Mashamba morogoro | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashamba morogoro

Discussion in 'Matangazo madogo' started by The hammer, May 26, 2012.

 1. The hammer

  The hammer JF-Expert Member

  #1
  May 26, 2012
  Joined: May 17, 2011
  Messages: 2,280
  Likes Received: 1,236
  Trophy Points: 280
  Wadau nauliza kwa yeyote ambaye ana taarifa za uhakika kuwa kuna mashamba yanauzwa kwa bei rahisi sana huko Moro kuwa hizo habari ni za kweli na hekari ni sh.ngapi na ni maeneo gani hasa mashamba hayo yapo sokoni...
   
 2. M

  Mrdash1 JF-Expert Member

  #2
  May 26, 2012
  Joined: Sep 21, 2010
  Messages: 1,379
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 0
  Mkuu ukitaka mashamba au shamba huko morogoro au sehemu ingine yoyote ya JMT isipokuwa unguja na pemba inakubidi kwanza ubainishe eneo unalolitaka mfano kama ni morogoro je ni kilosa? kilombero? ulanga? na baada ya hapo linalofuata ni wewe kufunga safari hadi kwenye hilo eneo ulilolipenda, tatu unaenda kwa ofisi za ardhi za wilaya, wao watakuambia sehemu yalipo hayo mashamba/shamba, hatua ya nne ni kukutana na viongozi wa serkali za kata na vijiji za maeneo hayo sasa serkali za vijiji wakikubaliana na wewe wanahitisha mikutano mkuu na wanavijiji wanatoa mawazo na maoni yao, wakikubalia basi umepata mashamba/shamba, lakini kwa ukweli siyo mashamba wala shamba bali ni mapori ambayo mengine hayajawahi kukanywagwa na mwanadamu tangu uumbaji, hivyo mwisho kabisa ni kazi kwako kubadili pori kuwa shamba.

  Gharama zitatofautiana kutoka eneo hadi eneo lakini kwa wastani ukijumlisha huduma zote kuanzia usafiri, chakula, malazi, kulipia vikao (sitting allowance) za serkali za kata/vijiji, kumtoa bwana ardhi ofisini, gharama ya kununua ardhi (pori) na kulisafisha ili liwe shamba ni 50,000.00 hadi 100,000.00 kwa hekari.
   
 3. N

  Nancy M Member

  #3
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 17, 2012
  Messages: 43
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 13
  Unahitaji ekari ngapi?
   
 4. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #4
  Sep 10, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  20 zatosha!!
   
 5. Shine

  Shine JF-Expert Member

  #5
  Sep 10, 2012
  Joined: Feb 5, 2011
  Messages: 11,514
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 0
  Pia na mashamba ya kukodi kwaajili ya kulima mpunga inakuwa je kwa kukodi yaani garama na procedure zake zikoje kwa anaejua anijuze
   
 6. bibliography

  bibliography JF-Expert Member

  #6
  Sep 10, 2012
  Joined: May 20, 2011
  Messages: 607
  Likes Received: 130
  Trophy Points: 60
  kuna mashamba yanauzwa sehemu moja inaitwa mafuru ni part ya wilaya ya mvomero nyuma ya chuo cha sua ni karibu sana about 10 km kutoka sua ekari ni sh elf 60 kupima + hela ya kikao cha serikali ya kijiji
   
 7. M

  Mboganyiru Member

  #7
  Sep 10, 2012
  Joined: Mar 22, 2012
  Messages: 33
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 15
  Asante kwataarifa kamanda. Mazao gani labda naweza lima eneo hilo? Hali ya maji ikoje huko? ubarikiwe.
   
 8. Shark

  Shark JF-Expert Member

  #8
  Sep 11, 2012
  Joined: Jan 25, 2010
  Messages: 20,140
  Likes Received: 7,391
  Trophy Points: 280
  contacts basi kaka!!
   
 9. m

  miettu Member

  #9
  Jul 30, 2013
  Joined: Sep 12, 2012
  Messages: 25
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  hayo mashamba bado yapo?
   
 10. sudy mlela

  sudy mlela Member

  #10
  Jul 30, 2013
  Joined: Jul 15, 2013
  Messages: 35
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Kuna ekari 4 zipo kibaha kwa mathias na zipo barabarani..
   
Loading...