Masheikh Na Wanazuoni wa Kiislamu Waunga Mkono Sensa ya Watu na Makazi

Kwa hiyo nchi zingine zinazotoa takwimu za dini hazina umoja wa kitaifa?Sikubaliani na hoja kwa sababu iko too simplistic
"M'Mungu angetaka mngekuwa kundi moja na mchungaji mmoja, lakini hitlafu miongoni mwenu lazima ziwepo!" hiyo ni kauli ya Allah! unaetaka muwe kundi moja wee ni nani?
 
View attachment 57778
sheikh hamis mattaka(kushoto) akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari kwa niaba ya mwenyekiti wa jopo la masheikh wanazuoni wa kiislam tanzania kuhusu mchakato wa kukusanya maoni ya katiba, sensa ya watu na makazi na hali ya zanzbar leo jijini dar es salaam. Kulia ni sheikh iddi simba.



taasisi ya masheikh na wanazuoni wa kiislamu tanzania imeunga mkono kauli iliyotolewa hivi karibuni na sheikh mkuu wa tanzania, mufti issa shaaban simba ya kuwataka waislamu na watanzania kote nchini kushiriki kikamilifu katika sensa ya watu na makazi itakayofanyika agosti 26 mwaka huu.


akizungumza na waandishi wa habari leo jijini dar es salaam kwa niaba ya mwenyekiti wa jopo la masheikh na wanazuoni wa kiislamu tanzania sheikh hamis mattaka amesema hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa baadhi ya makundi yanayowahamasisha waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kutoshirika zoezi la sensa ya watu na makazi.


amesema wao kama jopo la wanazuoni hawaoni tatizo la zoezi hilo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na kuongeza kuwa sensa ya watu na makazi ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na imepitishwa na bunge la jamhuri ya muungano wa tanzania.


jopo hilo limeiomba serikali kuweka sheria itakayozuia utoaji wa takwimu zinazohusu dini za watanzania zinazotolewa na vyanzo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kuwa kipengele hicho si sehemu ya sensa nchini.


“tunajua kuwa serikali ilikua na nia njema kukiondoa kipengele cha dini katika sensa hapana budi nia njema hiyo ya serikali ilindwe kwa kuweka sheria itakayozuia kutoa takwimu zinazohusu dini za watanzania” amesema sheikh mattaka.


amefafanua kuwa sensa ya awali ya mwaka 1957 kipengele cha dini kilihusishwa na baadaye kuondolewa katika sensa zilizofuata kwenye madodoso ya kukusanyia takwimu za kaya.


“sisi kama jopo kila siku tunasema ili twende salama kama wananchi wa nchi hii ni wajibu wetu kuheshimu na kufuata sheria kwa maana ya kutii sheria bila shuruti, kwa hiyo tunasema sensa ya watu na makazi ni jambo la kisheria si jambo la mitaani, hatuwezi kulumbana na kujadili jambo ambalo liko wazi kisheria na limepitishwa na wabunge tuliowachagua sisi wenyewe”


amefafanua kuwa zoezi la sensa ya watu na makazi litaiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa kuwa na takwimu sahihi za watu na makazi, hali ya kipato cha kaya, vizazi na vifo na pia kuiwezesha serikali kwapatia huduma bora wananchi wake.


katika hatua nyingine jopo la masheikh na wanazuoni wa kiislamu tanzania imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya katiba.


aidha jopo hilo limewataka watanzania wote kwa ujumla kuitumia fursa hiyo muhimu kutoa maoni ambayo yataiwezesha nchi kupata katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi.


“ sisi kama jopo la wanazuoni wa kiislamu tunawataka waislamu na watanzania wote kwa ujumla kuitumia fursa hii muhimu kwa kutoa maoni yao ili hatimaye nchi yetu ipate katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi ijayo” amesema sheikh mattaka.

