Mashehe waonywa wasigeuze misikiti pango la mafisadi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashehe waonywa wasigeuze misikiti pango la mafisadi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by MziziMkavu, Feb 19, 2012.

 1. MziziMkavu

  MziziMkavu JF-Expert Member

  #1
  Feb 19, 2012
  Joined: Feb 3, 2009
  Messages: 39,620
  Likes Received: 4,613
  Trophy Points: 280
  Masheikh na viongozi wa kiislamu wametahadharishwa kuepuka wasitumiwe na wanasiasa hasa wenye tuhuma za ufisadi, ili kutimiza azma yao ya kutaka kuingia madarakani.
  Badala yake wameshauriwa kutumia misikiti kwa ajili ya kuwaelimisha waumini wao kujiepusha na hatari ya kuiingiza nchi mikononi mwa mafisadi ambao hivi sasa wanatumia nyumba za ibada kugawa fedha.

  Alisema misaada inayoonekana kutolewa kwa kasi na wanasiasa kwa madhehebu ya dini, ina dalili za kuwa sehemu ya kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015.

  Tahadhari hiyo ilitolewa jana jijini Dar es Salaam wakati wa semina ya siku mbili, iliyohusisha viongozi wa kiislamu mkoani Dar es Salaam.

  Miongoni mwa mada zilizotolewa kwenye semina hiyo ni majukumu na wajibu wa viongozi kwa Kurani Takatifu na wajibu wa viongozi dini katika jamii.

  Mwenyekiti wa Taasisi ya Imamu Bukhar Islamic, Sheikh Khalifa Khamis katika mada yake iliyozungumzia majukumu na wajibu wa viongozi, alisema kuwa njia ya kumtambua mtu asiyefaa katika uongozi ni kubaini jinsi anavyoshiriki kununua madaraka kwa njia mbalimbali.

  Alisema baada ya kutambua hali hiyo, wameamua kama viongozi wa dini kutoa tahadhari kwa waumini wao kwa sababu mafisadi ni watu wa hatari kwa taifa.

  "Viongozi wa dini tumieni nafasi zetu kuwaelimisha waumini wasiingie mikononi mwa mafisadi kwani hatua iliyopo hapa nchini hivi sasa ni watu hao wanapita nchi nzima kwenye nyumba za ibada wakigawa fedha na anasa nyingine kama sehemu ya kampeni," alisema na kuongeza:

  "Watu hawa wanafanya hivyo kwa nia ya kujiandaa kuchukua madaraka mwaka 2015, ni hatari mno ikiwa nchi itaingia mikononi mwa mafisadi ambao wamekuwa wakijijali kwa kuhodhi rasilimali za nchi ambazo ni mali ya Watanzania wote," alisema.

  Alisema watu hao wanataka kutumia nafasi za uongozi ili kujinufaisha wenyewe. Alibainisha kuwa, wakati huu ambao nchi imeshafanya uchaguzi mambo yanayopaswa kufanyika ni kuliendeleza taifa kimaendeleo si kufanya kampeni za uchaguzi ujao.

  Pia Sheikh Khamis aliwataka waislamu wajiandae kushiriki kikamilifu katika mchakato wa Katiba na kuwaeleza kuwa hiyo ndio sheria mama na mkataba baina ya mtawala na mtawaliwa.

  Alilitaka kila kundi katika jamii kuwajibika ipasavyo katika kutoa maoni ambayo mwisho wa siku yatalinda maslahi yao.
  Alisema kuwa, wale watakaolala usingizi katika hiyo wasifikiri baada ya kupitishwa haki zao watazipata.

  Naye Sheikh Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Alhad Mussa Salum, aliwataka waumini wa kiislam kuwapuuzia baadhi ya watu ambao wanataka dhehebu la kiislamu lisishiriki katika mchakato wa Katiba kwa maelezo kuwa ni kafiri.
  Alhaj Salum alisema kuwa, waislamu ni sehemu ya Watanzania na kwamba ushiriki wao ni muhimu ili yale yanayowahusu yaweze kuwepo kwenye Katiba.

  "Tunapingana na fikra hizi kuwa Katiba hii ni kafiri, hakuna Katiba ya kikafiri bali ni ya kijamii, sisi ni Watanzania tunaishi ndani ya nchi moja isiyoongozwa kidini, kwa hiyo kila muumini wa kiislamu anatakiwa kuchangia mawazo yake," alisema.
  Alisema kuwa wataendelea kuzungumza na kujadili ili yale yanayowahusu yaweze kuwepo na kuheshimika ndani ya Katiba.

  Naibu Mufti Mkuu wa Tanzania, Sheikh Ali Mkoyogore katika mada yake iliyokuwa ikizungumzia wajibu wa viongozi wa dini katika jamii, alibainisha baadhi ya wajibu wa kiongozi huyo na kusema kuwa ni lazima awe mcha Mungu, tabia nzuri, lugha nzuri, mwadilifu, awe na subira, huruma, mshauri na misimamo.

  Kwa upande wake mgeni rasmi wa semina hiyo kuwa, Katibu Mkuu wa Baraza Kuu la Waislamu wa Tanzania (Bakwata), Sheikh Suleiman Lolila, alisema kuwa viongozi wa dini wanapaswa kuijua Katiba ili iwe rahisi kwao kuwasaidia waumini wao.  CHANZO: NIPASHE JUMAPILI

   
Loading...