#COVID19 Mashetani wanatumia hadi madhabahu ya kanisa kuzuia watu wasipate chanjo ya UVIKO-19

atuchanjwi atuish kwenye akili zako
inategemea unakataa kuchanjwakwa reason ipi, kuna aliyetuaminisha anaevidence za madhara na aliongea na mtengeneza chanjo alipoambiwa atoe ushahidi akamsingizia roho mtakatifu
 
Kwa mwili wa binadamu kufa na roho kuondoka Duniani na kurudi kwenye ulimwengu wa roho kabla ya kutimiza malengo ya Mungu ni furaha ya Shetani.
Andiko lako ni zito sana kwa atakayebarikiwa kuelewa.
Sio lazima mtu ufe kimwili mapema, zipo njia nyingine Shetani na Mawakala wake wanaweza kutumia, mfano kumwingia mtu na kumfanya kuwa kichaa maisha yake yote mpaka anakufa, ulevi wa kupindukia, uteja..
Kuna somo zuri nashauri kulisoma Marko 5: 1-20
 
Wewe tupe evidence kuwa hiyo chanjo ni salama la sivyo ndo wale wale mnaponda bila fact. Unazungumzia shetani wewe una uhakika hiyo chanjo sio mpango wa shetani??

Mashetani wameleta shida duniani halafu wanalaumu madhabahu
 
Asante
View attachment 1926902

SHETANI KAPANDISHA MOLI

Ndugu zangu tupo kwenye ulimwengu ambao shetani anatenda kazi sawasawa, ukiona mtu anasimama kupinga chanjo na hana evidence ya upingaji wake jua sio yeye bali ni mashetani yako kichwani yanamuongoza muhimu tumuombee

mashetani wanataka kuhakikisha mnakufa kwa ujinga wenu maana wao wanajua wanalolifanya


Nyakati hizi za mwisho kumekuwa ni nyakati mbaya na za hatari ambapo kumezuka mafundisho mengi ya uongo na ya mashetani ya kuwazuia watu wasiende hospitalini au kupata dawa za kisayansi kwa kisingizio cha Imani na maombi kwa Mungu kuwa ndio njia pekee inayotosha kutuponya na magonjwa yetu yatupatayo mara kwa mara. Shetani akijua muda wake umeisha na hivyo atataka kuwapoteza hata yamkini walio wateule kwa kuwafanya Kukosa maarifa ya Msingi kama tutakayojifunza kuhusu Ufahamu juu ya uwepo wa Hospitali katika mpango wa Mungu

Hakuna hatari kubwa kama Shetani akija kwa sura ya malaika wa nuru ambapo anakuja kwa kutumia maandiko kwa namna ile ile kama alivyomtokea Yesu nyikani.Vivyo hivyo nyakati hizi shetani amejigeuza na kuwadanganya wengi hata watu usiowadhania hasa waliokoka kwa kuwadanganya kupuuza njia nyinginezo za Mungu katika kutuponya magonjwa yetu kama kutumia dawa chanjo au kwenda hospitali na kuwafanya waamini kuwa kukataa kwenda hospitali au kutumia dawa ndio kuwa na imani kwa Mungu kupitia jina la Yesu kristo

Hivyo imani hizo potofu za kuacha kwenda hospitalini au kuacha kutumia dawa alizozimwaga shetani kwa namna hiyo imepelekea maelfu kwa maelfu ya watu hasa waliokoka kufa kwa kukosa tu maarifa ya kawaida.Na ndio maana leo tunachukua muda tena kujifunza kujua mpango wa mwingine wa Mungu wa kutuponya kupitia hospitali

Ila ni Muhimu kukumbushana kwamba Ni ukweli usiopingika Jina la Yesu lina nguvu kuliko majina yote na Kwa kupigwa kwake Yesu na damu yake kumwagika pale msalabani sisi sote tumepona.Pale tunapoliitia jina la Yesu lina uwezo wa kutuponya magonjwa yote hata yale yaliyoshindikana kwa wanadamu

Ni mapenzo ya Mungu kwamba watu wake wawe na Afya.
Biblia inasema
YOHANA 1:2:- "Mpenzi naomba ufanikiwe katika mambo yote NA KUWA NA AFYA YAKO , kama vile roho yako ifanikiwavyo."

