Masharti ya kuangalia TV nyumbani miaka ya 90

Mshua baada ya kugundua akiungurumisha pikipiki lake anapoingia mnasambaratika kama panya wezi akawa anakuja na gia nyutro hata hivyo tulikuwa tunanusa na kusikia sauti ya mnyororo anapokaribia ...maana bro alikuwa anajua kuwasha kideo sasa kuna siku alitufuma tulikula njuluti za kutosha kila mmoja wetu kwa mgawanyo wa kumtosha 5 of us nakumbuka bro alikula kona alikuwa form one lutengano ilikuwa Disemba kama hii 1993 !
Washua wa enzi za Nyerere hao, ukisikia gari liko getini mshua anakuja lazima sakafu yote iwe safi.

Kukiwa na karatasi moja tu sakafuni una kesi kubwa sana ya kujibu.
 
Hahahaha haya mambo yasikie tu, niliumia mguuni na bati kisa kuchungulia dirishani kuangalia TV kwa jirani, wazazi wa zamani walivyokua wagumu sikupelekwa hospitali wala nini nikajiuguza mwenyewe mpk nikapona na kuniachia bonge la kovu
Shangazi yangu alinunua TV Kwa hasira anadai watoto wake misuli ya mikono imewatoka utafikiri wanyanyua vitu vizito Kisa kuning'ia kwenye madirisha ya watu kuangalia TV
 
Washua wa enzi za Nyerere hao, ukisikia gari liko getini mshua anakuja lazima sakafu yote iwe safi.

Kukiwa na karatasi moja tu sakafuni una kesi kubwa sana ya kujibu.
Wazee zamani walikuwa si mchz

Ova
 
Watoto ilikuwa hamkai kwenye viti ni chini. Hapo wote ni kimyaa.
Tv inawashwa kuangalia taarifa ya habari tu TVT au movie kama ya hard target, derta force, Commando etc. Ila ndio nilimjuliaga yvonne chakachaka na Aurus mabele.
Wazee walikuwa wakoloni sana, linapokuja swala la TV. Yaani masharti kibao😀😀

Mitv yenyewe michogo dude lina kilo 30+😂
Zilivuma sana kati ya 1988 -1999
1. Double impact- Vandamme
2. Police assassin- Michele Yeoh
3. Rambo- Slyvester Stalone
4. Bloodsport- Vandame na Bolo Yeung
6. Delta force- Chuck Norris
7. Predator- Arnold Schwarzenegger
8. War bus
9. Blood first- Don the "dragon" Wilson
10. Except for no mercy- Jalal Merhi na Billy blanks
11. Enter the dragon- Bruce lee
12. The big boss- Bruce lee
13. Game of Death- Bruce lee
14. The kickboxer- Vandame na Tong Po.
15. Cobra- Slyvester Stalone
16. Mayhem - Brent-Huff
17. Strike commando -Reb Brown
18. Luck seven
19. Missing in action -Chuck Norris
20. Mafia Vs Ninja = Alexander Luo
21. America ninjas = Michael Dudikoff, David Bradley
22. Shaolin Vs Lama
23. Nam Angels- Brad Johson
24. Police story- Jack Chan
25. Black belt- Don the "dragon" Wilson
26. No retreat no surrender
27. The king of the kickboxer- Loren Avedon na Billy Blanks
28. Cyborg
29. China O'Brien- Cynthia Rothrock
30. The best of the best- Philip Rhee na Erick Robert
 
Zilivuma sana kati ya 1988 -1999
1. Double impact- Vandamme
2. Police assassin- Michele Yeoh
3. Rambo- Slyvester Stalone
4. Bloodsport- Vandame na Bolo Yeung
6. Delta force- Chuck Norris
7. Predator- Arnold Schwarzenegger
8. War bus
9. Blood first- Don the "dragon" Wilson
10. Except for no mercy- Jalal Merhi na Billy blanks
11. Enter the dragon- Bruce lee
12. The big boss- Bruce lee
13. Game of Death- Bruce lee
14. The kickboxer- Vandame na Tong Po.
15. Cobra- Slyvester Stalone
16. Mayhem - Brent-Huff
17. Strike commando -Reb Brown
18. Luck seven
19. Missing in action -Chuck Norris
20. Mafia Vs Ninja = Alexander Luo
21. America ninjas = Michael Dudikoff, David Bradley
22. Shaolin Vs Lama
23. Nam Angels- Brad Johson
24. Police story- Jack Chan
25. Black belt- Don the "dragon" Wilson
26. No retreat no surrender
27. The king of the kickboxer- Loren Avedon na Billy Blanks
28. Cyborg
29. China O'Brien- Cynthia Rothrock
30. The best of the best- Philip Rhee na Erick Robert
🤝Zote hizi nimeziona miaka hiyo ya 90 hadi 2000😀 tunatoka mbali aisee.

Ila wenzetu kiteknolojia walikuwa mbali yaani hizo dunia ya leo unazipata kwa 720p na baadhi kwenye 1080p ambazo ukiziangalia kwenye hizi flat zinaonyesha clear kabisa utadhani movie ya mwaka jana.

Mfano niliikumbuka ile American ninja ya kwanza kuishusha aisee inaonyesha saafi kabisa.720p
 
Wale wa Cartoon Network tangu enzi za 1990s mpoo?
Dah....kitambo sana
Image_1575817336.jpeg
 
Hahahaha haya mambo yasikie tu, niliumia mguuni na bati kisa kuchungulia dirishani kuangalia TV kwa jirani, wazazi wa zamani walivyokua wagumu sikupelekwa hospitali wala nini nikajiuguza mwenyewe mpk nikapona na kuniachia bonge la kovu
Pole Sana mkuu
 
Ndo muwaheshimu wanasayansisasa mtambue wanafanya kazi kubwa kurahisisha maisha.
 
Hakuna kuumia mkuu maana wakati ulikuwa bado sana, wakati mwanao ana switch on TV hadi sasa hivi kuna ambao hawana access na kitu kinacho itwa TV....

Techn na utandawazi vunakuwa haraka siku hadi Siku..
Sure
 
Hahahha.... kuangalia tv kwa jirani shuruti ukaoge kwanza ..... hauruhusiwi kukaa juu,ya,kochi

Wenye Tv kufunga milango ilikuwa ni kawaida.....basi tuna jazana dirishani kuchungulia Tv...dahh maisha hayana
Dunia inakwenda kasi mno
Tulishawahi kumwagiwa maji dirishani tena ya sabuni.
Tulikimbia kama vipofu full kugongana na kujibamiza kwenye miti sabuni inauma machoni balaa.
Nafikiri iliandaliwa mahususi kwa ajili yetu.
Lkn mkemia wa siku hiyo alikuwa na roho mbaya sana maana hakufuata viwango vya tbs.
Na ndio ulikuwa mwisho wetu wa kupiga chabo.
 
Back
Top Bottom