Masheikh Kizimbani kwa Kuvunja Ofisi!

Buchanan

JF-Expert Member
May 19, 2009
13,199
1,969
Na Said Njuki, Arusha

WAISLAM mkoani hapa, jana walifurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakihaha kuwadhamini viongozi wao waliopo rumande akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, ambaye pia na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa, Sheikh Adam Chorah.

Sheikh Chorah na wenzake, Sheikh wa BAKWATA Mkoa, Suleiman Milanzi, Katibu wa BAKWATA Mkoa, Bw. Hussein Kajabukama na Muumini mmoja, Bw. Ramadhani Kihago wapo rumande katika Gereza Kuu la Arusha wakituhumiwa kuvunja Ofisi
ya BAKWATA ya mkoa huo.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu
Charles Magesa na kusomewa shitaka linalowakabili ambalo hata hivyo walilikana na Hakimu huyo kueleza Mahakama hiyo kuwa dhamana za washitakiwa hao ziko wazi kwa sharti la kudhaminiwa na watumishi wa Serikali.

Pamoja na waumini hao kujiandaa kwa dhamana lakini hakukuwa na hata mmoja ambaye angeweza kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama hivyo walifanikiwa kuwapata wadhamini hao nje ya muda wa mahakama.

Kutokana na hali hiyo walilazimika kuandika hati ya kuletwa kwa washitakiwa hao mahakamani kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana lakini hata ombi hilo liligonga mwamba baada ya Hakimu kutoa amri kuwa watabaki rumande hadi Februari 10, Mwaka huu.

SOURCE: Majira.

Wana mambo makubwa hapo wengine ni waganga wanakosoa wenzao kwani wao
kupiga ramli mungu karuhusu?
 
Inasikitisha sana viongozi watamaa kiasi hicho mpaka mnakua dini huwezi kuwa na kama vibaka kisa hakieleweki wanawakosoa wenzao :::mbona wao ni waganga tena wapiga ramli???????
 
naona hapa mfano wa habari isiyo habari; maana kwa nini analeta taarifa isiyo kamili??
 
Yes, it is incomplete story. Wamevunja ofisi kwa sababu ya kuiba au walikuwa na ugomvi mwingine? ungetueleza then tujue walikuwa na haki au ni wahuni tu
 
naona hapa mfano wa habari isiyo habari; maana kwa nini analeta taarifa isiyo kamili??

As long as wamefunguliwa mashtaka mahakamani kuna uwezekano (a prima facie case) kwamba walichokifanya ni kiovu!
 
Na Said Njuki, Arusha

WAISLAM mkoani hapa, jana walifurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakihaha kuwadhamini viongozi wao waliopo rumande akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, ambaye pia na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa, Sheikh Adam Chorah.

Sheikh Chorah na wenzake, Sheikh wa BAKWATA Mkoa, Suleiman Milanzi, Katibu wa BAKWATA Mkoa, Bw. Hussein Kajabukama na Muumini mmoja, Bw. Ramadhani Kihago wapo rumande katika Gereza Kuu la Arusha wakituhumiwa kuvunja Ofisi
ya BAKWATA ya mkoa huo.

Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu
Charles Magesa na kusomewa shitaka linalowakabili ambalo hata hivyo walilikana na Hakimu huyo kueleza Mahakama hiyo kuwa dhamana za washitakiwa hao ziko wazi kwa sharti la kudhaminiwa na watumishi wa Serikali.

Pamoja na waumini hao kujiandaa kwa dhamana lakini hakukuwa na hata mmoja ambaye angeweza kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama hivyo walifanikiwa kuwapata wadhamini hao nje ya muda wa mahakama.

Kutokana na hali hiyo walilazimika kuandika hati ya kuletwa kwa washitakiwa hao mahakamani kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana lakini hata ombi hilo liligonga mwamba baada ya Hakimu kutoa amri kuwa watabaki rumande hadi Februari 10, Mwaka huu.

SOURCE: Majira.

Hii habari haiko sawa au?
Hawa ni viongozi na makatibu wa Bakwata wamevunja office za Bakwata! sasa, wameshtakiwa kwa kuvunja office usiku au funguo za office zilipote ikawalazimu wavunje ilwaingie ndani na kuendelea na kazi za Bakwata? Habari haijawa wazi.
 
Back
Top Bottom