Mashamba maeneo ya Bagamoyo

bwegebwege

JF-Expert Member
Jul 30, 2010
1,068
183
Wana JF!

Kunu ndugu yangu amenihabarisha kuwa kuna mashamba maeneo ya Bagamoyo (maeneo mbalimbali) na ni bei poa (hakunitajia bei)!

Binafsi nina nia ya kununua eneo kwa ajili ya kilimo kule; ingawa sijafika nimehakikishiwa kuwa ni maeneo mazuri sana kwa ufugaji na kilimo cha korosho, maembe na minazi!

Swali langu ningependa wana JF kama kuna yeyote mwenye taarifa inayohusiana na mipango ya baadaye ya serikali kwa maeneo ya Bagamoyo...naogopa kuchukua eneo leo (say ekari 50) halafu unaambiwa eneo hilo limetengwa kwa ajili ya kujenga kitu fulani...hasa ukizingatia kuwa serikali hii inaendesha mambo yake kisanii....

Kama kuna mtu anafahamu maeneo (say majina ya vijiji) ambavyo vipo katika mipango ya serikali kwa ajili ya ujenzi wa kitu fulani etc ninaomba sana anijulishe!! Ukinitajia maeneo unayojua kwamba ni ya "moto" basi ninapoenda huko nakuwa na tahadhari...au nakwepa mapema!!

Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo!

Nawasilisha
 
Wana JF!

Kunu ndugu yangu amenihabarisha kuwa kuna mashamba maeneo ya Bagamoyo (maeneo mbalimbali) na ni bei poa (hakunitajia bei)!

Binafsi nina nia ya kununua eneo kwa ajili ya kilimo kule; ingawa sijafika nimehakikishiwa kuwa ni maeneo mazuri sana kwa ufugaji na kilimo cha korosho, maembe na minazi!

Swali langu ningependa wana JF kama kuna yeyote mwenye taarifa inayohusiana na mipango ya baadaye ya serikali kwa maeneo ya Bagamoyo...naogopa kuchukua eneo leo (say ekari 50) halafu unaambiwa eneo hilo limetengwa kwa ajili ya kujenga kitu fulani...hasa ukizingatia kuwa serikali hii inaendesha mambo yake kisanii....

Kama kuna mtu anafahamu maeneo (say majina ya vijiji) ambavyo vipo katika mipango ya serikali kwa ajili ya ujenzi wa kitu fulani etc ninaomba sana anijulishe (KWA PM)!! Ukinitajia maeneo unayojua kwamba ni ya "moto" basi ninapoenda huko nakuwa na tahadhari...au nakwepa mapema!!

Nitashukuru sana kwa msaada wenu wa mawazo!

Nawasilisha
 
Duuh aisee, nafikiri kati ya sehemu yenye mashamba ya bei ghali ni bagamoyo, usitumie habari ya kuambiwa wee nenda mwenyewe utajionea. KUna kundi la watu wameamka na kwenda kuvamia maeneo huko bagamoyo, nakumbia kwa sasa mashamba ni ghali mno mno mno...! Heka moja sio chini ya 5-6 Milion kwa maeneo mazuri karibu na barabara. Kama unataka maeneo ya vijijini saaana hapo utapata kwa laki 3-5 kwa heka...! Nenda mwenyewe ukajionee usisubiri kupewa tarifa...!

Usisahau kuna ada ya cha juu kwa wale maafisa ardhi wa wilaya ili wakusaidie kukamilisha taratibu za ununuzi...!
 
Bwegebwege,kuwa makini sana na mashamba ya bagamoyo before hujanunua. Mume wangu alinunua shamba pale miaka mingi sana nyuma toka kwa wanakijiji. Amekuwa nalo bila shida yoyote. Na alikuwa ana pepaz zote kihalali toka wilayani. Miezi miwili iliyopita akaliuza maana alisema. Wakapeana documents zote na kukabidhiana kisheria.
After one week aliyenunua akampigia cm kuwa eti lile eneo ni la jeshi. Kumbe lilichukuliwa kinyemela na pepaz hazikupelekwa wilayani. Ikabidi arudishe pesa za watu.

Sasa kuwa makini sana maana kuna dhulma sana inayofanywa na watendaji wabovu wa serikali ambayo huwezi jua kirahisi.
 
Maeneo mengi ya pwani usanii mwingi... nenda idara ya Ardhi Bagamoyo wakuoneshe Masterplan/land use map ya wilaya...itakupa mwanga wa kuanzia..!!
 
Bwegebwege,kuwa makini sana na mashamba ya bagamoyo before hujanunua. Mume wangu alinunua shamba pale miaka mingi sana nyuma toka kwa wanakijiji. Amekuwa nalo bila shida yoyote. Na alikuwa ana pepaz zote kihalali toka wilayani. Miezi miwili iliyopita akaliuza maana alisema. Wakapeana documents zote na kukabidhiana kisheria.
After one week aliyenunua akampigia cm kuwa eti lile eneo ni la jeshi. Kumbe lilichukuliwa kinyemela na pepaz hazikupelekwa wilayani. Ikabidi arudishe pesa za watu.

Sasa kuwa makini sana maana kuna dhulma sana inayofanywa na watendaji wabovu wa serikali ambayo huwezi jua kirahisi.

Niliwahi kukatiwa pande pale Bao babu, baada ya kuvuka mto Mpiji kama unakwenda Bagamoyo, kumbe nimekatiwa ndani ya himaya ya watu ikala kwangu. Siku nyingine nikaingia Talawanda/Maguru matali karibu na Kiwangwa, nikakuta kuna kibao kinaonyesha kuwa pale ni eneo lililo chini ya utafiti wa gypsum, ukubwa wake haujulikani. Kuwa makini kama unataka ardhi mitaa ya wilaya hiyo.
 
Nawashukuruni sana kwa taarifa hizi ambazo itabidi nizifanyie kazi kwa kweli! Nimeona niulize maana nasikia kuna wawekezaji huko wamepewa ardhi kinyemela au kisheria na wenyeji wanakaa kimya wakati wanakuuzia. Kuna eneo nilijaribu, kufika tu naambiwa kuna Mzungu amepewa hapo Ekari 200+.....sasa nimekuwa mwoga kidogo!

Thanks guys
 
MKUU ULIFANIKIWA
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom