Mashairi ya Azimio la Arusha

Companero

Platinum Member
Jul 12, 2008
5,604
1,704
Malenga Mwanakijiji na Waghani wengine Mnaoliamini Azimio Arusha,

Kwanza nawasabahi kwa Salamu ya Ujamaa na Kujitegemea. Ombi langu kwenu ni kuhusu tenzi na mashairi ya Azimio la Arusha. Tuko katika harakati za kutimiza unabii wa Malenga Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyebashiri kuwa mwisho wa siku tutarejea kwenye maadili ya msingi ya Azimio la Arusha. Sanaa ni njia mojawapo ya kuamsha kizazi hiki cha kifisadi ili kirejee maadili hayo hivyo naomba mtunge tenzi na mashairi ya kuhusu Azimio. Pia kama inawezekana wekeni tenzi na mashairi ya zamani kama yale yaliyohaririwa na Farouk Topan na Grant Kamenju . Mimi naanza kwa kudondoa beti hizi zilizoghaniwa kwa uchungu na mchumba wa Seti Benjamin Mpinga: Shujaa na Shahidi wa Azimio la Arusha:

Seti umeniacha upweke
Lini tukae tucheke?
Mbona hukuniachia pete
Kifo chako kwangu teke.

Safari usiyorudi tena
Wapi tutaonana?
Mbona hukuniachia pete
Faradha ya upendo hakuna.

Seti, Seti, nipe uso wako
Nani atatekeleza ahadi zako?
Mbona hukuniachia pete
Azimio na kaburi lako.

Seti pendo la roho yangu
Kifo ni amri ya Mungu?
Mbona hukuniachia pete
Upweke wanitia uchungu.

Machozi yanatiririka
Kweli Seti umekatika?
Mbona hukuniachia pete
Kamwe ari isiyopimika.

Saa ya kurejea maadili ya msingi ya Azimio la Arusha kwa ari isiyopimika ni hii!

Wasalaam,

Kamaradi wa Kaloleni
 
Seti ameacha wengi
wenye kutopenda tungi
japo hawakuwepo Arusha
wao waogopa rushwa!

pete sio ya dhahabu
ila yatosha ajabu
kutukumbushia mbali
na tuache ubahili!
 
"Hata kidogo. Sikubali kurudi nyuma kama wale vijana wawili waliotuhadaa pale Momella" - Seti Benjamini Mpinga: Shujaa wa Azimio la Arusha masaa machache kabla ya kulifia Azimio
 
Back
Top Bottom