Mashamba yote kupimwa viwanja Kinondoni

Egnecious

JF-Expert Member
Jul 8, 2015
875
960
MASHAMBA YOTE KUPIMWA VIWANJA KINONDONI.

NI MKAKATI WA KUMALIZA MIGOGORO YA ARDHI, UVAMIZI

Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Mh Ally Hapi ameeeleza kuwa Manispaa ya Kinondoni imeandaa mpango mkakati wa kupima ardhi na mashamba yote yanayomilikiwa na umma na wananchi binafsi ili kuwezesha ardhi yote kuwa na hati na kuweka mpango bora wa matumizi unaozingatia uwepo wa huduma za jamii.

Akieleza uamuzi huo DC Hapi amebainisha kuwa mkakati huo unalenga kumaliza kabisa migogoro ya ardhi wilayani humo na kwamba wamiliki wa mashamba wasioweza kumudu gharama za upimaji watalazimika kuingia makubaliano maalum na manispaa hiyo ili kulipia gharama hizo kwa mtindo wa kugawana idadi ya viwanja baada ya upimaji. Viwanja vitakavyogawiwa kwa manispaa vitauzwa kwa wananchi wengine ili kulipia gharama za upimaji wa ardhi.

Aidha amewataka wavamizi wote wa maeneo ya wazi kuacha mara moja kufanya uhalifu huo kwani ni kinyume cha sheria na hatua kali zitachukuliwa dhidi yao.

Ametoa kauli hizo leo alipokuwa akizungumza na watendaji na viongozi wa kata ya Wazo katika ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo pamoja na utekelezaji wa shughuli za maendeleo katika wilaya ya Kinondoni.

Amesema migogoro mingi ya Ardhi husababishwa na ardhi kutopimwa na hivyo kuchochea uvamizi na ujenzi holela usiozingatia sheria.
Maeneo yanayoongoza kwa uvamizi ni kata za Mabwepande, Bunju na Wazo ambako baadhi ya wananchi wanamiliki mashamba makubwa ambayo hayajaendelezwa.

Katika hatua nyingine Mh. Hapi amekagua ujenzi wa Shule mpya ya sekondari eneo la Salasala ambayo inajengwa kwa fedha zitokanazo na sakata la kampuni ya Zantel ambalo DC Hapi aliliibua mwishoni mwa mwaka jana ambapo kampuni hiyo ya simu ilikua imekwepa kulipa zaidi ya shilingi milioni 600 kwa manispaa ya Kinondoni kwa miaka kadhaa.

Hii ni Kata ya Tano kati ya Kata kumi za awamu ya pili ya Ziara yake katika Manispaa ya Kinondoni.
1488052486022.jpg
 
Back
Top Bottom