Masheikh walaani vurugu za kidini:Wasema fujo si mafundisho ya dini;Wawaonya wanasiasa kutojitumbuki | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masheikh walaani vurugu za kidini:Wasema fujo si mafundisho ya dini;Wawaonya wanasiasa kutojitumbuki

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by nngu007, Oct 22, 2012.

 1. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #1
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145
  JUMATATU, OCTOBA 22, 2012 05:57 NA KHAMIS MKOTYA


  *Wakemea tabia ya kutoheshimu sheria
  *Wasema fujo si mafundisho ya dini
  *Wawaonya wanasiasa kutojitumbukiza

  TAASISI ya Masheikh na Wanazuoni wa Kiislamu Tanzania, imelaani vurugu za kidini zilizoibuka hivi karibuni na kusababisha hofu kubwa kwa jamii.

  Taasisi hiyo pia imewataka wananchi kuzingatia utawala wa sheria na kusisitiza kuhusu umuhimu wa kujenga utamaduni wa kuheshimu mamlaka za kisheria.

  Tamko hilo lilitolewa na Katibu Mkuu wa taasisi hiyo, Sheikh Khamis Mataka, wakati akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana.

  Sheikh Mataka alisema, taasisi yake imesikitishwa na vurugu hizo, ambazo zimechafua sifa ya dini ya Kiislamu, kuonekana kama dini ya fujo na vurugu.

  Sheikh Mataka alisema, Uislamu ni dini ya upendo na amani na kwamba, kupinga amri za mamlaka za kisheria ni kupinga amri za Mwenyezi Mungu.

  Sheikh Mataka alisema, taasisi yake imesikitishwa na kitendo cha Kur-ani kunajisiwa na kusema kuwa, vurugu zilizojitokeza ni matokeo ya Jeshi la Polisi kuchelewa kuchukua hatua.

  Masheikh hao, walikutana kutafakari afya ya jamii kufuatia kunajisiwa kwa Kur-ani na ghasia za uchomaji wa makanisa eneo la Mbagala, jijini Dar es Salaam.

  "Taasisi ya Masheikh imesikitishwa na mhemko hasi na ghadhabu za baadhi ya Waislamu, zilizopitiliza na kuvuka mipaka.

  "Ghadhabu hizi zimetoa mwanya wa kutendeka uhalifu wa aina mbalimbali, ikiwamo kuchoma kanisa na kuharibu mali za watu wengine.

  "Hayo si mafundisho ya dini ya Kiislamu, kwani Uislamu hauruhusu mlalamikaji kujipa haki ya kuhukumu na kuadhibu.

  "Hisia ikija dini inakutaka kulipokea jambo hilo kwa upole bila kukurupuka, tolerance (uvumilivu) inatakiwa, jazba haitakiwi katika dini.

  "Taasisi ya Masheikh pia imesikitishwa na baadhi ya Waislamu wenzetu, kutumia mikusanyiko isiyohalali kupingana na Jeshi la Polisi kwa shinikizo la kutaka kuachiwa watuhumiwa walio katika mikono ya Dola.

  "Taasisi ya Masheikh, pia imesikitishwa na baadhi ya askari waliotumia vibaya ruhusa ya kutumia nguvu kubwa katika kuzima fujo bila kuzingatia mazingira na shughuli za kijamii," alisema.

  Katika mkutano huo, Sheikh Mataka aliwaonya na kuwataka wanasiasa, kutotumia vurugu hizo kama mtaji wa kisiasa, kwani kufanya hivyo ni hatari kwa amani ya nchi.

  Sheikh Mataka alisema, machafuko ya kidini ni mabaya zaidi kuliko machafuko mengine yakiwamo ya kisiasa, ukabila na ukanda na kuwataka viongozi kukemea kwa nguvu zote.

  "Taasisi ya Masheikh inawatahadharisha wanasiasa, kujiepusha kwa namna moja au nyingine kubariki vurugu za vikundi vya kidini, waache kutoa ushawishi.

