Mashemeji huwa ni wapambe sana, wapambe nuksi

Evelyn Salt

JF-Expert Member
Jan 5, 2012
63,592
112,649
Kwenu mashemeji...

Hadi sasa hajatokea bado mtu wa kuivunja rekodi ya mashemeji kwa upambe, mashemeji ni wapambe sana yani ni wapambe nuksi. Halafu tabia zao zinavyofanana unaweza kudhani lilikusanywa kundi la watu wakawekwa pamoja wakaambiwa nyie mtaitwa shemeji na tabia zenu zitakua hizi.

Hawa mashemeji ni marafiki, au ndugu wa boyfriend/mme.

Tabia zao: (upambe wao)

1. Wapo ambao huwa wanakuaga ni wambea, hawa utakuta kila kinachofanyika kwa mhusika basi anakua anakipenyeza kimbea mbea kwa mwanamke mfano labda mwanaume ana kadem kengine basi shemeji analeta upambe upambe kudokeza dokeza ili ujue, au sometimes kusema kabisa hawa shemeji wako na umama.

2. Wapo ambao sio wambea, mioyo ina kufuli ila wapambe mnoooo unakuta mwenye mzigo ana wanawake labda watatu x,y and z shemeji anawajua wote na kote anajifanya kapaelewa akienda kwa x, shem yani jamaa anakupenda sijui umempa nini (kama mwanamke ni zombi basi ndio kujikuta chautamu). Akienda kwa y shem yani siku ukimuacha jamaa atajiua. Anamalizia kwa z, shem jamaa hawezi kuishi bila wewe....khaaa shemeji nyie ni nyk.

3. Shemeji mlinzi, hii tabia ni karibia ya wote, siipendi, labda yupo na jamaa akimaliza kuongea na mtu wake kwa simu shemeji anapewa simu asalimiee cha kwanza kwa shemeji kukisikia ni "mambo shem usijali tunakulindia"

4. Kubwa kuliko ukijichanganya tu kuwashirikisha migogoro mashemeji utasikia, Mungu wangu mbona jamaa anafanya hivi, kwani kakosa nini kwako hadi anafanya hivi kwa mwanamke kama wewe, yani mi namuomba Mungu anipe mwanamke kama wewe sipati, hapa shemeji anaanda ROAD TO MASIHARA, pia wana ukenge wa kunyapia nyapia weka mbali hawa!!!

Shemeji kwanini nyie ni wapambe?
 
Tatizo kubwa la nchi yetu, na kwa kweli mataifa yote duniani, ambalo ni chimbuko, msingi na shina la matatizo mengine yote ni UJINGA, MARADHI na UMASKINI. Ujinga na Maradhi ni baba na mama, Umaskini ni mtoto wao mpendwa^ ~ Baba wa Taifa.
 
Boys will be boys..

Yaani kama kuna mwanamke anafikiri rafiki wa mume wako au Ndugu yake wa kiume..
Atakuja eti kumzuia Ndugu yake asichepuke basi huyo mwanamke akapimwe akili...

Kila mwanaume ni mfalme kwenye himaya yake... Hatuelekezani namna ya kuendesha ufalme wake..mtu akiamu kuwa na michepuko 20 ni yeye...

Binafsi katika kesi sitaki kusikia ni mdada aje kwangu eti mdogo wangu au Kaka yangu au rafiki ana michepuko...hayanihusu mkishindwana achananeni Tu bila kuhusisha wengine
 
^Tatizo kubwa la nchi yetu, na mataifa yote, ambalo ni chimbuko, msingi na shina la matatizo mengine yote ni UJINGA, MARADHI na UMASKINI. Ujinga na Maradhi ni baba na mama, Umaskini ni mtoto wao mpendwa^ ~ Baba wa Taifa.
Jifunze kuinjoi part zote za haya maisha, kuna siasa kuna mapenzi na fujo nyingine kibao....karibu Shemeji
 
😂😂😂 mashemejiiiiiii kuishi nao kinafiki tu,, kwa sasa mahusiano yangu huwa Ni mimi, hisia zangu, mwili wangu na akili yangu, sihitaji ushauri wala upambe, na ukiuleta utarudi nao sitakagi ushambenga kwenye maisha yangu mimi
 
Boys will be boys..

Yaani kama kuna mwanamke anafikiri rafiki wa mume wako au Ndugu yake wa kiume..
Atakuja eti kumzuia Ndugu yake asichepuke basi huyo mwanamke akapimwe akili...


Kila mwanaume ni mfalme kwenye himaya yake...
Hatuelekezani namna ya kuendesha ufalme wake..mtu akiamu kuwa na michepuko 20 ni yeye...

Binafsi katika kesi sitaki kusikia ni mdada aje kwangu eti mdogo wangu au Kaka yangu au rafiki ana michepuko...hayanihusu mkishindwana achananeni Tu bila kuhusisha wengine
Ishu sio kuzuia wala kulinda, ila ule upambe upambe wa kijinga, msome senorita hapo utaelewa vema boss
 
Kwenu mashemeji.....

Hadi sasa hajatokea bado mtu wa kuivunja rekodi ya mashemeji kwa upambe, mashemeji ni wapambe sana yani ni wapambe nuksi. Halafu tabia zao zinavyofanana unaweza kudhani lilikusanywa kundi la watu wakawekwa pamoja wakaambiwa nyie mtaitwa shemeji na tabia zenu
Hao ni mashemeji wa mume, hebu siku moja ututafutie na tabia za mashemeji wa mume hasa wale wa kike ndio utashangaa vizuri. Yaani rafiki au ndugu wa kike wa mke au girlfriend.
 
Back
Top Bottom