Mashaidi wa kesi ya kupinga ubunge wa mh Lema wakimbia

Crashwise

JF-Expert Member
Oct 23, 2007
22,227
8,735
Nikatika hali ya kushangaza toka jana baada ya kesi kuhairishwa hadi leo ndipo mashaidi walipoanza kurushiana maneno na hatimaye kupelekea mashaidi leo kutouzuria mahakamani mchana wa leo ndipo wakili waupande wao kuomba kesho atawaleta mambo yamekuwa magumu kwao kwa kutoa ushaidi wa uongo wanaanza kukimbiana wenyewe
 
Posho za zilipunguzwa baada ya kuona kesi inaenda kuwa-Zuberi(kuwat** Vidole)!!
 
Wakamatwe wasweke ndani ndio watajua ubaya wa njaa za kujitakia! Ujinga mtupu
 
Hv kwa wale wenye ujuzi na sheria kidogo,hakuna kipengele kinachowezesha jamaha kupata kifungo iwapo itathibitika wametoa ushahidi wa uongo?
 
Naskia shahidi wa kwanza bw musa mkanga ameishiwa kinoma coz kutafuta umaarufu huku mama btilda hakum2ma
 
Hv kwa wale wenye ujuzi na sheria kidogo,hakuna kipengele kinachowezesha jamaha kupata kifungo iwapo itathibitika wametoa ushahidi wa uongo?

Mkubwa!

Nakwambia vipengele vipo kabisa ila sasa si unajua ni njaa ya tumbo ndiyo inawapa watu wakati mgumu Mkubwa!

Hwa mashahidi wote wa kesi ya Mheshimiwa Mbunge G. Lema wote wale ni wa kuokotwa na magamba.

Na hii lazima ile kwao flu!
 
yaaani ukisikiliza ushahidi wenyewewe wanaoutoa, naona mambo yanawendea komboooo
 
Iyo kesi lengo lake ni kumpa wakti mgumu lema asiwe karibu na wananchi,ila magamba wamestukiwa,IVI SHAHIDI WA KWANZA hajalazwa kwa presha kutokana na faces fever kunako court?
 
Hao mashahidi wa uongo ni wa kuwapopea mawe mitaani popote pale watakapoonekan. Ndiyo hao wanaorudisha vita vya ukombozi nyuma!!
 
Kweli njia ya mwongo ni fupi, ngoja tuendelee kusikilizia, mwaka huu tutaona mengi sana toka kwa wana magamba.
 
wamekimbiaee? Sasa kibao kiwageukiwe wao washtakiwe wafungwe

Shahidi wajana dhidi ya wakili wa Lema Kimomogoro yalikuwa kama ifuatavyo Wakili Umesema maneno gani yamekuuma Lema aliyatamka? Shahidi Swala la kuolewa zanzibar liliniuma sana Wakili Umesema ilikuuma wewe hukutaka aolewe zanzibar? Haikukupendeza? Shahidi Mimi ilinipendeza ila Lema haikumpendeza kabisa Wakili Nani alikujulisha Lema haikumpendeza Batilda kuolewa zanzibar uliyatoa wapi? Shahidi kutokana na swali lako ndiyo maana nikakujibu hivyo baada ya mahojiana ya Kimomomgoro kumalizika alifuata wakili wa serekali Masanja kumuhoji shahidi kama ifuatavyo Wakili Umezaliwa wapi? Shahidi Karangai kata ya kibwe tarafa ya mbuguni wilaya ya Arumeru Wakili Leo wewe ni mkazi wa wapi hapa Arusha mjini Shahidi mkazi wa sokoni 1 mtaa wa makao mapya Wakili kwa hiyo wewe sio mkazi wa karangai siyo? Shahidi Ndiyo Wakili Nini kilisababisha usiwe mkazi wa karangai na sasa uwe mkazi wa sokoni1 Shahidi Nimeolewa Wakili Kwa hiyo kilichosababisha usiwe mkazi wa karangai na uwe leo mkazi wa asokoni 1 ni kuolewa siyo? Shahidi Ndiyo Wakili unamfahamu Dk Batilda? Shahidi Ndio ninamfahamu kwa kumwona kwenye picha Jaji Hujamuona ana kwa ana kwa macho tangu uzaliwe? Shahidi Sijawahi kumuona Wakili Pia unafahamu kwamba amoelewa? Shahidi Nasikia tu ameolewa Wakili Mume wake unamfahamu? Shahidi Simfahamu Wakili Unafahamu kwamba mume wake anaishi Zanzibar? Shahidi Sifahamu ila nimesikia kwamba anaishi zanzibari Wakili Ulipoolewa toka karangai ukahamia sokoni 1 Batilda alipoolewa akahamia kwa mume wake Zanzibar ni kosa? Shahidi Sio kosa Wakili Hivi kuolewa katika jamii ni sifa mbaya au nzuri? Shahidi Ni sifa nzuri Wakili Kwa hiyo mtu akisema Amina Ally ameolewa sokoni 1 atakuwa amekupo sifa mbaya au nzuri Shahidi Ni sifa nzuri Wakili Kwa hiyo mtu akisema Batilda ameolewa Zanzibar atakuwa amesema vibaya? Shahidi Atakuwa amesema vizuri
 
Mkubwa!

