Mashehe wa Uamsho, nani alaumiwe kati ya Serikali ya Rais Kikwete, Magufuli na Samia?

G4rpolitics

JF-Expert Member
Jul 29, 2015
4,334
5,183
Kama ilivyo hapo juu, wale Mashehe wa Uamsho walikamatwa Enzi za Rais Kikwete, lawama zikaja kwenye Serikali ya Mwendazake, saa hizi zimeelekezwa kwa Mama wakati mhusika mkuu yupo.

Sijawahi kusikia akiulizwa ni kwa nini hao watu waliwakamatwa kipindi cha uongozi wake, walikuwa wana makosa yapi?

Saa hizi amekuwa akipambwa kuwa alikuwa Kiongozi mzuri, lawama za hao Mashehe inabidi ipewe serikali ya awamu ipi?
 
Tangu tusikie kelele kuhusu hilo kundi, mpaka leo hakuna jipya. Binafsi naona hawaonewi, ila ni utaratibu mbovu wa uendeshaji mashtaka uliopo Tz hufanya hukumu kuchelewa.
 
Inawezekana ikawa sawa, lakini si muwafunge basi!!miaka tisa sasa bado kesi, haijakamilika?waafrika tuna tabu sana!ndio maana watu wengi wanahisi kuwa labda ni uonevu tu!!
Kukaa miaka yote hiyo ni kufungo tosha. Kama binadamu Inasikitisha mno.
 
Kama ilivyo hapo juu, wale Mashehe wa Uamsho walikamatwa Enzi za Rais Kikwete, lawama zikaja kwenye serikali ya Mwendazake, saa hizi zimeelekezwa Kwa Mama wakati mhusika mkuu yupo, sijawahi kusikia akiulizwa ni kwa nini hao watu waliwakamatwa kipindi cha uongozi wake, walikuwa wana makosa yapi? Saa hizi amekuwa akipambwa kuwa alikuwa Kiongozi mzuri, lawama za hao Mashehe inabidi ipewe serikali ya awamu ipi?
Watanzania wamejaa unafiki kuna watanzania wangapi wapo magerezani kwa kuonewa tu hatusikii chochote!
 
Hao siyo mashehe wa uamsho bali ni watuhumiwa wa ugaidi. Hawakukamatwa kwa kuwa ni mashehe bali walikamatwa wakiwa na tuhuma za ugaidi. Ungeuliza hivi: Wale watuhumiwa wa ugaidi waliokamatwa huko zanzibar wakati wa serikali ya awamu ya nne alaumiwe nani? Angalizo: Hawakumatwa na Kikwete bali walikamatwa na vyombo vya ulinzi na usalama. Tusitake kuchochea hisia bila sababu! Huwezi kujua kama ukifanikiwa kuzichochea athari itakuwaje? Tanzania tumekuwa na amani sana mpaka wengine wanataka kulewa na amani hiyo! Nawasilisha!
 
Walaumiwe hao Mashekhe Magaidi, wanataka Tanzania yetu ipoteze Amani tuliyonayo kama wenzao walivyopoteza amani ya Msumbiji, Kenya, Somalia n.k

Wana record ya Ugaidi wa wazi kabisa kwa kuuwa Watalii watatu Mombasa, kwa kummwagia Padri pamoja na Watalii tindikali Zanzibar

Wanataka kuanzisha dola ya kipumbavu na kuanzisha mahakama ya kadhi

Wanalazimisha utawala usiofaa na wanataka kila mtu afuate mwongozo wao

Kuwaachia huru hawa ni kuhatarisha Amani ya Nchi.


Wabillah Tawfiq,
 
Halafu mleta mada anaeleza kabisa kuwa walikamatwa ktk awamu ya nne. Sasa awamu ya sita inahusikaje hapo? Fanya kitu kinaitwa solve problem by Gaus elimination method!

1. Mama Samia mtoe kabisaaa, hausiki hata chembe.

2. Awamu ya 5 weka pembeni, suala kalikuta mahakamani kaliacha mahakani. Hakuwa na mamlaka ya kusamehe mahabusu.

3). Awamu ya nne toa kabisa, watuhumiwa walihamishwa tu kutoka nchi nyingine yenye Rais, bendera na wimbo wa taifa. Huyu wa awamu ya nne kasaidia tu kuwahifadhi kwa chakula, malazi na matibabu!

4). Awamu ya tatu usiitaje kabisa haikuwagusa hata kidogo maana walikuwa bado ni raia wema!

Hapa tatizo ni ugaidi tu. Hata Osama Kama si ugaidi angekuwepo bado!
 
Kama ilivyo hapo juu, wale Mashehe wa Uamsho walikamatwa Enzi za Rais Kikwete, lawama zikaja kwenye serikali ya Mwendazake, saa hizi zimeelekezwa Kwa Mama wakati mhusika mkuu yupo, sijawahi kusikia akiulizwa ni kwa nini hao watu waliwakamatwa kipindi cha uongozi wake, walikuwa wana makosa yapi? Saa hizi amekuwa akipambwa kuwa alikuwa Kiongozi mzuri, lawama za hao Mashehe inabidi ipewe serikali ya awamu ipi?
Tatizo sio nani apewe lawama, tatizo ni je, walikamatwa wakiwa hawana makosa!?

Watanzania hasa wanaharakati na wanasiasa ni watu wa ajabu sana

Tangu wakamatwe hakuna makanisa yanachomwa Moto wala mapadri kumwagiwa tindikali, watu hawalioni hili!?
 
Kweli kabisa waache kumlaumu JK kama yeye binafsi. Uraisi ni taasisi. Vyombo vya Dola , ulinzi na usalama vina wajibu wake pia.

Tuitunze amani ya Taifa letu.
 
Back
Top Bottom