Mashemeji zangu mambo vipi? Ebu pitieni hapa kidogo Ili twende sawa

Heloo

JF-Expert Member
Apr 3, 2012
4,227
2,000
Nashukuru kama wote wazima,

Leo naomba nitete na shemeji zangu wapendwa.

Ninyi ni mashahidi vilio vya mahusiano na pia kwenye ndoa vimekuwa vingi sana. Na kama nilivyotangulia kuwaasa wanawake wenzangu Si vibaya sana pia nikageukia Na kwenu shemeji zangu.

Kwanza kabisa naomba nitoe pongezi kwa walioelewa uzi wa kwanza kuhusu mahusiano jinsi ya kunusuru hali, lakini ikielekeza zaidi kwa wanawake na wadada kwa ujumla.

Mmeona jinsi akina Mrs. Air, Espy, Ulweso na wengi wengi walivyofunguka. Nilifurahishwa na nimefurahishwa na mjadala ule unaoendelea hii imetoa picha halisi jinsi tunavyoishi majumbani mwetu na wapenzi.

Nini kinawakera wadada/wamama na kama kweli ewe shemeji yangu unapenda amani na ndoa yenye furaha utakuwa umechota kitu toka kwa wanawake/ wadada wote waliochangia, kwani hali ndivyo ilivyo majumbani mwetu. OK. Sasa Leo zamu yenu. Naomba nanyi mjitahidi yafuatayo lengo ni kujenga na si kubomoa huu ni ushauri tu.

1.Jitahidi sana kumjali mkeo/, mpenzi wako kwa nyakati zote za maisha yenu. Kwa maana wakati wa uzima na ugonjwa. Tumeshuhudia mke/mpenzi anaumwa Baba yupo busy na Moira wa Ulaya, au na michepuko. Hii hupunguza mapenzi.

2.Mheshimu mpenzi, mke wako mfanye malkia wako. Hii ni kutokumfokea mbele za watu akikosea subiri wakati wa usiku mkiwa peke yenu chumbani utamkanya.

3.Zawadi. Hakikisha miezi 3 haipiti hujamzawadia kitu chochote mpenzi, iwe kanguo, kiatu, au chochote hata nguo ya ndani, hii huimarisha sana mahusiano.

4.Mridhishe mkeo kitandani. Nature ya mwanaume huridhika haraka na inawezekana ikawa automatically, lakini Mara nyingi ninyi mashemeji, hamu yenu ikiisha basi unageukia upande wa pili.Unamwacha mama/mpenzi na hamu.Hii huzaa chuki.

5.Epuka kumyanyasa mke/mpenzi. Hii inachangia sana mapenzi ndani ya nyumba kupunguza. Mfano. Unaanza kuchelewa kurudi, unaongea na wanawake wa nje bila kificho kwa Simu, huoni maumivu yake. Kumbuka mpenzi/mke anakupikia anafanya mengi mazuri.Mthamini.

6.Mkeo/ mpenzi wako huyo kawaacha wengi kakubali kuwa na wewe kwa shida na raha, wengine mnakuwa hata kujijenga bado anakuvumilia, anahatarisha mpaka uhai wake kwa kukuzalia watoto watakaochukua jina lako. Mwanamke ni kitu cha thamani sana.Hakikisha anakuwa na furaha wakati wote.

7.Muamini mkeo. Inatokea una miradi, viwanja au mali mbalimbali mshirikishe awe ni sehemu ya kila kitu chako, asiwe mke jina tu. Lenu ni moja ndo maana ukawa naye, ukamuamini.

8.Uvumilivu. Naomba Mungu akujalie uvumilivu, imetoka mkeo /mpenzi kachelewa kuzaa anzeni utaratibu wa kwenda kwa wataalamu wa afya usianze kumnyanyasa na kuanza kutafuta michepuko. Huenda tatizo ni lako. Kuna ile dhana mbona mimi nina mtoto tayari kwingine. Hapana Huwa Inatokea kutokana na mazingira na vyakula homons kuchange.

9.Jitahidi sana unapoamua kuanza kuishi na mkeo au mpenzi wako. Ndugu wasije kukaa na ninyi nyumba moja hata kama wanakuja iwe ni wa kuja na kuondoka, epuka kumuweka mama mzazi nyumba moja na mkeo hata kama unampenda sana labda kwenye ugonjwa. Tafiti zinaonyesha mwanzo wa migogoro ni hayo. Ndugu wake watembee ila wasihamie.

10.Wote mnatakiwa kukimbilia ibadani. Asiachwe mama pekee!
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom