Mashamba ya Balali yavamiwa na wanakijiji wenye Hasira

MC

JF-Expert Member
Joined
Oct 5, 2007
Messages
762
Points
225

MC

JF-Expert Member
Joined Oct 5, 2007
762 225
Source ITV News,


Wananchi waishio eneo la Mbweni wamevamia mashamba ya Dr.Balali na kuanza kugawana kwa madai kuwa yanatokana na pesa za ufisadi pesa ambazo wameziita kuwa ni mali yao 'Wananchi' zoezi lilisitishwa baada ya mlizi wa mashamba hayo kuripoti polisi kitendo ambacho kilisababisha wananchi hao kutawanyika baada ya askari kuwasiri.


Kimsingi mimi binafsi jambo hilo limenifurahisha kwa kuwa naona kabisa watanzania hawataki tena mambo ya danganyatoto, wananchi wamechoka na jinsi mafisadi wanavyobebwa na jinsi sheria zinavyopindishwa. Japo si vizuri kuchukua sheria mkononi lakini kama wanaotakiwa kuchukua sheria hawawajibiki ni bora uamuzi huo wa wananchi.


Mafisadi wengine mjiandae tutaanza kuzichukua mali zenu (ambazo kimsingi ni za watanzania wote)kwa nguvu kama serikali itaendelea kuwakumbatia.
 

Forum statistics

Threads 1,389,308
Members 527,903
Posts 34,022,687
Top