Mashimo ya choo Laki saba au milioni 700? Kuna mtu anadanganya hapa! | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashimo ya choo Laki saba au milioni 700? Kuna mtu anadanganya hapa!

Discussion in 'Uchaguzi Tanzania' started by buckreef, Oct 30, 2010.

 1. b

  buckreef JF-Expert Member

  #1
  Oct 30, 2010
  Joined: Mar 19, 2010
  Messages: 310
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  CAG aagiza tuhuma dhidi ya Dk Kawambwa kuvaliwa njuga

  Saturday, 30 October 2010 (Mwananchi)

  MKAGUZI na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG), Ludovick Utouh, amemwagiza Mkaguzi Mkazi wa Mkoa wa Pwani kuzivalia njuga tuhuma zilizotolewa na mgombea urais wa Chadema, Dk Willibrod Slaa, dhidi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo kwamba ilitumia Sh3.5 bilioni kwa ujenzi wa matundu 20 ya vyoo katika shule tano za msingi.


  Akizungumza katika mahojiano maalum na Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC1) juzi, Utouh alisema ameamua kufanya hivyo kwa kuwa fedha hizo zinatokana na Mpango wa Kuboresha Elimu ya Msingi (MMEM).


  Dk Slaa alitoa tuhuma hizo hivi karibuni katika mkutano wake wa kampeni kwenye viwanja vya Mwembeyanga jijini Dar es Salaa na kwamba, taarifa hizo zimo katika taarifa ya utekelezaji wa ilani ya CCM na ahadi za Mbunge wa Bagamoyo, Dk Shukuru Kawamba, kwa Rais Jakaya Kikwete.

  Kwa mujibu wa Dk Slaa, kila matundu manne ya vyoo katika shule tano za msingi wilayani humo, yalitumia Sh700 milioni na hivyo kufanya fedha yote iliyotumika kujenga matundu 20 ya vyoo kufikia Sh3.5 bilioni, hali inayoashiria ufisadi mkubwa.


  "Bajeti yote ya sekta ya elimu katika Mkoa wa Pwani ni Sh12 bilioni sasa kama Sh3.5 bilioni sawa na asilimia 30 ya bajeti yote inatumika kujenga matundu 20 ya vyoo, nimemwagiza mkaguzi mkazi wa mkoa huo kuzivalia njuga tuhuma hizo katika kazi yake ya mwaka huu," alisema Utouh.


  "Tutalifanyia kazi na baadaye tutakuja na ukweli au uongo wa tuhuma hizo. Tunatarajia ripoti yake itatoka Machi mwakani," aliongeza Utouh.

  Kwa upande wake, Dk Kawambwa ambaye pia ni mgombea ubunge wa Bagamoyo alisema tuhuma hizo ni za uongo na uzushi na zimepangwa.


  "Huo ni uongo na uzushi wa Dk Slaa na watu wake. Hata kitabu alichosoma jukwaani ni cha kwake na sio cha kwangu, cha kwangu kinaonyesha matundu manne ya vyoo yalijengwa kwa Sh700,000," alisema Dk Kawambwa alipozungumza na Mwananchi kwa simu na kuongeza:


  "Dk Slaa ametunga kitabu hicho na kuongeza zero tatu katika Sh700,000 ndio maana akapata Sh700,000,000 kwa kila matundu manne ya vyoo."

  Dk Kawambwa alisema bajeti yote ya sekta ya elimu katika Halmashauri ya Wilaya ya Bagamoyo haifiki Sh3.5 bilioni wakati bajeti yote ya wilaya hiyo katika sekta zote ni Sh21 bilioni.
   
Loading...