Uchaguzi 2020 Masheikh wa BAKWATA waanza kumpigia Kampeni Dkt. Magufuli waziwazi bila aibu

mdudu

JF-Expert Member
Feb 6, 2014
3,296
2,000
Mleta post kichwa cha habari kingesomeka hivi,

Mashekh wa CCM wampigia debe mgombea wa CCM.
 
Chapa Nalo Jr

JF-Expert Member
Dec 8, 2010
7,245
2,000
Huyu Sheikh ni Mnafiki sana. Hata Bashite kwa sasa amemuelewa kuwa jamaa ni mnafiki. As of now is no longer with Bashite. Kuna video alionekana akimkandia Bashite baada ya kuachia u RC.

Huyu mbele ya pesa na ubwabwa, hata nguo anamvulia me mwenzake
 
HesabuKali

JF-Expert Member
Jan 4, 2016
2,135
2,000
Katika ukombozi unaotakiwa kufanyika ni Waislamu kuifuta Bakwata, hakuna aibu kubwa tunapata waislamu kama kuwa na chombo kinachoitwa Bakwata ambayo imesheheni wajinga wengi, yaani asilimia zaidi ya 90 ya viongozi wa Bakwata ni STD 7.

Kwanza uislam haujakataza kupata Elimu ya dunia, lakini kitendo cha safu ya uongozi wa Bakwata kwa ukubwa wake kuongozwa na mbumbumbu tena ushahidi upo hata huo upande wa dini hawa watu ni weupe kichwani kabisa..ni dharau kubwa kwa Waislam.

Na serikali imeamua kukumbatia hiki kikundi cha wajinga kwani kama baraza hili litabadili muundo wake na kuongozwa na wasomi kama yalivyo mabaraza mengine ya dini za kikristo basi CCM itakuwa imekosa kikundi chao cha wajinga cha kuwapigia kampeni.
Kuna sababu gani mtu kama Alhadi Mussa kuwa Sheikh Mkuu wa mkoa wa Dar?

Aibu tunaipata sisi na mkijaribu kufanya mabadiliko serikalini lazima iingilie kati ili hiki kikundi cha wajinga kiendelee kubaki.
 
julaibibi

JF-Expert Member
Jun 16, 2020
331
250
Missile nation umekosea.Mimi pia nilisikiliza hio dua.kama huelew dua zinavyoombwa rudi ukae chini ufanye research yako vizuri. usifikri shekh mkubwa kama yule alivamia tu kuomba dua .
 
Missile of the Nation

JF-Expert Member
May 24, 2018
7,587
2,000
Missile nation umekosea.Mimi pia nilisikiliza hio dua.kama huelew dua zinavyoombwa rudi ukae chini ufanye research yako vizuri. usifikri shekh mkubwa kama yule alivamia tu kuomba dua .
Hakuna muislamu anayeomba dua kwa jina la Yesu au Jibril au hata Muhammad. Kufanya hivyo ni kufuru kubwa.

Dua kwenye Uislamu inaombwa kwa jina la Allah peke yake.

Sasa kama Alhadi amempokea Yesu kuwa BWANA na muokozi wake aache kujifanya muislamu
 
Mwangwi

Member
Dec 30, 2017
94
125
Missile nation umekosea.Mimi pia nilisikiliza hio dua.kama huelew dua zinavyoombwa rudi ukae chini ufanye research yako vizuri. usifikri shekh mkubwa kama yule alivamia tu kuomba dua .
Usimtetee Alhad. Alhad kakosea. Halafu kwa hayo maneno yako ya mwisho unatakiwa uzingatie haya; "Ijue Haqq, utawajua walio katika Haqq".
 
nguvu

JF-Expert Member
Jun 13, 2013
8,924
2,000
Katika kile kinachoonekana ni unafiki wa dhahiri wa BAKWATA, Masheikh wa BAKWATA wameanza kutumia podium mbalimbali za hadhara kumfanyia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Wiki kadhaa zilizopita Sheikh wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam bwana Alhadi, alionekana kung'aka na kumshambulia Muinjilisti Mwingira kwa madai kuwa anafanya kampeni madhabahuni, lakini haikupita hata miezi mitatu Sheikh huyo anasimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kutumia jina la dini kumpigia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Tofauti na Askofu Bagonza na Mwamakula ambao wao huombea mikutano bila ya kuwaambia wananchi wamchague nani, huyu sheikh wa BAKWATA wa Dar es salaam amekwenda mbali na kupiga kampeni kabisa kuuombea kura mgombea huyo wa CCM.

Wakati huohuo, Sheikh huyo wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam amewashangaza sana Waislamu kwa kwenda kinyume kabisa na Imani ya dini ya dini hiyo kwa kufanya maombi kwa jina la Yesu kitu ambacho ni marufuku na ni kufuru kubwa sana kwa mujibu wa dini hiyo. Katika dini ya Uislamu inapaswa kuomba kwa Jina la ALLAH(Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi) peke yake na si kwa jina la Kiumbe yeyote hata awe nabii au hat Malaika. Kwa mujibu wa dini ya Kiisamu Yesu ni nabii na Siyo Mungu.

Kauli hiyo imedhihirisha kuwa Sheikh huyo anaweza kufanya lolote hata kufanya kufuru ya wazi ilimradi awe karibu na watawala.

