Masheikh Na Wanazuoni wa Kiislamu Waunga Mkono Sensa ya Watu na Makazi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masheikh Na Wanazuoni wa Kiislamu Waunga Mkono Sensa ya Watu na Makazi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kiganyi, Jun 30, 2012.

 1. Kiganyi

  Kiganyi JF-Expert Member

  #1
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 30, 2012
  Messages: 1,244
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 0
  Picha na 1.jpg
  Sheikh Hamis Mattaka(kushoto) akitoa tamko mbele ya waandishi wa habari kwa niaba ya Mwenyekiti wa jopo la Masheikh wanazuoni wa kiislam Tanzania kuhusu mchakato wa kukusanya maoni ya Katiba, Sensa ya watu na Makazi na Hali ya Zanzbar leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Sheikh Iddi Simba.  Taasisi ya masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imeunga mkono kauli iliyotolewa hivi karibuni na Sheikh mkuu wa Tanzania, Mufti Issa Shaaban Simba ya kuwataka waislamu na watanzania kote nchini kushiriki kikamilifu katika Sensa ya watu na Makazi itakayofanyika Agosti 26 mwaka huu.


  Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam kwa niaba ya mwenyekiti wa jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania Sheikh Hamis Mattaka amesema hatua hiyo inafuatia kuwepo kwa baadhi ya makundi yanayowahamasisha waumini wa dini ya kiislamu na wananchi kutoshirika zoezi la Sensa ya watu na makazi.


  Amesema wao kama jopo la wanazuoni hawaoni tatizo la zoezi hilo kutokana na umuhimu wake kwa taifa na kuongeza kuwa Sensa ya watu na makazi ipo kwa mujibu wa sheria za nchi na imepitishwa na Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


  Jopo hilo limeiomba serikali kuweka sheria itakayozuia utoaji wa takwimu zinazohusu dini za watanzania zinazotolewa na vyanzo mbalimbali ndani na nje ya nchi kwa kuwa kipengele hicho si sehemu ya sensa nchini.


  “Tunajua kuwa serikali ilikua na nia njema kukiondoa kipengele cha dini katika Sensa hapana budi nia njema hiyo ya serikali ilindwe kwa kuweka sheria itakayozuia kutoa takwimu zinazohusu dini za watanzania” amesema Sheikh Mattaka.


  Amefafanua kuwa Sensa ya awali ya mwaka 1957 kipengele cha dini kilihusishwa na baadaye kuondolewa katika Sensa zilizofuata kwenye madodoso ya kukusanyia takwimu za kaya.


  “Sisi kama jopo kila siku tunasema ili twende salama kama wananchi wa nchi hii ni wajibu wetu kuheshimu na kufuata sheria kwa maana ya kutii sheria bila shuruti, kwa hiyo tunasema Sensa ya watu na makazi ni jambo la kisheria si jambo la mitaani, hatuwezi kulumbana na kujadili jambo ambalo liko wazi kisheria na limepitishwa na wabunge tuliowachagua sisi wenyewe”


  Amefafanua kuwa zoezi la Sensa ya watu na makazi litaiwezesha serikali kupanga mipango ya maendeleo kwa kuwa na takwimu sahihi za watu na makazi, hali ya kipato cha kaya, vizazi na vifo na pia kuiwezesha serikali kwapatia huduma bora wananchi wake.


  Katika hatua nyingine jopo la masheikh na wanazuoni wa Kiislamu Tanzania imewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika mchakato wa ukusanyaji wa maoni ya katiba.


  Aidha jopo hilo limewataka watanzania wote kwa ujumla kuitumia fursa hiyo muhimu kutoa maoni ambayo yataiwezesha nchi kupata katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi.


  “ Sisi kama jopo la wanazuoni wa kiislamu tunawataka waislamu na watanzania wote kwa ujumla kuitumia fursa hii muhimu kwa kutoa maoni yao ili hatimaye nchi yetu ipate katiba itakayokidhi matakwa ya wananchi kwa miaka mingi ijayo” amesema Sheikh Mattaka.

  Kiganyi, JF.
  Mwanzo - wotepamoja.com

   
 2. Kiziza

  Kiziza JF-Expert Member

  #2
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 10, 2011
  Messages: 440
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 0
  Afadhali hopefully wale wabishi sasa wataelewa...
   
 3. MwanaFalsafa1

  MwanaFalsafa1 JF-Expert Member

  #3
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 5,566
  Likes Received: 28
  Trophy Points: 135
  Waislamu siku zote huwa wanajitambia kuwa wamoja leo hii nashangaa kila taasisi na kundi ya Kiislamu inakuja na kauli yake yenyewe na kila mmoja inadai kuwakilisha msimamo wa Waislamu wote nchini.
   
 4. norbit

  norbit JF-Expert Member

  #4
  Jun 30, 2012
  Joined: Jul 30, 2007
  Messages: 496
  Likes Received: 212
  Trophy Points: 60
  mashehe ubwabwa utawaona tu
   
 5. Sibonike

  Sibonike JF-Expert Member

  #5
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 23, 2010
  Messages: 10,286
  Likes Received: 4,989
  Trophy Points: 280
  Wasomi ni wasomi tu hata wawe wa dini yoyote na kabila lolote! Sensa ni muhimu jamani
   
 6. RGforever

  RGforever JF-Expert Member

  #6
  Jun 30, 2012
  Joined: Apr 3, 2011
  Messages: 6,186
  Likes Received: 1,905
  Trophy Points: 280
  TV IMAAN NDO WAMETAJWA HAPA
  Kelele Nyingi.... Umoja Sifuri. Ngoja Ponda aibuke na Empted people wake
   
 7. dudus

  dudus JF-Expert Member

  #7
  Jun 30, 2012
  Joined: Feb 28, 2011
  Messages: 7,769
  Likes Received: 6,099
  Trophy Points: 280
  Hivi kumbe Idd Simba ni Shehe? Jamani, ni Idd yule yule anayekabiliwa na kesi ya ufisadi UDA na Mwenyekiti wa Umoja wa Wazee wa CCM au ni Idd mwingine? Ha ha ha ha ha! Kweli kuna watu majasiri.
   
 8. Chilisosi

  Chilisosi JF-Expert Member

  #8
  Jun 30, 2012
  Joined: Oct 19, 2008
  Messages: 3,055
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 135
  Kuna tofauti kubwa sana kwenye appearance KATi ya waliotoa hili tamko na wale hamnazo Wa uamsho au Akina ponda, Hawa jamaa wanazuOni wanaonekana ni wasomi na wanaelewa dini Yao vizuri Kabisa, hivi kwa nini Hawa jamaa wasitwmbelee Kule urojoni Zanzibar kutoa darasa, sababu watu wengine wanaupaka Madoa uisilamu kwa sababu hawana elimu
   
 9. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #9
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Masheikh na wanazuoni wa kiIslam wana hoja ya msingi ukisoma bandiko lao kwa makini tena bila kengeza la udini utagundua jambo moja muhimu nalo ni kuheshimu sheria za nchi.Lingine wamegusia sensa ya mwaka 1957 ambayo ilikuwa na kipengele cha dini baadae ikaondolewa kwa faida ya umoja wa waTanzania.

  Inashangaza kidogo anatokea Sheikh mwenye uraia wa Burundi anapewa covarege kubwa na vyombo vyetu vya habari bila kuhoji nini madhumuni ya hicho kipengele cha dini.
   
 10. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #10
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  The Hypocrites will be in the lowest depths of the Fire: no helper wilt thou find for them;-

  -Sura 4 (An-Nisa), ayah 145, Qur'an[SUP][/SUP]
   
 11. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #11
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Kwa hiyo nchi zingine zinazotoa takwimu za dini hazina umoja wa kitaifa?

  Sikubaliani na hoja kwa sababu iko too simplistic
   
 12. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #12
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  majambo.

  Ikiwa haukubaliani hama Tanganyika nenda katika hizo nchi wanazotoa takwimu za dini mbona rahisi sana.


   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 13. w

  wimbi la mbele JF-Expert Member

  #13
  Jun 30, 2012
  Joined: Jan 4, 2011
  Messages: 647
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  Nimesema leteni evidence iliyoonyesha kuwa Tanzania ikitoa stats za imani ya dini amani itavunjika

  na nimeuliza nchi zipi ambazo amani imevuunjika kwa sababu ya sensa iliyoonyesha imani za watu?
   
 14. Dotworld

  Dotworld JF-Expert Member

  #14
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 3,929
  Likes Received: 143
  Trophy Points: 160
  [​IMG]
   
 15. Ngongo

  Ngongo JF-Expert Member

  #15
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 20, 2008
  Messages: 12,155
  Likes Received: 3,634
  Trophy Points: 280
  Wanazuoni wanaonekana wasomi wa elimu dunia na elmu ahera ingawa Idd Simba akiachiwa nafasi kidogo ankwapua kila kitu ha ha ha ha.


  [​IMG]
   
 16. m

  makwesa Member

  #16
  Jun 30, 2012
  Joined: Jun 17, 2012
  Messages: 49
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Mnajidanganya subirini redio imani na tv imani ndizo zinakubalika na waislamu wengi nchini.
   
 17. s

  sweke34 JF-Expert Member

  #17
  Jun 30, 2012
  Joined: Sep 28, 2010
  Messages: 2,533
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 135
  majambo... hizo ni nchi nyingine na zipo kwenye mazingira mengine na wana malengo yao kuweka kipengele cha dini kwenye sensa. Na sisi Tanzania tuna mipango na malengo yetu tunapofanya sensa. Serikali yetu haiwezi kuweka dini kwenye mipango yake ya maendeleo kwani haina lengo la kuendeleza kundi fulani la dini. Idadi ya watoto, vijana,wazee ,kipato nk ni vitu vinavyowekwa kwenye mipango ya maendeleo kwa sababu vinahusu watanzania wote tofauti na dini inayohusu kikundi fulani tu katika jamii...
   
  Last edited by a moderator: Jan 4, 2016
 18. Kibanga Ampiga Mkoloni

  Kibanga Ampiga Mkoloni JF-Expert Member

  #18
  Jun 30, 2012
  Joined: Aug 9, 2007
  Messages: 14,578
  Likes Received: 1,675
  Trophy Points: 280
  Waislam tuna tatizo kweli, Mungu atuone na atuokoe kwenye haya majanga ya kuto kujitambua!
   
 19. M

  Michael Mwakyusa JF-Expert Member

  #19
  Jun 30, 2012
  Joined: Mar 18, 2012
  Messages: 307
  Likes Received: 11
  Trophy Points: 35
  Masheik wasomi wanaielewa dini vizuri wanatii mamlaka sio kama wale wenye midevu MUNGU awabariki tunataka amani.
   
 20. S

  Sideeq JF-Expert Member

  #20
  Jun 30, 2012
  Joined: Dec 12, 2009
  Messages: 2,417
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 0
  Jamani njaa mbaya! ......ndio maana Umar ibn Khatab alikuwa akisema "Ufukara huongoza kwenye kufuru"
   
Loading...