Mashaka: Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu ya Kikatiba | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Mashaka: Kazi na Mamlaka ya Waziri Mkuu ya Kikatiba

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by Kasheshe, Nov 3, 2010.

 1. Kasheshe

  Kasheshe JF-Expert Member

  #1
  Nov 3, 2010
  Joined: Jun 29, 2007
  Messages: 4,690
  Likes Received: 91
  Trophy Points: 145
  52
  .-(1) Waziri Mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,usimamiaji, utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.
  (2) Waziri Mkuu atakuwa Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni.
  (3) Katika utekelezaji wa madaraka yake, Waziri Mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote a mbayo Rais ataagiza kwamba yatekelezwe.

  ===>Kuna mawaziri wakuu wamekuwa wananipa wasiwasi kama kweli wanafanya kazi zao za kikatiba... no wonder badala ya wananchi kulalamika utendaji mbovu wa Waziri Mkuu, yote wanampelekea Rais.

  Kalagabaho

   
 2. J

  JokaKuu Platinum Member

  #2
  Nov 3, 2010
  Joined: Jul 31, 2006
  Messages: 12,730
  Likes Received: 4,949
  Trophy Points: 280
  Kasheshe,

  ..kwa hiyo huu uozo wa Kikwete mnataka mumlaumu Pinda?

  ..the fact remains kwamba Mawaziri wanateuliwa na Raisi, na ndiye mwenye maamuzi ya mwisho juu yao.

  ..kwa mfumo wetu, Waziri Mkuu asipokuwa mtu wa karibu na kipenzi cha Raisi, basi lazima atapwaya, hata kama kweli anaijua kazi yake.
   
 3. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #3
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  Waziri Mkuu ni mtendaji Mkuu wa Serikali, yeye ni Kiranja wa Baraza la Mawaziri, Kiranja wa Bungeni, Kiranja katika utendaji wote wa Serikali husika.

  Katika Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania huu wadhifa umekuwa tofauti. Tumeshuhudia Waziri Mkuu wa Tanzania Mh. Pinda akitoa kauli ambazo baadaye anatokea kiongozi mwingine anaipinga kauli ya Waziri Mkuu Mfano

  (1) Ishu ya Luhanjo,
  (2) kukemea jambo kwa niaba ya Serikali mfano kuwasimamisha Dakitari na Katibu Mkuu Wizara ya Afya,
  (3) Alitoa amri ya kuwafukuza kazi madakitari wote ambao hawatatii amri ya kurudi kazini,
  (4) Alitoa ahadi kwa niaba ya Serikali alipoongea na madakitari aliahidi kuwa serikali itajitahidi kutekeleza madai yao kwa awamu.
  (5) Bungeni alitoa kauli kwa niaba ya Serikali kuwa Wabunge wameshaanza kulipwa posho mpya ambayo Raisi amesaini.
  (6) ..............  Tunaona kuwa kila anachosema basi atatokea kiongozi mwingine wa Serikali kumpinga. Hii inatia mashaka katika kuelewa nini madaraka ya Waziri Mkuu wa Tanzania???


  Natoa Hoja


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 4. Njowepo

  Njowepo JF-Expert Member

  #4
  Mar 5, 2012
  Joined: Feb 26, 2008
  Messages: 9,297
  Likes Received: 381
  Trophy Points: 180
  Nadhani madakatari watakkuwa walisahau kuongeza kuwa PM nae by Jtano awe ameachia madaraka!
  He is not firm on decision apa ndo nakumbuka the like of Sokoine
   
 5. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #5
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280
  RIP E. Sokoine alikuwa ni mfano wa kuigwa lakini katika viongozi wetu wa sasa hakuna mwenye uwezo wa kuiga ya Sokoine. Alikuwa mchapakazi haswaaa.


  MIZAMBWA
  INANIUMA SANA!!!
   
 6. Matola

  Matola JF-Expert Member

  #6
  Mar 5, 2012
  Joined: Oct 18, 2010
  Messages: 36,045
  Likes Received: 13,261
  Trophy Points: 280
  Naona umeamuwa kuwatafuta mashabiki wa Lowasa walipo, subiri tu sasa hivi....
   
