Mashemeji huwa ni wapambe sana, wapambe nuksi

Tatizo kubwa la nchi yetu, na kwa kweli mataifa yote duniani, ambalo ni chimbuko, msingi na shina la matatizo mengine yote ni UJINGA, MARADHI na UMASKINI. Ujinga na Maradhi ni baba na mama, Umaskini ni mtoto wao mpendwa^ ~ Baba wa Taifa.
Leo nimekuelewa sana wee mbogamboga kwa mtu mzito hawezi kuelewa jambo hapa. Ila umeamdika very brief. Ujinga wetu unatupelekea ujuaji sana. Vijana kujiina wajaanjaaaa...

Shkamoo ndugu yangu.
 
Kuna faida kubwa maana siku nyingine atakupigia pande yeye
Mi sihitaji kupigiwa pande na mtu yeyote, ngoma yangu naicheza mwenyewe.... halafu nnavojua huo upambe wa mashemeji wala sinaga muda nao, hata ikitokea tumeshibana ni marufuku kuleta upambe, story zihusu mambo mengine tu.
 
Wanaume hatutoi siri hovyo za michepuko ya jamaa yetu kwa shemeji mkubwa. It's our rule as men. Ukiona mtu anakupakupa dondoo za mahusiano ya Mr wako basi jua anatafuta kamseleleko kwako

Sent from my SM-A115F using JamiiForums mobile app
 
Kwenu mashemeji...

Hadi sasa hajatokea bado mtu wa kuivunja rekodi ya mashemeji kwa upambe, mashemeji ni wapambe sana yani ni wapambe nuksi. Halafu tabia zao zinavyofanana unaweza kudhani lilikusanywa kundi la watu wakawekwa pamoja wakaambiwa nyie mtaitwa shemeji na tabia zenu zitakua hizi.

Hawa mashemeji ni marafiki, au ndugu wa boyfriend/mme.

Tabia zao: (upambe wao)

1. Wapo ambayo huwa wanakuaga ni wambea, hawa utakuta kila kinachofanyika kwa mhusika basi anakua anakipenyeza kimbea mbea kwa mwanamke mfano labda mwanaume ana kadem kengine basi shemeji analeta upambe upambe kudokeza dokeza ili ujue, au sometimes kusema kabisa hawa shemeji wako na umama.

2. Wapo ambao sio wambea, mioyo ina kufuli ila wapambe mnoooo unakuta mwenye mzigo ana wanawake labda watatu x,y and z shemeji anawajua wote na kote anajifanya kapaelewa akienda kwa x, shem yani jamaa anakupenda sijui umempa nini (kama mwanamke ni zombi basi ndio kujikuta chautamu). Akienda kwa y shem yani siku ukimuacha jamaa atajiua. Anamalizia kwa z, shem jamaa hawezi kuishi bila wewe....khaaa shemeji nyie ni nyk.

3. Shemeji mlinzi, hii tabia ni karibia ya wote, siipendi, labda yupo na jamaa akimaliza kuongea na mtu wake kwa simu shemeji anapewa simu asalimiee cha kwanza kwa shemeji kukisikia ni "mambo shem usijali tunakulindia"

4. Kubwa kuliko ukijichanganya tu kuwashirikisha migogoro mashemeji utasikia, Mungu wangu mbona jamaa anafanya hivi, kwani kakosa nini kwako hadi anafanya hivi kwa mwanamke kama wewe, yani mi namuomba Mungu anipe mwanamke kama wewe sipati, hapa shemeji anaanda ROAD TO MASIHARA, pia wana ukenge wa kunyapia nyapia weka mbali hawa!!!

Shemeji kwanini nyie ni wapambe?
Mbona hizi ni kama tabia za mawifi??
 
Back
Top Bottom