Nakwambia vipengele vipo kabisa ila sasa si unajua ni njaa ya tumbo ndiyo inawapa watu wakati mgumu Mkubwa!

Hwa mashahidi wote wa kesi ya Mheshimiwa Mbunge G. Lema wote wale ni wa kuokotwa na magamba.

Na hii lazima ile kwao flu!

Mkuu nimefuatilia hapo kidogo tu kuna mkuu kaweka majibizano yalivyokua jana kati ya shaidi na mawakili,nimechoka mwenyewe,huu ni upotezaji wa muda wakati kuna kesi za msingi zinakosa kusikilizwa,nafikiri jaji/hakimu mwenyewe hata wamrubuni vipi hatotaka kuharibu taaluma yake kwa kuhukumu sivyo ndivyo!jamaha hawakujipanga sawa sawa kutengeneza uongo kwy kesi hii au watu wanaowatumia hawako sawia
 
Kwa hayo mahojiano yaliwekwa na Mgafilika basi hii kesi ni ze comedy.Ni yale yale ya kuhakikisha mbunge hapati muda wa kufanya kazi zake za kibunge na pia uwaziri kivuli wa mambo ya ndani
 
Mkuu mgafilika; niruhusu ni-edit post yako hapo juu:

Shahidi wajana dhidi ya wakili wa Lema Kimomogoro yalikuwa kama ifuatavyo:

Wakili: Umesema maneno gani yamekuuma Lema aliyatamka?

Shahidi: Swala la kuolewa zanzibar liliniuma sana

Wakili: Umesema ilikuuma wewe hukutaka aolewe zanzibar? Haikukupendeza?

Shahidi: Mimi ilinipendeza ila Lema haikumpendeza kabisa

Wakili: Nani alikujulisha Lema haikumpendeza Batilda kuolewa zanzibar uliyatoa wapi?

Shahidi: kutokana na swali lako ndiyo maana nikakujibu hivyo.

Baada ya mahojiano ya Kimomomgoro kumalizika alifuata wakili wa serekali Masanja kumuhoji shahidi kama ifuatavyo:

Wakili: Umezaliwa wapi?

Shahidi: Karangai kata ya kibwe tarafa ya mbuguni wilaya ya Arumeru

Wakili: Leo wewe ni mkazi wa wapi hapa Arusha mjini?

Shahidi: mkazi wa sokoni 1 mtaa wa makao mapya

Wakili: Kwa hiyo wewe sio mkazi wa karangai siyo?

Shahidi: Ndiyo

Wakili: Nini kilisababisha usiwe mkazi wa karangai na sasa uwe mkazi wa sokoni 1

Shahidi: Nimeolewa

Wakili: Kwa hiyo kilichosababisha usiwe mkazi wa karangai na uwe leo mkazi wa asokoni 1 ni kuolewa siyo?

Shahidi: Ndiyo

Wakili: Unamfahamu Dk Batilda?

Shahidi: Ndio ninamfahamu kwa kumwona kwenye picha

Jaji: Hujamuona ana kwa ana kwa macho tangu uzaliwe?

Shahidi: Sijawahi kumuona

Wakili: Pia unafahamu kwamba amoelewa?

Shahidi: Nasikia tu ameolewa

Wakili: Mume wake unamfahamu?

Shahidi: Simfahamu

Wakili: Unafahamu kwamba mume wake anaishi Zanzibar?

Shahidi: Sifahamu ila nimesikia kwamba anaishi Zanzibari

Wakili: Ulipoolewa toka karangai ukahamia sokoni 1, Batilda alipoolewa akahamia kwa mume wake Zanzibar ni kosa?

Shahidi: Sio kosa

Wakili: Hivi kuolewa katika jamii ni sifa mbaya au nzuri?

Shahidi: Ni sifa nzuri

Wakili: Kwa hiyo mtu akisema Amina Ally ameolewa sokoni 1 atakuwa amekupo sifa mbaya au nzuri?

Shahidi: Ni sifa nzuri

Wakili: Kwa hiyo mtu akisema Batilda ameolewa Zanzibar atakuwa amesema vibaya?

Shahidi: Atakuwa amesema vizuri

Jamani kwa mwenye uelewa wa sheria, hivi role ya wakili wa serikali kwenye kesi kama hii (za uchaguzi) huwa ni nini? Kidogo hoja zake zimeniacha kwenye dilema.
 
Yaaani pamoja na majibu kama haya ya shahidi hakimu bado anasikiliza kesi???
 
Back
Top Bottom