Buchanan
JF-Expert Member
- May 19, 2009
- 13,199
- 1,969
Na Said Njuki, Arusha
WAISLAM mkoani hapa, jana walifurika katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Arusha wakihaha kuwadhamini viongozi wao waliopo rumande akiwemo Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa, ambaye pia na Mwenyekiti wa Halmashauri Kuu ya Baraza Kuu la Waislamu (BAKWATA) Mkoa, Sheikh Adam Chorah.
Sheikh Chorah na wenzake, Sheikh wa BAKWATA Mkoa, Suleiman Milanzi, Katibu wa BAKWATA Mkoa, Bw. Hussein Kajabukama na Muumini mmoja, Bw. Ramadhani Kihago wapo rumande katika Gereza Kuu la Arusha wakituhumiwa kuvunja Ofisi
ya BAKWATA ya mkoa huo.
Watuhumiwa hao walipandishwa kizimbani mbele ya Hakimu
Charles Magesa na kusomewa shitaka linalowakabili ambalo hata hivyo walilikana na Hakimu huyo kueleza Mahakama hiyo kuwa dhamana za washitakiwa hao ziko wazi kwa sharti la kudhaminiwa na watumishi wa Serikali.
Pamoja na waumini hao kujiandaa kwa dhamana lakini hakukuwa na hata mmoja ambaye angeweza kutimiza masharti yaliyowekwa na mahakama hivyo walifanikiwa kuwapata wadhamini hao nje ya muda wa mahakama.
Kutokana na hali hiyo walilazimika kuandika hati ya kuletwa kwa washitakiwa hao mahakamani kwa ajili ya kutimiza masharti ya dhamana lakini hata ombi hilo liligonga mwamba baada ya Hakimu kutoa amri kuwa watabaki rumande hadi Februari 10, Mwaka huu.
SOURCE: Majira.