Uchaguzi 2020 Masheikh wa BAKWATA waanza kumpigia Kampeni Dkt. Magufuli waziwazi bila aibu

Sijui tumefikaje hapa?! Viongozi wa dini kutumika kufanya siasa, hiki ni kiwango kikubwa kabisa cha kufilisika sera na kuamua kutumia ushawishi wa imani kupata wafuasi wa siasa.....


Hili linahitaji kujadiliwa kwa kina...
 
Umewaona Wazee wa Gambosh walivyomtunuku manyanga Mhe Tundu Lissu pale Bariadi
Si walisema mtu atakae jitokeze kushindana na Magufuli atakufa nao walikua tayari kummaliza au kumpoteza kabisa huku DC wa Bariadi Bwn.Kiswaga Festo akisema nae yupo pamoja nao
 
Hawana tofauti na umoja wa wanawake wa CCM,hilo ni tawi maslahi la ccm,wamejificha humo wanafiki kibao.
 
Mbona mnashangilia Sheikh Ponda aliposema Waislamu wote wamchague Lissu. Je Ponda siyo kiongozi wa dini? Kumbe mkuki kwa nguruwe.
Kuna Waislam hawawaungi mkono Ponda wala Bakwata . Mmoja wapo katika hao Waislam ni mimi.
 
Katika kile kinachoonekana ni unafiki wa dhahiri wa BAKWATA, Masheikh wa BAKWATA wameanza kutumia podium mbalimbali za hadhara kumfanyia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Wiki kadhaa zilizopita Sheikh wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam bwana Alhadi, alionekana kung'aka na kumshambulia Muinjilisti Mwingira kwa madai kuwa anafanya kampeni madhabahuni, lakini haikupita hata miezi mitatu Sheikh huyo anasimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kutumia jina la dini kumpigia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Tofauti na Askofu Bagonza na Mwamakula ambao wao huombea mikutano bila ya kuwaambia wananchi wamchague nani, huyu sheikh wa BAKWATA wa Dar es salaam amekwenda mbali na kupiga kampeni kabisa kuuombea kura mgombea huyo wa CCM.

Wakati huohuo, Sheikh huyo wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam amewashangaza sana Waislamu kwa kwenda kinyume kabisa na Imani ya dini ya dini hiyo kwa kufanya maombi kwa jina la Yesu kitu ambacho ni marufuku na ni kufuru kubwa sana kwa mujibu wa dini hiyo. Katika dini ya Uislamu inapaswa kuomba kwa Jina la ALLAH(Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi) peke yake na si kwa jina la Kiumbe yeyote hata awe nabii au hat Malaika. Kwa mujibu wa dini ya Kiisamu Yesu ni nabii na Siyo Mungu.

Kauli hiyo imedhihirisha kuwa Sheikh huyo anaweza kufanya lolote hata kufanya kufuru ya wazi ilimradi awe karibu na watawala.

Kitendo cha Sheikh Alhadi kusema kuwa anaomba kwa jina la Yesu, kisha baadae kutamka Bismillah Rrahmaani rrahiim (yaani kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema) anaimply kuwa Jina la Allah ndiyo Jina la Yesu kitu ambacho ni kufuru kubwa sana kwa muislamu kuifanya.

Matendo haya ya BAKWATA kushindwa kulinda misingi ya dini ya uislamu yanaendelea kujitokeza mara kwa mara na yamekuwa yskiwakera waislamu wengi.

Ni wajibu wa Sheikh Mkuu na waislamu kiujumla kuchukua hatua maana hii tabia ya Masheikh hawa kuvunja misingi ya waziwazi ya dini ya kiislamu kwa sababu ya maslahi machache ya dunia yatapotosha watoto wa kiislamu na waislamu wengine kuikosa Tawhidi ya kweli.

Kama Alhadi alidhani waislamu watampa kura mgombea wa CCM kwa kufanya kufuru ya wazi namna hii basi ndiyo kwanza kamharibia!


 
Back
Top Bottom