MaxShimba
JF-Expert Member
- Apr 11, 2008
- 35,772
- 4,054
VIONGOZI wa kiislamu nchini, wamebaini mwelekeo mbaya wa ustawi wa Watanzania kisiasa na kijamii na hivyo kuwataka kuwa makini katika kuchanganya siasa na dini.
Wamesema kama hilo halitazingatiwa kuna hatari ya nchi kuingia katika machafuko na kuharibu jina zuri la Tanzania, ambalo kwa kipindi kirefu limekuwa likiendana na amani na utulivu.
Hadhari hiyo ilitolewa Dar es Salaam jana na Taasisi na Jumuiya za Kiislamu nchini zilizokutana katika ukumbi wa Diamond Jubilee, kutoa tamko la Waislamu juu ya matukio yanayoendelea kuliandama Taifa.
Akisoma tamko hilo kwa niaba ya Waislamu, Shehe wa Msikiti wa Idrisa, Ally Said Bassaleh, alisema wakati Tanzania ilifanya uchaguzi mkuu Oktoba 31 na kumchagua Rais, wabunge na madiwani na CCM kutoa Rais, wabunge na madiwani wengi, yamejitokeza matukio ya uvunjifu wa amani.
Hata hivyo, walisema mazingira hayo yamesababisha viongozi wa dini kuingilia kati na kutoa matamko kana kwamba Serikali imeshindwa kufanya hivyo.
Shehe Bassaleh alisema kutokana na matukio hayo hivi sasa nchi ipo katika hatari ya kuingia kwenye machafuko na aliitaka Serikali kudhibiti viongozi wa dini wanaotoa kauli zisizozingatia sheria na zinazopingana na Katiba ya nchi.
Alisema baadhi ya viongozi hao wamekuwa wakiingilia masuala ya kisiasa na kutoa maelekezo ya nini kifanyike, kinyume na taratibu, huku vyombo vya Dola vikisita kuwachukulia hatua, suala ambalo ni hatari kwa mustakabali wa Taifa kama litaachwa liendelee.
Alisema mfano mzuri ni tukio la hivi karibuni la mauaji ya Arusha, ambapo maaskofu walijitokeza na kutoa tamko la kulaani mauaji hayo, wakati yapo mauaji ambayo yamekuwa yakifanywa na polisi na wao kukaa kimya.
Hivi sasa hatulali kutokana na mauaji ya Arusha lakini wapo watu waliuawa Micheweni, Pemba mwaka 2001, lakini hakuna aliyelaani mauaji hayo.
Polisi walifanya mauaji mengine Msikiti wa Mwembechai, lakini hilo nalo lilifumbiwa macho leo ni kipi cha ajabu kilichotokea Arusha hadi iwe hatulali? alihoji.
Alisema viongozi wa dini pia wamekuwa wakiingilia masuala ya dini nyingine kama vile kupinga suala la Tanzania kujiunga na Jumuiya ya Kiislamu ya Kimataifa (OIC) na kufunguliwa kwa Mahakama ya Kadhi bila sababu za msingi.
Waislamu wameiomba Serikali kujiunga na OIC kama njia mojawapo itakayowezesha nchi kupata misaada itakayotumika kuinua hali zao katika elimu na uchumi.
Makanisa yamepinga kwa nguvu zao zote pendekezo hili.
Serikali ilipofanya utafiti wa kina ilijiridhisha kuwa kujiunga na OIC kuna manufaa na hakuna madhara yoyote na Bernard Membe (Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa), alitamka hilo bungeni lakini Serikali ilibadili msimamo wake, alisema Shehe Bassaleh.
Januari 5, wafuasi wa Chadema walifanya maandamano yaliyokatazwa na Jeshi la Polisi na kukabiliana na polisi hata kusababisha watu watatu kupoteza maisha na wengine kadhaa kujeruhiwa.
Kutokana na tukio hilo, maaskofu wa Arusha walitoa tamko la kulaani Jeshi la Polisi, ambalo lililazimika kutumia silaha za moto baada ya kubaini kuwa walikuwa hatarini pamoja na kituo chao, chenye ghala la silaha ndogo na kubwa.
Uamuzi huo wa maaskofu ulikemewa na CCM Mkoa wa Arusha, ambayo iliwaasa viongozi hao wa dini kuacha kuingilia masuala ya siasa, vinginevyo wavue majoho na kupanda majukwaa ya kisiasa.
Source: Habarileo