 7. mizambwa

  mizambwa JF-Expert Member

  #7
  Mar 6, 2012
  Joined: Oct 8, 2008
  Messages: 4,409
  Likes Received: 568
  Trophy Points: 280

  Yaani RIP E. Sokoine alikuwa mchapakazi mzuri; tulimpenda lakini Mungu alimpenda zaidi.

  Nakumbuka katika harakati za kupambana na Wahujumu Uchumi na Biashara ya magendo. Watu walikuwa wanatupa bidhaa mbalimbali kwa hofu ya kukamatwa; hata pesa zilikuwa zinatelekezwa ovyo kwani waliogopa akishikwa nazo ni hatari.

  Naye Sokoine alikuwa si kiongozi wa kukaa ofisini na kusubiri watendaji kumletea taarifa ya kiutendaji; alikuwa anaingia mitaani kufuatilia mwenyewe, hadi Mwananyamala alifika kukagua uuzaji wa vyakula madukani (Kipindi kile iliitwa biashara ya ULANGUZI).

  Kiongozi gani leo hii anaweza kufika Mwananyamala kutembea kwa miguu mitaani, kama alivyofanya Sokoine??

  MIZAMBWA
  IANNIUMA SANA!!!
   
 8. c

  change we need Member

  #8
  Apr 22, 2012
  Joined: Aug 10, 2011
  Messages: 81
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  Habari wana Jf,

  nafikiri kuna habari kibao zinazoendelea bungeni kwa hivi sasa ukianzia na ripooti ya CAG na reaction ya wabunge juu ya waziri mkuu mengi yamesikika, najaribu kufikiria hivi tatizo la waziri mkuu kutokuwa na nguvu ya maamuzi ni suala ambalo katiba inambana asiwezi kuwaadhibu walio chini yake au ni uwezo binafsi wa mtu anayesimamia nafasi hiyo?

  Kwa maana kwamba kama kiongozi atakuwa dhaifu basi hakuna kitu na kama anauwezo atafanya maamuzi magumu hili limekaaje?
  unaweza kuchukulia mifano ya mawaziri wakuu waliotangalia pia na kuona au kuweka ulinganisho..
   
 9. Teacher1

  Teacher1 JF-Expert Member

  #9
  Apr 22, 2012
  Joined: Jan 29, 2011
  Messages: 313
  Likes Received: 24
  Trophy Points: 35
  Uwazili mkuu na urais ni tasisi kubwa mkuu, kuwajibisha waziri fulani bila bosi wake kutaka ni jambo gumu sana, maana kila aliyepewa uwazili kapewa kwasababu nyingi zikiwamo zile binafsi ukiachilia mbali kuweza au kutokuweza kazi. Wakati fulani unapoleta pendekezo la kumuondoa mtu unaweza kujibiwa kuwa bora uondoke wewe kuliko huyo utafanyaje.

  Jambo la kuweka wazi ni kuwa kati ya Rais na Wazili mkuu nani ananguvu zaidi juu ya waziri? maana tuliona wakati wa mjadala wa Ngereja Waziri mkuu alisema angekuwa na mamlaka angemtoa wakati uleule lakini atawasiliana na rais akifika kwenye safari yake. Sijui alipowasiliana alijibiwa nini ila hlikutekelezwa kwa namna hiyo namshauri Waziri mkuu ajiuzuru yeye kulinda heshima yake mbele ya umma.
   
 10. N

  NYAMKANG'ILI JF-Expert Member

  #10
  Apr 22, 2012
  Joined: Apr 1, 2012
  Messages: 223
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 35
  MKUU HOJA YAKO NZURI, NZITO. Ninapojaribu kuchangia hoja hii, ninakumbana na mambo mengi. Muhimu, makubwa mawili kama ulivyogusia yaani kupwaya kwa PM kazini ni
  (1) KATIBA haikumpa meno au
  (2) yeye mwenyewe kashindwa kazi.

  Mchango wangu ni huu:

  PM PINDA hajashindwa kazi ila anakwazwa na mambo kadhaa kutenda kazi zake. Jambo kubwa ni KATIBA ikunganishwa na RAIS. Jingine ni siasa za makundi ndani ya CCM.

  Ntaanza na KATIBA na RAIS. Kwa mujibu wa Katiba yetu RAIS ndiye mtendaji, yaani tuna EXECUTIVE PRESIDENT ambaye ndiye CHIEF EXECUTIVE OFFICER (CEO) wa serikali; na CEO huyu halazimishwi kikatiba kufuata ushauri wa mtu yeyote ikiwa ni pamoja na wa PM (angalia ibara ya 37 ya Katiba ya 1977 TANZANIA).

  MKANGANYIKO unakuja sasa kwa kuangalia ibara ya 52 INAYOAINISHA kazi za PM kuwa ni
  (1) kusimamia kazi za siku kwa siku za serikali;
  (2) kuongoza shughuli za serikali bungeni; na
  (3) kutenda kazi atakazoelekezwa na CEO RAIS

  MKANGANYIKO ni kuwa PM akapewa KAZI hizo Kikatiba, wakati, HANA MAMLAKA ya kuzisimamia, MAMLAKA yako kwa CEO RAIS (PM hana mamlaka hata ya kumsimamisha kazi mfagizi katika utumishi wa umma MAANA yeye PM siyo mamlaka yake ya nidhamu bali KATIBU MKUU wa ofisi ya PM anaweza kumsimamisha mgagizi, itakuwaje WAZIRI?). SASA PM huwa anafanyaje kazi zake? PM anachofanya ni 'umbea', yaani mtu/WAZIRI akimkwamisha anachofanya ni kulalamika kwa CEO RAIS. NA hapa ndo nasema RAIS anamkwamisha PINDA, kwani PM analalamika kwa CEO na CEO hachukui hatua.

  NINI cha kufanya,
  (1) kwa sasa PINDA anaweza kujiuzulu; na
  (2) mbele ya SAFARI kwenye mchakato wa Katiba mpya PM ndiye afanywe kuwa CEO.

  SIASA za makundi ndani y a CCM nazo ni kikwazo kwa PM, KWANI kuna kundi linataka serikali ishindwe ili wajenge hoja kuwa wao ndio suluhisho na hili JK analijua ndo maana anasita kutolea mambo mengi maamuzi kwa kuona kuwa ni vita ya makundi, na, iwapo akiamua hivi inakuwa ushindi kwa kundi hili au lile. CHAKUFANYA wananchi tuchukue hatua, CCM tuipumuzishe. THANX, TCHAO
   
 11. sammosses

  sammosses JF-Expert Member

  #11
  Apr 26, 2012
  Joined: Jan 24, 2011
  Messages: 1,205
  Likes Received: 83
  Trophy Points: 145
  Tutamsema sana waziri mkuu lakini wakati mwingine tuangalie majukumu yake kikatiba,Waziri mkuu kwa mujibu wa sheria ana majukumu yafuatayo:

  Ibara ya 52.-(1) Waziri mkuu atakuwa na madaraka juu ya udhibiti,usimamiaji,utekelezaji wa siku hata siku wa kazi na shughuli za Serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  (2) atakuwa kiongozi wa shughuli za serikali bungeni

  (3) katika utekelezaji wa madaraka yake,waziri mkuu atatekeleza au kusababisha utekelezaji wa jambo lolote au mambo yoyote ambayo Rais ataaagiza kwamba yatekelezwe

  Ukitazama tena ibara ya 53.-(1)Bila kuathiri masharti ya katiba hii,waziri mkuu atawajibika kwa rais kuhusu utekelezaji wamadaraka yake.

  (2) serikali ya Jamhuri ya Muungano,chini ya mamlaka ya rais,ndiyo itakuwa na uwezo wa kufanya maamuzi juu ya sera ya serikali kwa ujumla,na mawaziri,chini ya uongozi wa waziri mkuu,watawajibika kwa pamoja Bungeni kuhusu utekelezaji wa shughuli za serikali ya Jamhuri ya Muungano.

  Kutokana na ibara tajwa hapo juu utaona ni jinsi gani Waziri mkuu alivyo rubber stamp kutekeleza yale anayoamriwa na bosi wake(rais),halii hii ina sababisha rais kufanya mambo atavyo kwa kuwa tu katiba ndiyo inatamka hivyo.Mwalimu JK Nyerere aliwahi kusema katiba hii ina mfanya rais kuwa Diktekta kutokana na kuhodhi madaraka makubwa sana ndani ya nchi kwa mujibu wa katiba.

