Mashahidi wa Uganda wakumbukwa

kbm

JF-Expert Member
Oct 5, 2012
5,222
1,670
Mashahidi Wakristo wakumbukwa Kampala
Waumini wa madhehebu ya kikatoliki wanaoshiriki makumbusho ya mwaka huu wa mashahidi wa Namugongo nchini Uganda wamekuwa wakiwasili mjini Kampala, huku kukiwa na ulinzi mkali.
“Shughuli kuu za maadhimisho zimefanyika leo, ikiwa ni pamoja na ibaada maalum.”

Mtakatifu Charles Lwanga, na wakristo wenzake, walikuwa ni kundi la wakristo (Wakatoliki na pia kanisa Anglikana), ambao waliuawa chini ya amri ya Mwanga wa Pili, ambaye wakati huo alikuwa Kabaka wa Buganda, kati ya mwaka 1885 hadi 1887.
Kabaka alikuwa na wasiwasi kwamba wakristo hao walihatarisha uongozi wake.
22 kati ya mashahidi hao wa kidini waliouawa walikuwa ni Wakatoliki, na Papa Paul wa sita aliwatangaza kama watakatifu, tarehe 18, mwaka 1964.
Ingawa wale ambao walikuwa ni wa kanisa la Anglikana hawakutangazwa kama watakatifu chini ya kanisa Katoliki, Baba Mtakatifu alizitaja sifa zao.
Mashahidi hao wakristo hukumbukwa kila mwaka, tarehe 3 mwezi Juni.

[h=2]01. Wafiadini wa karne ya 19 [/h]
Kati yao wanajulikana na kuheshimiwa duniani kote kwa namna ya pekee Wakatoliki 22 waliokuwa wahudumu wa ikulu ya kabaka wa Buganda Mwanga II (1884 - 1903) ambao waliuawa kati ya tarehe 15 Novemba 1885 na tarehe 27 Januari 1887 kwa sababu ya kumwamini Yesu Kristo baada ya kuhubiriwa Injili na Wamisionari wa Afrika walioandaliwa na kardinali Charles Lavigerie.

Ndio wafiadini wa kwanza wa kusini kwa Sahara kuheshimiwa na Kanisa Katoliki kama watakatifu. Majina yao ni haya:



Katika ibada ya kuwatangaza hao (1964), Papa Paulo VI alitaja pia kwa jumla wafiadini wengine wa dhuluma hiyo waliokuwa wa madhehebu ya Anglikana.[SUP][1][/SUP]
[h=3]
02. Wafiadini wa Anglikana
[/h]Labda ni wengi zaidi Waanglikana waliouawa katika dhuluma hiyo, kuanzia Yusufu Lagamala, Mark Kakumba na Noah Seruwanga waliokatwakatwa vipandevipande na kuchomwa moto tarehe 31 Januari 1885.
Waliofuata ni askofu James Hannington na wenzake waliouawa tarehe 29 Oktoba 1885 kabla hawajaingia Buganda.
Mwaka 1886, kati ya tarehe 25 Mei na 3 Juni, waliuawa: Moses Mukasa (kwa mkuki), Muddwaguma na Elias Mbwa (kwa kuhasiwa), David Muwanga (tarehe na aina ya kifo chake haijulikani), Omuwanga, Kayizzi Kibuka, Mayanja Kitogo aina ya kifo chao haijulikani), Alexander Kadako na Frederiko Kidza (kwa kupigwa), Noah Walikaga , Daniel Nakabandwa, Kiwanuka Gizayo, Mukasa Lwa Kisiga, Lwanga, Mubi, Wasswa, Kwabafu, Kifamunyanja, Muwanga Njigija (wote kwa kuchomwa moto), Robert Munyagabyanjo (kwa kukatwakatwa vipandevipande na kuchomwa moto).
[h=3]
03. Mfiadini wa Uislamu
[/h]Katika dhuluma hiyohiyo aliuawa pia Mwislamu mmoja.
Mwanzoni mwa karne ya 20 vijana wawili tena wa Kanisa Katoliki walimfia Yesu (1918) wakatangazwa wenye heri na Papa Yohane Paulo II mwaka 2002: Daudi Okelo na Jildo Irwa.
[h=3]Mfiadini wa Anglikana [/h]Askofu Luwum wa Kanisa la Anglikana la Uganda aliyeuawa na Idi Amin
Mwaka 1977 Idi Amin alimuua askofu mwingine wa Anglikana, Janani Luwum.
 
Mimi Mkatoliki halafu Jumuiya yangu imepewa jina lao watakatifu mashahidi wa Uganda tunasherehekea siku yao Jumamosi hii tarehe 08..karibuni tusali pamoja
 
Back
Top Bottom