Ninawaonea huruma sana wale Waendesha Mashataka wa Serikali! Wanastrugle sana sana kuonesha kuwa akina Mbowe walikuwa na makosa ya ugaidi.
Yule shahidi wa jana aliposema tu yale maneno "Mpo chini ya ulinzi kwa sababu mnajihusisha na vitendo vya ugaidi" yakawa yametofautiana na maelezo yake.
Hapo moja kwa moja inaonesha jinsi alivyopangwa kimkakati wakati akijua fika kuwa wakati hao watuhumiwa wakikamatwa hakukuwa kamwe na kitu kilichoitwa kosa la ugaidi.
Kwangu mimi hata mtu mmoja tu akionewa huwa ninaumia sana. Hapa hawa watu wanaapa kusema kweli mbele za Mungu, yaani hawana hofu kwenda kuongea uwongo mchana kweupe ili tu kuwapendezesha wanasiasa wanaotawala nchi.
Dada yangu muuza mbege hivi huna hata hofu ya Mungu? Hivi leo Mbowe na wenzake wakiachiwa wakawa huru utafunika wapi uso wako huo?
Ikatokea Mbowe akaja kuinuliwa na Mungu akaiongoza nchi hii wewe utamwambia nini Mungu wako?
WaTanzania tupendane, chuki hivi zinatupeleka pabaya sana! Sio vizuri kumshuhudia mwenzio uwongo kwa kuwa tu Mungu haaadhibu wakati huo huo! Kuna wakati tutalia na kusaga meno.
Ni hayo tu leo!