Masheikh D’Salaam kutoa tamko mgogoro Arusha leo | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masheikh D’Salaam kutoa tamko mgogoro Arusha leo

Discussion in 'Habari na Hoja mchanganyiko' started by kilimasera, Jan 15, 2011.

 1. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #1
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  IDADI ya taasisi zinazojiingiza kwenye mgogoro wa CCM na Chadema, uliosababisha polisi kuua watu watatu na kuujeruhi 29 mkoani Arusha inazidi kuongezeka, baada ya Baraza Kuu la Jumuiya na Taasisi za Kiislaam (T), kuandaa mkutano utakaoshirikisha jumuiya na taasisi mbalimabili kutoa tamko.

  Tayari, hadi sasa taasisi mbalimbali za dini, jamii, uchumi, siasa na viongozi wa vyama na serikali, wamejitokeza na kutoa misimamo yao kuhusu mgogoro huo, huku mitazamo ikikinzana.
  Katika matamko hayo wapo waliolaumu polisi kwa kusababisha mauaji hayo, wengine wakilaumu wanasiasa kwa kukiuka amri ya vyombo vya ulinzi na usalama.

  Katibu wa baraza hilo, Sheikh Ponda Issa Ponda, alisema mkutano huo utafanyika ukumbi wa Diamond Jublee jijini Dar es Salaam kuanzia saa 2:00 asubuhi hadi saa 6:00 mchana.

  "Lengo la mkutano huu ni kuweza kujadili kwa kina mgogoro wa Arusha na kuweza kutoka na msimamo wetu kupitia tamko la pamoja ambalo litasomwa kwa niaba mbele ya waandishi wa habari na washiriki wote," alisema Sheikh Ponda.

  Sheikh Ponda, ambaye pia ni Katibu wa Kutetea Haki za Waislaam Tanzania, alisema tayari zaidi ya jumuiya na tasisi 10 za Kiislaam zimethibitisha ushiriki wao.

  "Mkutano utazishirikisha taasisi zaidi ya 10 na tayari zimethibitisha ushiriki wao, wadau na washiriki wa mkutano huu watapata fursa ya kuchambua chanzo, mwenendo na athari za mgogoro wa Arusha kwa wenyeji wake na Watanzania kwa upana," alisema.

  Alisema suala la Arusha halipaswi kunyamaziwa na kwamba, lazima kwa upande wao watoe tamko ili kuonya na kukemea au kutahadharisha mambo mbalimbali kwa usalama wa taifa.
   
 2. PakaJimmy

  PakaJimmy JF-Expert Member

  #2
  Jan 15, 2011
  Joined: Apr 29, 2009
  Messages: 16,236
  Likes Received: 308
  Trophy Points: 180
  Tunasubiri hilo tamko!
   
 3. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #3
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  Hivi kwa mfano wakisema kwamba CHADEMA walifanya makosa kitatokea nini??maana maaskofu waliishaipinga serikali na kulaani mauaji na nazungumza hivyo kwasababu baadhi ya mashekhe wameshaanza kuiunga mkono polisi na wengine wakisema misikiti ilipigwa mawe!
   
 4. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #4
  Jan 15, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,762
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  hapo ndo pagUmu na mafisadi wanajua hapo ndo pakucheza napo tuu!
   
 5. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #5
  Jan 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Hakuna kitakachotokea kwa sababu haikuwa lazima Masheikh kuwa support Maaskofu. Wako huru na ni ruksa kuonyesha msimamo wowote ule.

  Kuunga au kutounga mkono mapolisi kunategemea tu na kiwango cha utashi na uchambuzi wa mambo. Mimi ninachojua tamko lolote watakalotoa litawahusu wao na siyo maaskofu
   
 6. Gerad2008

  Gerad2008 JF-Expert Member

  #6
  Jan 15, 2011
  Joined: Jun 9, 2009
  Messages: 489
  Likes Received: 89
  Trophy Points: 45
  Dawa ya mtu mbishi ni kumpuuza wala usimjadili na akiona hamna anaye draw attention kwake ataendelea na shughuli zake
   