Kiganyi, jf.
mwanzo - wotepamoja.com


wakiristo wanahaha. Mimi navyojua wanaharakati wa kiislam wapo imara. Hao ndio tunawaoasikiliza. Akina sheikh ponda na wengine na sio hawa bakwata
 
masheik wasomi wanaielewa dini vizuri wanatii mamlaka sio kama wale wenye midevu mungu awabariki tunataka amani.

hahah. Wakiristo wanahaha kutaka kuficha ukweli. Ngojeni mtasikia siku ya sensa ikifika. Maandamano hadi kieleweke. Mwiba ulipingilia ndipo utapotoka. Hao wanafata mkumbo tu. Hawana ushawishi wowote katka harakati za waislam.
 
Sensa ina vipengele vingi sana ukiacha hili moja la dini (hii itakuwa ni upungufu katika questionnare yenyewe)

Lakini kukataa whole process kwasababu ya kipengele kimoja SIDHANI KAMA NI BUSARA

Mimi nafikiri watu washiriki lakini waendelea kutoa mapungufu ya sensa, kama ambavyo tunatoa mapungufu ya MoU, kukataa mahakama ya kadhi n.k iko siku wataelewa
 
Sasa sheikh ponda akija mtamtambua labda mmdanganye na wali maharage ndio haesabiwe.
 
wakiristo wanahaha. Mimi navyojua wanaharakati wa kiislam wapo imara. Hao ndio tunawaoasikiliza. Akina sheikh ponda na wengine na sio hawa bakwata

===================

Niliwahi kuandika hapo awali kwamba hizi kelele za BAKWATA na akina Ponda zitamalizika tu wakeshapewa cho chote na serikali. Haya ni matokeo ya maneno yangu. Mliosoma comments zangu mtakumbuka maneno haya " Panya akitaka jina, hujipitisha kwa watu".:flypig: Ila sitashangaa wale ambao gawio hawajapatiwa wakaja na tamko lingine, kwani ufalme wao tayari unahasimiana wao kwa wao. Ukiona haya yanatokea, hasa kwa wanaotegemewa kulinda maadili ktk jamii, basi Mteule uwe macho.
 
ndio raha ya kuwa na wasomi wanaoweza kuona mambo kwa upana wake...tatizo la wale kina yakhe wengine ILIMU ilipofika majumbani kwao ilitumbukia vyooni
 
Waislam hatuitambui taasisi hiyo na hilo sii tamko la waislam!idd simba na kikundi chake ni ma puppets wa ccm mafisadi
 



attachment.php

Nani kampa IDDI SIMBA USHEKHE? washajilambia vimilioni kwa ajili ya kuwagawa waumini. Hatari sana kwa taifa.
 
Malumbano na sideeq mnatokwa mapovu sana, udini wenu mnaweza ata kujilipua, sasa thread hii wakristo wameingiaje mnaanza kuwashutumu? Hao waliosema mshiriki sensa ni viongozi wenu wa bakwata, hamtaki mnaacha kuesabiwa au mwende bakwata mkalaumu huko, siyo kila kitu mnalaumu wakristo, na ubavu wa kuikataa bakwata hamna.
 
Hivi kumbe Idd Simba ni Shehe? Jamani, ni Idd yule yule anayekabiliwa na kesi ya ufisadi UDA na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM au ni Idd mwingine? Ha ha ha ha ha! Kweli kuna watu majasiri.

Sheikh hata madrasa ya wanafunzi kumi hawana
 
ndevu ndio uwanaume hata yesu alikuwa nazo ndevu,kuhusu waislamu wanajua kama ni mtu wa serikali hivyo yupo kwa maslahi yao na hawa mashekhe hawatambuliki wametokea wapi
 
Nimesema leteni evidence iliyoonyesha kuwa Tanzania ikitoa stats za imani ya dini amani itavunjika

na nimeuliza nchi zipi ambazo amani imevuunjika kwa sababu ya sensa iliyoonyesha imani za watu?

Takwimu kuhusu imani za dini hazina tija yo yote kwa serikali kupanga maendeleo ya taifa. Lakini kila kundi la imani lina uhuru wa kuhesabu idadi ya waumini wake. Ninaamini makanisa, misikiti na masnagogi yana takwimu rasmi za waumini wake ambazo wanazihitaji ili kupanga mipango ya kuendeleza imani zao. Kama kundi la imani linalosubiri kufanyiwa kazi hiyo na serikali basi imekula kwenu!!!! Ya Kaizari aachiwe Kaizari!!!!
 
Back
Top Bottom