Mashati ya dukani

jashmoe32

JF-Expert Member
Dec 4, 2012
1,087
423
Samahanini wajumbe ila ni sehem gani hapa Dar naweza pata mashati ya kiume kwa bei nzuri na yawe ya dukani,naomba msaada mana kuna sehem nimeenda na wamesema ni 30 kwenda juu mpaka nkakata tamaa mana nna Interview jumapili
 
Una intervie JUMAPILI?! Dah, sasa mkuu kama umekimbia shati za elf30 unasema bei ghali mbona balaa hilo sasa, maana hata shati la maana la mtumba ni 30 mpaka 40!! Anyway naona ungeandika NAHITAJI MASHATI YA BEI RAHISI, wenyewe wanaita RONYA!...nenda congo utayakimbia mwenyewe mkuu, hata elf5 unapata shati.
 
Hahahaha pole mkuu mimi nipo mwanza ila umenichekesha sana kwa jinsi unavyotafuta mashat Original..tafuta mtumba kaka nenda pale karume utapata shat la mtumba zuri kupita hilo Original unalotaka...
 
Unataka kitu kizuri kwa gharama nafuu...!!!

Bei ya shati dukani huanzia 25k na kuendelea, yale ya mtumba yanayotoka Nairobi huanzia 15k na kuendelea.

Pita Makumbusho, Mwenge, Kino kwa Ustaadh, Posta kwa Lameck ununue shati zuri la mtumba kwa 20k tu..

Kama huna hiyo pesa nenda Ilala Boma, Karume, Tandika sokoni, K'koo mtaa wa Kongo kajipatie mashati yale ya mpira kwa raha zako...
 
jitahidi uwe simple ili mwajili wako akuone si mpenda makuu kwa sababu ukishanunua shati jipya litakunyima kujiamini kwa sababu utakuwa kila wakati unajiangalia angalia mbwembwe za hapa napale
Na ole wako mwajili wako akagundua hilo utakuwa umeshajipotezea maksi za kuajiliwa hapo.Nakushauri angalia nguo zako ambazo huwa zinakufanya upendeze na piga pasi vizuri then tinga hizohizo

Ni ushauri tu waweza kuuchukua au ukaacha
 
Thanks alot kwa ushaur mkubwa and al put that in consideration
 
kaka nenda kariakoo mtaa wa aggrey upande wa kushoto kama umetokea kwenye keep left kuelekea ACB kuna maduka ya suti suti hivi..either ni mbele au nyuma wanauza mashati elf 17000
 
Kaka kwani yaliyoko ndani hali zake ni tete sana? Unaweza ukaibua moja toka sandukuni bado ukaonekana smart tu. Hofu yangu ni kama kila interview uinunulie shati si itakula kwako?
 
kaka nenda kariakoo mtaa wa aggrey upande wa kushoto kama umetokea kwenye keep left kuelekea ACB kuna maduka ya suti suti hivi..either ni mbele au nyuma wanauza mashati elf 17000

Basi sichangii tena. Huu ndio ushauri madhubuti.
 
Back
Top Bottom