Kitendo cha Sheikh Alhadi kusema kuwa anaomba kwa jina la Yesu, kisha baadae kutamka Bismillah Rrahmaani rrahiim (yaani kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema) anaimply kuwa Jina la Allah ndiyo Jina la Yesu kitu ambacho ni kufuru kubwa sana kwa muislamu kuifanya.

Matendo haya ya BAKWATA kushindwa kulinda misingi ya dini ya uislamu yanaendelea kujitokeza mara kwa mara na yamekuwa yskiwakera waislamu wengi.

Ni wajibu wa Sheikh Mkuu na waislamu kiujumla kuchukua hatua maana hii tabia ya Masheikh hawa kuvunja misingi ya waziwazi ya dini ya kiislamu kwa sababu ya maslahi machache ya dunia yatapotosha watoto wa kiislamu na waislamu wengine kuikosa Tawhidi ya kweli.

Kama Alhadi alidhani waislamu watampa kura mgombea wa CCM kwa kufanya kufuru ya wazi namna hii basi ndiyo kwanza kamharibia!

Nichukue nafasi hii kukushangaa wewe mtoa mada kwa kuchelewa kuifahamu bakwata, alhad na genge lake hawako pale kwaaajili ya ALLAH wanamaslahi yao binafsi
 
pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
5,651
2,000
Hata kusoma tu uislamu unasema
"soma kwa jina la ALLAH mwingi wa rehema mwenye kurehemu;
Sembuse kuomba?
 
pye Chang shen

JF-Expert Member
Jul 11, 2016
5,651
2,000
Tatizo ni elimu. Mtu kaishia madrasa, unatarajia nini.
Sio kweli tatizo kuishia madrasa bali ni udhaifu wa mtu binafsi kushindwa kuwa mwadilifu kwa dini yake
Wako wengi ambao hawakusoma na ni waumini wazuri tu hata huko kwa dini ya wazungu wako pia wasiokwenda shule
Lakini ni watiifu sana kwenye dini
 
ksk

JF-Expert Member
Mar 30, 2016
254
225
Katika kile kinachoonekana ni unafiki wa dhahiri wa BAKWATA, Masheikh wa BAKWATA wameanza kutumia podium mbalimbali za hadhara kumfanyia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Wiki kadhaa zilizopita Sheikh wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam bwana Alhadi, alionekana kung'aka na kumshambulia Muinjilisti Mwingira kwa madai kuwa anafanya kampeni madhabahuni, lakini haikupita hata miezi mitatu Sheikh huyo anasimama kwenye majukwaa ya kisiasa na kutumia jina la dini kumpigia kampeni Mgombea uraisi wa CCM.

Tofauti na Askofu Bagonza na Mwamakula ambao wao huombea mikutano bila ya kuwaambia wananchi wamchague nani, huyu sheikh wa BAKWATA wa Dar es salaam amekwenda mbali na kupiga kampeni kabisa kuuombea kura mgombea huyo wa CCM.

Wakati huohuo, Sheikh huyo wa BAKWATA wa mkoa wa Dar es salaam amewashangaza sana Waislamu kwa kwenda kinyume kabisa na Imani ya dini ya dini hiyo kwa kufanya maombi kwa jina la Yesu kitu ambacho ni marufuku na ni kufuru kubwa sana kwa mujibu wa dini hiyo. Katika dini ya Uislamu inapaswa kuomba kwa Jina la ALLAH(Mwenyezi Mungu muumba mbingu na nchi) peke yake na si kwa jina la Kiumbe yeyote hata awe nabii au hat Malaika. Kwa mujibu wa dini ya Kiisamu Yesu ni nabii na Siyo Mungu.

Kauli hiyo imedhihirisha kuwa Sheikh huyo anaweza kufanya lolote hata kufanya kufuru ya wazi ilimradi awe karibu na watawala.

Kitendo cha Sheikh Alhadi kusema kuwa anaomba kwa jina la Yesu, kisha baadae kutamka Bismillah Rrahmaani rrahiim (yaani kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema) anaimply kuwa Jina la Allah ndiyo Jina la Yesu kitu ambacho ni kufuru kubwa sana kwa muislamu kuifanya.

Matendo haya ya BAKWATA kushindwa kulinda misingi ya dini ya uislamu yanaendelea kujitokeza mara kwa mara na yamekuwa yskiwakera waislamu wengi.

Ni wajibu wa Sheikh Mkuu na waislamu kiujumla kuchukua hatua maana hii tabia ya Masheikh hawa kuvunja misingi ya waziwazi ya dini ya kiislamu kwa sababu ya maslahi machache ya dunia yatapotosha watoto wa kiislamu na waislamu wengine kuikosa Tawhidi ya kweli.

Kama Alhadi alidhani waislamu watampa kura mgombea wa CCM kwa kufanya kufuru ya wazi namna hii basi ndiyo kwanza kamharibia!

Mbona mnashangilia Sheikh Ponda aliposema Waislamu wote wamchague Lissu. Je Ponda siyo kiongozi wa dini? Kumbe mkuki kwa nguruwe.
 
HRT

JF-Expert Member
Jul 31, 2015
438
500
Mbona mnashangilia Sheikh Ponda aliposema Waislamu wote wamchague Lissu. Je Ponda siyo kiongozi wa dini? Kumbe mkuki kwa nguruwe.
Ponda ni kiongozi wa Taasisi gani ya Kiislamu?
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom