Mashehe kuongea kiswahili kama kiarabu..!

majebsmafuru

JF-Expert Member
May 1, 2017
452
624
Hili swala la mashehe kuongea kiswahili kama vile hawakijuwi vizuri na chenye lafudhi ya kiarabu ni manjonjo au ndio ukweli mashehe wetu kiarabu kinapanda sana mpaka yawa taabu na shidaaa kuongea kiswahili kama sisi cha kibantu hasa hasa?! Twauliza tu..Itabidi na maaskofu nao wawe basi na lafudhi ya kiingereza wanapohubiri makanisani! Waende sambamba na mashehe!:);)
 
Hoja ni kwamba kuna uhisiano gani wa kiingereza na ukristo?
 
Kwa asilimia kubwa kiswahili kinatoka na kiarabu na hata ukiangalia baadhi ya maneno yanatumika kama yalivyo kwa lugha zote mbili.
Neno kama 'shukrani...sabaa, sita, kabur... hayo ni baadhi ya maneno (kwa uchache) ambayo yanatumika na lugha zote kama yalivyo...
Kiswahili kilianzia pwani, sehemu kama zanzibar, dar es salaam n.k, na tunajua kuwa sehemu hizi ndizo zilikaliwa na waarabu so kuongea kiswahili katika lafudh ya kiarabu ni kama kukirudisha kwenye asili yake.
 
Yani mmefundishwa Kiswahili kutoka huko kwenu bara, tayari mnajiona wajuvi!!!
Wajuvi wa kiswahili TZ ni wachache sana, ila swala analouliza huyu bwana ni lafudhi, wewe wasikilize mashehe au wale manguli wa kusoma Koran! Ila nami ntafuatilia kiswahili cha mapadri, je kina lafudhi ya kiingereza, kilatino au kirumi?!
Hahahaha ila kuna kaukweli hapo...waTZ kwa swaga na umaskini wetu acha kabisa..:);)
 
Hili swala la mashehe kuongea kiswahili kama vile hawakijuwi vizuri na chenye lafudhi ya kiarabu ni manjonjo au ndio ukweli mashehe wetu kiarabu kinapanda sana mpaka yawa taabu na shidaaa kuongea kiswahili kama sisi cha kibantu hasa hasa?! Twauliza tu..Itabidi na maaskofu nao wawe basi na lafudhi ya kiingereza wanapohubiri makanisani! Waende sambamba na mashehe!:);)
Ni aina ya ujinga ulijengwa na waarabu walipoleta dini.nikimsikia mtu anaongea hivyo napata hasira,kuna mapadrii pia hutumia lafudhi ya kiebrania japo wao ni wakati ule tu wa kuongoza ibada ila kwa hawa wa kuigiza lafudhi ya kiaarabu wenyewe mpaka mtaani unawasikia eti wanalaza kiswahili utadhani wametokea Oman,kumbe ni wa Ikungi Singida
 
Ni aina ya ujinga ulijengwa na waarabu walupoleta dini.nikimsikia mtu anaongea hivyo hasira,kuna mapadrii pia hutumia lafudhi ya kiebrania japo wao ni wakati ule tu wa kuongoza ibada ila kwa hawa wa kuigiza lafudhi ya kiaarabu wenyewe mpaka mtaani unawasikia eti wanalaza kiswahili utadhani wametokea Oman,kumbe ni wa Ikungi Singida
Hahahahaha sina mbavu kabisa...:):):)
 
Hili swala la mashehe kuongea kiswahili kama vile hawakijuwi vizuri na chenye lafudhi ya kiarabu ni manjonjo au ndio ukweli mashehe wetu kiarabu kinapanda sana mpaka yawa taabu na shidaaa kuongea kiswahili kama sisi cha kibantu hasa hasa?! Twauliza tu..Itabidi na maaskofu nao wawe basi na lafudhi ya kiingereza wanapohubiri makanisani! Waende sambamba na mashehe!:);)
Wew itakuwa ni wale wa
Radha
Shure
Mzuli
Reo
Balafu
 
Ni utumwa na dini uchwara hizi za kigeni.
Pumbafusana.

Achana nao wote na wapuuze waone Kama wapuuzi wengine tu.

Niliwahi kukutana na mmoja anaomba michango ya kuandaa chakula cha watoto yatima yaani anavyoongea ikabidi kwanza nicheke.

Kisha nikamuuliza, unajua kuongea Kiswahili Kama Mimi niongeavyo !?

Akajibu, ndiyo .

Nikamuuliza tena, Mbona sasa unaongea hivyo Kwa kuiga vitu visivyo na maana!?

Nikamwambia ongea Kiswahili sanifu upate hela za futali ya watoto. Ukiendelea hivi utashindwa kupata hela.
Basi, akaongea Kiswahili sanifu nikampatia michango maisha yakaendelea.

Kwa hiyo, ni ujinga tu na utumwa (brainwashing waliofanyiwa na warabu pori).

Hata dini zingine nazo wanabadilisha sauti na lafudhi za Kiswahili nawaangalia nabakia kucheka tu maana utumwa umewajaa hadi kwenye visigino.
 
Hiyo ni colonial legacy na ipo kwenye dini zote

1.Muislamu hupenda kumuiga muarabu aliyemletea dini kuanzia mavazi, chakula tabia hata matamshi ambayo mara kwa mara wanashindwa kutamka vyema lahaja za kiswahililakini mbongo anaanza kumuiga tena huyo anayekosea ili afanane naye

2.Mkristo naye hupenda kumuiga mzungu aliyemletea dini kuanzia mavazi, tabia, lugha na matamshi. Sana sana walokole ndio wamekubuhu kwenye hili, unakuta mzungu anashindwa kutamka lahaja za kiswahili kama jioni yeye ataita CHIONI sasa unakuta mbongo nabii wa magumashi naye anaiga vile vile makosa ya mzungu.......CHIONI YA LEO BWAANA ATAKUCHA KUONGEA MAHALI HAPA""
 
Back
Top Bottom