Hospitali zinasimama kutekeleza mpango huu wa Mungu katika kuwatibu wagonjwa na kuwapa Elimu jinsi ya kuwa na Afya njema na kuepukana na maradhi. Bila kuwapo Hospitali mabilioni ya watu wangekuwa wanakufa hovyo hovyo tu bila sababu za msingi. Kwa sehemu kubwa Hospitali zinatekeleza kile ambacho Mungu anakitaka kifanyike, muhimu ni kwamba wanasayansi na watafiti kazi yao imebarikiwa na Bwana

View attachment 1926913

MWANZO 50:2-3:- "Yusufu akawaagiza watumishi wake waganga, kwamba wampake baba yake dawa asioze. Waganga wakampaka dawa Israeli. Siku zake arobaini zikaisha, maana hivyo hutimizwa siku za kupaka dawa. Wamisri wakamlilia siku sabini."

Yusufu alikuwa ni mtu aliyemjua na kumcha Mungu sana. Lakini bado alikuwa na matatibu wake ambao kazi yao ilikuwa ni kumtibu yeye na nyumba yake. Leo tukienda hospitali kuna dawa za maiti anazodungwa ili asioze. Utabibu huu haukuanzia leo ulikuwepo tangu wakati wa Biblia.

View attachment 1926927

WAKOLOSAI 4:14:-"Luka, YULE TABIBU MPENDWA, na Dema, wanawasalimu."
Huyu Luka ni mmojawapo wa waandishi wa vitabu vitakatifu vya Mungu, Injili ya Luka na Matendo kwenye Neno la Mungu. Mungu asingeweza kumchagua mtu anayefanya kazi isiyompendeza. Biblia inampotaja Luka pamoja na kazi yake ya udaktari (utabibu). Bila shaka Kuna kusudi maalumu ambalo neno la Mungu linataka kutufundisha kwamba KAZI YA UTABIBU MBELE ZA MUNGU INAKUBALIKA. Na kama inakubalika basi kwenda hospitali ni sehemu ya mapenzi ya Mungu kwa watu waliookoka.

Hivyo tukishakuufahamu ukweli huu wa kibiblia kuhusu mpango wa Mungu wa kutumia hospitali katika kutuponya,Hivyo asiwepo mtu awaye yote atakayedanganyika na mafundisho haya ya mashetani yanayozagaa kuwakataza watu kutumia dawa au kwenda hospitalini kusikiliza ushauri wa madaktari

Wengi wao wanaojifanya wanakataa kwenda hospitali kwa madai wana imani kubwa kwa Mungu, waulize , Je wameitumiaje imani yao hiyo kubwa kuwaleta watu wengi kwa Yesu(Mpaka sasa wana watu wangapi wamewaleta na kuwasimamisha kwa Yesu?)? Waulize, Je wameitumiaje imani yao hiyo kubwa kuleta suluhu ya magonjwa mazito kama Ukimwi au Corona ambayo yametikisa dunia(Yaani ni wangapi wameponya magonjwa hayo makubwa kwa ishara na ajabu za kutisha kupitia hizo imani zao?).? Utagundua ni maneno tu ya mdomoni yanayotaja uweza wa Mungu lakini hakuna matokeo yeyote makubwa waliyofanya kupitia imani hizo wanazozisema wanazo.Nguvu ya ukiri na imani inaambatana na matokeo ya wazi yakudhihirika katika mwili
 
Kwani watu waliochanja mna kiherehere sana? Wewe umeshachanja na unadai upo salama piga kimya.
 
Hata mimi nimeyaona mashetani manne hapo juu... hivi na hili la chini hapo ndilo baba yao la mashetani, mbona limeungua hivyo? Au lina kansa ya misuli maana naona mifupa ya kiunzi tu
 
Hata mimi nimeyaona mashetani manne hapo juu... hivi na hili la chini hapo ndilo baba yao la mashetani, mbona limeungua hivyo? Au lina kansa ya misuli maana naona mifupa ya kiunzi tu
🤣🤣🤣
 
Halafu mkuu hiyo hapo nyuma ya mashetani iliyoko kama tufe hivi bila shaka ndo "madhabu" yenyewe, au siyo?
 
Sisi ni kina nani hasa hata twende kinyume na matakwa ya mwenye Dunia yake? Yeye kasema siku hizi za mwisho watu watarudi katika ujinga na watakao nusurika ni wale watakao fuata neno lake na mitume yake.

Tusipoteze nguvu nyingi kuwajadili hawa ambao Mwenye Dunia yake alishawapa kibali cha moto na tujikite katika ibada za kweli ili tuwe miongoni mwa wale watakao Kaa kuliani kwa Bwana.
amina
 
Aseee kumbe kuna watu ni vichekesho😂😂,,Hivi mtu kbsa unaweka ma-alien ya Avatar,,duuuh!
 
Back
Top Bottom