Mashehe wa Bara Ongozeni harakati za kuupinga Muungano; Tanganyika isiidhulumu Zanzibar

Status
Not open for further replies.
Pasco,

Kwani humfahamu Mwanakijiji ni mdini? Mbona hajasema Maaskofu wasaidieni masheikh wa zanzibar (tena ni baadhi na sio wengi) kudai na kupata wanachokitaka. Kwanini imekuwa of interest zanzibar mbona hazisemei fujo zilizotokea Mwanza mpaka misahafu ikachomwa moto na msikiti au kule waathirika ni waislamu? Huu ni uchochezi na fitina na hapo hampati zama za propaganda na ujinga zilishapita zamani siku hizi kila mtu mjanja na muelewe na nini unachotaka kukifanya.

Na watu wanaoendekeza udini kama hawa watalaaniwa
 
Huu ni uhaini!.
Nimemkumbuka Nyerere, angekuwepo, tusingefika hapa!. Tukiwaambia JK is a weak president, watu hawataki kukubali!.
Hao masheikh wa kukundi cha Uamsho, wanakuwa tolerated under pretex ya religious tolerance hivyo kutenda vitendo vya jinai ya uhaini kwa muda mrefu na kuachwa hivi hivi wakiangaluwa!. Lakini wafuasi wao walipofanya jinai ya violence, ndipo wakakamatwa!. Kwa huu udhaifu wa JK, sasa sio tena CCM itamfia mikononi nwake, bali sasa muungano unataka kumpasukia!.

Mzee Mwanakijiji please stop this reciplicles za kihaini, japo muungano wenyewe sio halali, lakini "the end justifies the meas"!.

Hata kama muungano una matatizo, matatizo ya kuvunjika yatakua makubwa mno. Ungevunjika miaka ya sitin kusingekuana madhara lakin kwa sasa hivi ni hatari sana kuvunja muungano. Hata hawa wanaosema wanadhulumiwa nashindwa kulewa wanadhulumiwa wapi.
 
Duh! kumbe ni AJIRA,
From facebook MM anasema

"La kwanza: Viongozi wote wa Zanzibar wanaofanya kazi kwenye ofisi za Muungano si itabidi waachie nafasi zao zote kupisha Watanganyika kushika nafasi hizo na kama wapo Watanganyika wanaoshika nafasi kwenye serikali ya Zanzibar nao itawapasa waziachilie mara moja. SIKU MOJA BAADA YA MUUNGANO? "

Duuuuuuh..wawinda ajira ingieni barabarani.
 
Nawasihi mashehe wa bara wafuate mfano wa wale wa Zanzibar; watuongoze kupinga Muungano ili Zanzibar iwe huru. Haiwezekani watu wa Tanganyika (wakiwemo mamilioni ya Waislamu) wawe wanawadhulumu Waislamu wa Zanzibar kwa kuendeleza Muungano. Tafadhalini mashehe kwa hili hata miye nitawaunga mkono!! Muungano umalizwe kusiwepo na dhulma, ukandamizaji na uonevu unaofanywa na Watanganyika (Waislamu kwa Wakristu) dhidi ya Wazanzibari!

Kabla hamjanirukia... there is a point am making...

Kwa nini usianze na kuambia Maaskofu na Mapadre, Wachungaji, waongoze hizo harakati unazotaka wewe sababu ni dini moja mnajua mnachokifanya.

Wewe unakuwa na sura mbili moja unataka kuonekana mtu makini katika jamii ya Watanzania na ingine unaonesha dhamira yako halisi ya udini na chuki dhidi ya Uislam.

Nimesoma makala yako kwenye Tanzania Daima kuhusu muungano nimeunganisha na hii thread yako ndio nimejua sura zako mbili.

Kwenye maandishi yako kuwa makini usitake kuwagawa Watanzania kama wale waandishi wa Kenya na Rwanda walivyowagawa wananchi wao leo wana kesi za kujibu kwenye mahakama za kimataifa.
 
Last edited by a moderator:
Duh! kumbe ni AJIRA,
From facebook MM anasema

"La kwanza: Viongozi wote wa Zanzibar wanaofanya kazi kwenye ofisi za Muungano si itabidi waachie nafasi zao zote kupisha Watanganyika kushika nafasi hizo na kama wapo Watanganyika wanaoshika nafasi kwenye serikali ya Zanzibar nao itawapasa waziachilie mara moja. SIKU MOJA BAADA YA MUUNGANO? "

Duuuuuuh..wawinda ajira ingieni barabarani mpaka kieleweke.
 
Hata kama muungano una matatizo, matatizo ya kuvunjika yatakua makubwa mno. Ungevunjika miaka ya sitin kusingekuana madhara lakin kwa sasa hivi ni hatari sana kuvunja muungano. Hata hawa wanaosema wanadhulumiwa nashindwa kulewa wanadhulumiwa wapi.

Tunaposema Muungano kuvunjika haina maana unavunjika tu kama kipande cha mti uliokauka. Kuvunjika kwa Muungano kunaendana na mazungumzo ya kuvunja Muungano na makubaliano hadi na tarehe ya kuachana. So usiwe na wasiwasi, matatizo hayo unayoyafikiria yatashughulikiwa katika mazungumzo ya utengano.
 
