe. Ipo hivi, haya mashimo kuna namna yanatengenezwa kuchuja maji na taka mwili. Maji taka hunyonywa na ardhi kuelekea chini wakati zile taka mwili hubakia na kuoza na kugeuka wadudu ambao hupotelea ardhini huko na kurutubisha udongo.

But ili yawe effective inatakiwa kujua utaratibu wake wa namna ya kuyajenga. Shimo la nyumbani kwa bi mkubwa lilijengwa 1989 hadi leo hapa naandika, mwaka huu 2021 mwezi February, halijawahi kujaa wala kuvujisha siri za ndani yake.......
 
Daah 89 hadi leo si wanasema ni ya kileo/kisasa? Kumbe tangu zamani yalikuwako? Asante kwa ushuhuda.
 
Similar Discussions

12 Reactions
Reply
Back
Top Bottom