 7. kilimasera

  kilimasera JF-Expert Member

  #7
  Jan 15, 2011
  Joined: Dec 2, 2009
  Messages: 3,073
  Likes Received: 17
  Trophy Points: 135
  any way mimi kabla ya hilo tamko natabiri mashekhe watasema CHADEMA ilifanya makosa yaani dalili zote naziona unajua kikubwa kwamba ni mtazamo wangu tu lakini kwamba kutokana na uchaguzi uliopita kuathiriwa na udini watu wengi wamekua wakihusisha CHADEMA na ukristu CUF na uislamu na CCM Pia na uislamu nasema CCM na uislamu kwa kuwa mwenyekiti na katibu wake ni waislamu mbaya zaidi katibu anakua anachafua hali ya hewa mara kwa mara kwa kuhongea pointless nje ya chama!na kunukkuu mistari ya bible kitu ambacho maaskofu wamemkosoa na kumpinga kabisa kwamba haijui bible na asiongee kwa kuquote mistari ya bible!Hivyo mashekhe sababu wanajua mwenyekiti na katibu wa chama ni dini yao lazima ili kuepusha wasiingie aibu watatetea upande wao!
   
 8. Lokissa

  Lokissa JF-Expert Member

  #8
  Jan 15, 2011
  Joined: Nov 20, 2010
  Messages: 7,079
  Likes Received: 154
  Trophy Points: 160
  mhhhh siddhani kama watalaani watakubali polisi walikuwa sahihi kuuwa kama alivosema Imam wa Msikiti Mkuu wa Ijumaa jijini Arusha, Shehe Mohamed Hambal, aliyekuwa akihutubia msikitini hapo katika swala ya Ijumaa jana.

  Alisema hivyo wakati akitoa msimamo wa Waislamu wa Arusha juu ya tukio hilo lililosababisha vifo vya watu watatu, Watanzania wawili na raia mmoja wa Kenya.

  Shehe alisema katika mkutano wa hadhara wa Chadema ulioongozwa na Katibu Mkuu, Dk. Willibrod Slaa na Mbunge wa Moshi Mjini, Philemon Ndesamburo, kwa nyakati tofauti walitoa kauli za uchochezi kwa wafuasi wao zilizoashiria uvunjifu wa amani
  .

  tunaenda wapi Tanzania ya Leo kama kiongozi wa dini anabariki mauaji??????????
   
 9. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #9
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Nadhani uko sahihi maana nia yao siyo kusema kutoa kauli juu ya kilichotokea bali ku'react' dhidi ya kauli ya/za maaskofu. Kama nia ni kulaani wasingesubiri ipite wiki ndiyo waone kuna ubaya ulitokea. Kwa kawaida ubaya wowote ukitokea mtu ana'react' muda huo huo au muda mfupi baadaye atakapopata habari. Na mara nyingi masheikh hawako concerned na welfare ya Watanzania bali maslahi yao kama Waislamu na ndiyo maana mara nyingi wanawashangaa maaskofu wanapokemea kitu maana the latter wanahusika kuchangia katika welfare ya wananchi na chochote kinachotokea dhidi ya wananchi kinawagusa. Waislamu wanaguswa tu pale mhusika mmojawapo anapokuwa Mwislamu mwenzao au ku'react' dhidi ya maaksofu as if wao ndio wanaowafundisha maaskofu kitu gani waseme na kitu gani wasiseme!
   
 10. M

  Magobe T JF-Expert Member

  #10
  Jan 15, 2011
  Joined: Mar 19, 2008
  Messages: 2,945
  Likes Received: 356
  Trophy Points: 180
  Serikali/CCM watakuwa wamepata support nzuri na hivyo kuendeleza ubabe kwa vile wanajua wanafanya kinachoonekana ni cha haki kwa mtazamo wa dini fulani. Na kwa vile Waislamu wameahidiwa na serikali mchakato wa kuanzisha Mahakama ya Kadhi na kujiunga na OIC, hawawezi kusema lolote dhidi ya serikali kama maaskofu watakuwa wameshatoa kauli kuikosowa serikali. Hali hii itaendelea hadi hapo watakapoona kuwa wameingizwa mkenge ndipo wanapoweza kuipinga serikali tena. Lakini as long as serikali inazidi kuwapa matumaini hawawezi kuipinga ng'o!
   
 11. M

  MCHARA Senior Member

  #11
  Jan 15, 2011
  Joined: Jan 15, 2011
  Messages: 111
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 35
  Wakiunga mkono polisi wakati ukweli wa Mungu polis ndo wana makosa ndo utakuwa mwanzo wa udini kwani wakristo watadhan waislam wanamuunga mkono rais kwa kuwa ni mwislam jambo ambalo tunaomba mungu apishe mbali.
   
Loading...