  Hali kama hii ya katiba isiyo na mashiko,ndiyo njia pekee inayoweza kusababishwa matabaka ya watu ndani ya jamii zetu bila kujali tunawatendea nini wananchi wetu.Mambo yamekuwa magumu kutokana na uchumi kushuka unaofanywa makusudi na mawaziri katika kutekelza majukumu yao.Waziri mkuu hapa utaona yupo yupo tu hana jipya zaidi ya kusulubiwa bungeni.Ingependeza kama sheria ingeweka wazi wakati bunge linawakilisha ripoti zake kuhusu matumizi ya umma, Rais angetakiwa kisheria kuhudhuria vikao hivyo na kujibu hoja za kamati kuliko hivi sasa.

  Kwa mantiki hii utagundua kutokana na ulegelege na kumnyima madaraka waziri mkuu ya kimaamuzi nchi hii itazidi kupokea kejeli za watawala na kuona kama upepo unaovuma tu na mwisho wake utaisha.Wanajamii wenzangu na karibisha mchango wenu tujaribu kuitibu hali hii kwani miongoni mwa changamoto tunazo toa kwa serikali, nyingi zinatoka ndani ya JF
  Ubovu wa katiba na mapungufu yake isiwe silaha ya kuwaadhibiwa wananchi kwa kufisidi mali za umma
   
 12. emmanuel1976

  emmanuel1976 JF-Expert Member

  #12
  Apr 28, 2012
  Joined: Jun 17, 2011
  Messages: 301
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Wadau wenzangu, je kuna haja ya kuwa na waziri mkuu mwenye mamlaka katika katiba mpya? na kama ndiyo kwa nini? na je kuna haja pia ya kufuta cheo cha waziri na kubaki na katibu mkuu kama kiongozi wa wizara? kama ndiyo, kwa ninina faida yake ni nini?
   
 13. VUTA-NKUVUTE

  VUTA-NKUVUTE JF-Expert Member

  #13
  Jun 14, 2012
  Joined: Nov 25, 2010
  Messages: 5,868
  Likes Received: 6,566
  Trophy Points: 280
  Kumekuwa na maoni mbalimbali juu ya nini hasa mamlaka ya Waziri Mkuu Pinda au yeyote awaye.Wengi wana maoni kuwa Waziri Mkuu Pinda hajiamini(au anaogopa) kuwaadhibu viongozi mbalimbali wa Serikali wanaovurunda wakiwemo Mawaziri. Suala la akina Jairo linajulikana vyema. Waziri Mkuu Pinda huishia kusema 'ingekuwa ni mamlaka yangu...'

  Waziri Mkuu anaundwa na kupewa mamlaka na Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.Anaundwa chini ya Ibara ya 51 na kupewa 'mamlaka' chini ya Ibara ya 52.Kwa kiingereza Ibara hiyo ya 52 inasomeka hivi:
  52.​
  -(1) The Prime Minister shall have authority over the control,supervision and execution of the day-to-day functions and affairs of theGovernment of the United Republic.(2) The Prime Minister shall be the Leader of Government business in theNational Assembly.(3) In the exercise of his authority, the Prime Minister shall perform or
  cause to be performed any matter or matters which the President directs to be
  done

  Kwa kifupi,Ibara ndogo ya 3 ya Ibara ya 52 niliyoinukuu hapo juu inampoka 'mamlaka' Waziri Mkuu. Hawezi kufanya lolote bila ya maelekezo ya Rais.Waziri Mkuu hana mamlaka yoyote hata ya uteuzi wa kiongozi yeyote wa kiserikali.Kama huteui,huwezi kutengua.Hiyo ndiyo sheria.

  Waziri Mkuu labda tu ni Kiongozi wa shughuli za Serikali Bungeni.Basi.Hata Mawaziri wanamshinda. Sheria nyingi za Bunge,kwa mfano,humpa uwezo Waziri wa Wizara husika kuunda sheria ndogondogo.Pia,Waziri hupewa mamalka ya uteuzi wa Wakurugenzi na Wajumbe wa Bodi za Mashirika mbalimbali.

  Waziri Mkuu hana lolote.Hateui yeyote Tanzania.Kuanzia sasa,tuendelee na ufahamu huo kichwani...
   
Loading...