Kwa nini usianze na kuambia Maaskofu na Mapadre, Wachungaji, waongoze hizo harakati unazotaka wewe sababu ni dini moja mnajua mnachokifanya.

Wewe unakuwa na sura mbili moja unataka kuonekana mtu makini katika jamii ya Watanzania na ingine unaonesha dhamira yako halisi ya udini na chuki dhidi ya Uislam.

Nimesoma makala yako kwenye Tanzania Daima kuhusu muungano nimeunganisha na hii thread yako ndio nimejua sura zako mbili.

Kwenye maandishi yako kuwa makini usitake kuwagawa Watanzania kama wale waandishi wa Kenya na Rwanda walivyowagawa wananchi wao leo wana kesi za kujibu kwenye mahakama za kimataifa.

Duh; wewe ukitaka kuwashauri mapadre na wachungaji unaweza kufanya hivyo sivyo? au hadi Mwanakijiji aseme ndio unalipa uzito?
 
Kwa anayetaka kumuelewa MM. Aaangalie hiyo Video Clip.

Ukichangia bila kuitizama hiyo Video Clip utakua unatoka Nje ya mada.

Naionea huruma Zanzibar.

Sababu anazotoa huyu Bwana kutetea kuukata muungano Hazina mshiko jamani.
 
MM,

Masheikh wa Tanganyika wapambane na mfumo kristo unaongozwa na kanisa katoliki kuendelea kuwakandamiza waislamu na fitna zinazozunguka. Masheikh za zanzibar wanatosha kuwatoa jasho nyie wafuasi wa kanisa katika suala la muungano hawahitaji masheikh wa kutoka Bara.

mh! hapo sasa pabaya,
 
Huu ni uhaini!.
Nimemkumbuka Nyerere, angekuwepo, tusingefika hapa!. Tukiwaambia JK is a weak president, watu hawataki kukubali!.
Hao masheikh wa kukundi cha Uamsho, wanakuwa tolerated under pretex ya religious tolerance hivyo kutenda vitendo vya jinai ya uhaini kwa muda mrefu na kuachwa hivi hivi wakiangaluwa!. Lakini wafuasi wao walipofanya jinai ya violence, ndipo wakakamatwa!. Kwa huu udhaifu wa JK, sasa sio tena CCM itamfia mikononi nwake, bali sasa muungano unataka kumpasukia!.

Mzee Mwanakijiji please stop this reciplicles za kihaini, japo muungano wenyewe sio halali, lakini "the end justifies the meas"!.

Pasco, Wazanzibar (Waislam?) wa Zanzibar wanaandamana kudai kura ya maoni kuhusu Muungano wetu ikiwa ni haki yao ya kikatiba achilia mbali waliofanya jinai ya kuchoma moto makanisa, Ni vipi leo Watanzania (Waislam) wa bara wakiandamana kwa malengo yale yale iwe uhaini? Mbona unakuwa na double standard kwa kitu kile kile?

Bado naamini kuwa kwa watu waliostaarabika ni wajibu wao kuhoji jambo lolote toka kwa watawala pale wanapoona mambo hayaendi kama inavyotakiwa, kumbuka wanainchi ndio nguzo ya watawala na wanapaswa kusikilizwa, Hebu fikiria mziki uliopo Syria sasa hivi umesababishwa na nini?

I plead guilty! kama maneno yangu haya madogo yanalingana na uhaini na wanaofanya hivyo Zanzibar wanaambiwa ni haki yao basi neno haki limepoteza maana. Uhaini siyo hawa viongozi waliotengeneza mazingira ya kuvunja Muungano? Wameshindwa kuuokoa miye nawaambia kile kilicho obvious - tena kutoka kwa mtu ambaye ameutetea muungano sana na a pan-africanist to the core - it is about time to say 'let Zanzibar go'! Tuanze tu mahusiano ya nchi mbili kama tunavyohusiana na Malawi, Iran, Kenya na Uingereza na nchi nyingine duniani. Kwanini uwe ni uhaini to state the obvious?

Halafu unajipinga mwenyewe; kama unaamini Muungano siyo "halali" uhaini unakuwepo vipi? Kama ndoa haipo mtu akisema muachane utadai vipi talaka?

in the name of almight allah...tuwape wazanzibar wanachokitaka....kuwabembeleza ktk muungano kunawafanya waamini kuna kikubwa tunachokipata toka kwao....
 
kwani miye ni msemaji wa kila mtu na wa kila kitu? wengine nao si wanaweza kusema na wanayo haki ya kusema? Au mpaka niseme mimi ndio kipate umuhimu? Ukitaka maaskofu waunge mkono mashehe Zanzibar sema tu; miye nitakuunga mkono.

Hivi kwa akili yako Masheikh wanaweza kufuata ushauri wako dhaifu kama huu.
 
MMJ hata wewe unachochea makanisa ya Bara (Tanganyika) yaanze kuchomwa? ulijifanya kumpinda Dogo Janja kua kauli yake ya Uchochezi, Je hii yako?
 
Kumbe Muungano ni 'dubwana'!? Ndio maana CCM hawataki ujadiliwe kwenye uandikaji/urekebishaji wa katiba!
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom