Plot4Sale Mashamba yanauzwa, kukodishwa na kukopeshwa kwa bei nafuu

VKP Investment for youth ni taasisi inayojishughulisha na miradi mbalimbali ya ARDHI ikiwemo mashamba na viwanja vilivyo sehemu mbali mbali Tanzania, ikilenga kumilikisha watanzania Ardhi kupitia miradi yake na taratibu zihusuzo Ardhi Tanzania.

1. Kwa sasa wanauza 700,000 per acre kwa mashamba yalioko Bagamoyo na 400,000 per acre kwa mashamba yalioko Bungu – Rufiji.

2. Wanakopesha bila riba (lipa 30% ya bei ya shamba/kiwanja na kamilisha ndani ya miezi 7 kiasi kilichobaki.)

3. Wanakodisha mashamba kwa bei nafuu. 50,000(elfu hamsini) per acre kwa msimu, ambapo msimu ni miezi 8.

Ofisi zetu zipo Mbezi tankibovu, jengo la The Future Resort.

Facebook: vkp investment

Simu: 0785700540
Safi sana. Tutakucheki.
1. Bagamoyo sehemu gani Mkuu, kwa sababu bagmaoyo ni Pana.
2. tangaza jina lako, hapo kwenye avatar ondoa hiyo ya Munchie weka vkp investment. tumia Fulsa
 
1. Yapo Bagamoyo Fukayosi kama unaelekea Msata.

2. Asante, nitafanya hivyo.
 
Bei zako ni kubwa sana ndugu sipo hapa kukuharibia Bali kupeana elimu,Fukayosi hadi kiwangwa mashamba mengi hayazidi laki 3 na nusu kwa eka na kwa upande wa bungu ekari moja ni Tsh elfu 30 tu.
 
mkuu, tuwekee registration / LEGAL details zako hapa tujue tuna deal na mtu official..
 
Hivi ardhi ya kwetu eti mtukodishie hivi sikuhizi huwa wananchi wageni mpaka muwakodishie mashamba??? Huwezi kulima pisha wanaoweza kulima..
 
Bei zako ni kubwa sana ndugu sipo hapa kukuharibia Bali kupeana elimu,Fukayosi hadi kiwangwa mashamba mengi hayazidi laki 3 na nusu kwa eka na kwa upande wa bungu ekari moja ni Tsh elfu 30 tu.
fukayosi ni kabla ya kiwangwa au ni baada
 
Bei zako ni kubwa sana ndugu sipo hapa kukuharibia Bali kupeana elimu,Fukayosi hadi kiwangwa mashamba mengi hayazidi laki 3 na nusu kwa eka na kwa upande wa bungu ekari moja ni Tsh elfu 30 tu.

Kama unayo pesa tasilimu nenda kanunue hayo ya bei nafuu. Lakini kama pesa ya kuungaunga hapa ndipo.
 
Bei kama kubwa si ukatafute wenyewe hauni jamaa ni kama agent unadhani aliamka tuu akakuta hizo details katumia gharama na kumbuka analipia na ofisi na wafanyakazi ww kama hauwezi usimwaribie mwezio ridhiki yake ,sio lazima unachokuta jf unachangia kama halikuhusu sepa
 
Hatuwezi kulea matapeli bei zingekuwa reasonable sawa Ila sio hizi alizoweka,bei za kitapeli......Kote nazunguka kutafuta mashamba bungu jaribu kisele kiwangwa bei nazijua vizuri,from elfu 30 hadi laki 4???
 
Asante kiongozi umesomeka. Kwa waliokusoma watachangamkia haraka.
 
Kwa huko kiwangwa na fukayozi kuna umbali gani kutoka bagamoyo mjini hadi huko? Jee nauli ni shillingi ngapi? Na jee usafili upo unapatikana kirahisi? Na jee kwa heka moja ya kununuwa wanauza shillingi ngapi?

Cc Savimbi jr,Munchie
 
Bungu nina eneo kubwa sana nimenunua haha ila sio kwa hiyo bei...siaribu biashara ila bungu maeneo hayafiki laki 4...ni bei nzuri sana
 
Nahotaji kununua shamba ila bei ya ekari lisizidi laki 4 location ningependa zaid iwe maeneo ya pwan ya rufiji......kwa atakaejua anaeuza shamba atanishtua
 
bungu iiko wapi kwa hapa dar nami nahitaji shamba uko

Bungu mbele ya mkuranga kutoka mkuranga kama vijiji 3 au 2 kama sikosei....kama upo serious kweli unaweza kupata maeneo kule na ukafurahia mwenyewe....
 
Similar Discussions

Back
Top Bottom