  "Wanasiasa watuletee sera zao, ilani za vyama vyao na mikakati ya kujenga uchumi wa nchi, hatutaki watuletee dini zao, kabila zao wala kanda zao, haya yatatugawa zaidi badala ya kutuungunisha," alisema.

  Baadhi ya waandishi wa habari, walitaka kujua msimamo wa taasisi hiyo, kutokana na uwamuzi wa Serikali wa kupiga marufuku mihadhara ya kidini kwa kipindi cha mwezi mmoja.

  Waandishi hao wa habari walitaka kujua iwapo Masheikh hao wanakubaliana na uwamuzi huo, ambao unaweza kutafsiriwa kuwa unalenga kuzuia kueneza dini.

  "Sisi hatuoni tatizo juu ya uwamuzi huo, kwani Serikali haijafunga misikiti wala makanisa, kwa hiyo ibada zinaendelea na shughuli za kueneza dini kupitia nyumba za ibada zinaendelea.

  "Kilichopigwa marufuku ni mikutano ya nje, kama makanisa, misikitiki na nyumba nyingine za ibada zingefungwa, hapo pangekuwa na tatizo, lakini kwa sasa tatizo hakuna," alisema.

  Sheikh Mataka aliandamana na masheikh wengine akiwamo Mwenyekiti wa taasisi hiyo, Sheikh Mohamed Mtulia na wajumbe wengine, Sheikh Mohamed Iddy Mohamed, Hassan Hassanoo na Salim Said.


   
 2. nngu007

  nngu007 JF-Expert Member

  #2
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 2, 2010
  Messages: 15,871
  Likes Received: 56
  Trophy Points: 145

  Ndio Masheikh tunaowataka; Wanajua ELIMU ya DUNIA na DINI... Kwahiyo Kama ni MATAKWA ya WAISLAMU ni kufuata SHERIA kuyadai...
   
 3. Masanilo

  Masanilo JF-Expert Member

  #3
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 2, 2007
  Messages: 22,303
  Likes Received: 168
  Trophy Points: 160
  Bravo sheikh Mataka
   
 4. Money Stunna

  Money Stunna JF-Expert Member

  #4
  Oct 22, 2012
  Joined: Aug 9, 2011
  Messages: 13,105
  Likes Received: 284
  Trophy Points: 160
  mim ninachoamin dini zote uislam na ukristo tunaamin kwenye upendo na amani,hao wauni wachache ponda na wenzake inabid washugulikiwe ipasavyo kwa kuhatarisha amani ya nchi
   
 5. grndossy

  grndossy JF-Expert Member

  #5
  Oct 22, 2012
  Joined: Apr 20, 2011
  Messages: 311
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 0
  Tunatamani viongozi wote wa kidini waseme kwa ujasiri hivi ila wakisema tukiwatazama tuwaamini kwamba wanachosema ni kweli. Mbarikiwe sana.
   
 6. A

  Amri kuu ni Upendo JF-Expert Member

  #6
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 18, 2012
  Messages: 310
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Waaooo!!
   
 7. Mlaleo

  Mlaleo JF-Expert Member

  #7
  Oct 22, 2012
  Joined: Oct 11, 2011
  Messages: 9,863
  Likes Received: 3,308
  Trophy Points: 280
  Hasanoo naye ni mtu wa maono? madawa ya Kulevya kaacha kuuza? hii mikutano yao kama salim Said naye yumo basi watakuwa wamefanya na kuandaa hayo maneno pale The Chef Pride Salim Said namuomba awe ni mfadhiri tu asijiingize kwenye mambo haya Afanye biashara zake tu haya mambo yatamvurugia biashara zake... kwani kuna watakao pokea haya kwa hisia tofauti tofauti... hawa mashehe awatafutie Office na sio kwenye hotel yake
   
Loading...