Mashabiki wa Yanga waipongeza timu yao kwa kunyakuwa ubingwa

moodykabwe

JF-Expert Member
Aug 16, 2015
625
602
YANGA WHATSAPP SUPPORTERS MAKAO MAKUU Tunajipongeza safari Tulioanza na timu yetu Toka mwanzo ____________________________Na


Hatimaye timu ya Wananchi Dar es Salaam Young African ( Yanga ) imetwaa ubingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara huku ikiwa na Mechi 3 Mkononi Baada ya kufikisha point 68 katika Michezo 27. Point ambazo haziwezi kufikiwa na Timu yoyote.


Yanga sasa anakuwa bingwa kwa kuweka historia ya kuchukua Kombe la ligi kuu Mara 26
>=======<
》》》》》》》》》》》

Timu ya Yanga inayoshiriki ligi kuu ya Tanzania Bara Jana imetwaa taji la ligi kuu inadhaminiwa na kampuni ya mitandao ya simu ya Vodacom. Yanga imefanikiwa kutwaa kombe kabla ya mechi yake kutokana na timu ya Simba kukubali kipigo kutoka timu ya Mwadui hivyo haitaweza tena kufikisha alama ilizonazo Yanga.

Yanga inatwaa taji la ligi kuu kwa kufikisha alama 68 ambazo kutokana na kufungwa Simba hawatoweza kuzifikisha tena na ilikuwa ndio timu pekee ambayo ingeweza kufikisha alama hizo hivyo kuhitimisha mbio ubingwa na Yanga kufanikiwa kutwaa taji kwa mara ya pili mfululizo.Macho na masikio tunaenda kubeba kombe la shirikisho sasa CAF

Tunakushuku Mungu kwa kutusimamia Tumemaliza la nyumbani-!!


Mungu ibariki Yanga Africa CAF
Mungu ibariki YWSMM

Asaivi tunawaza kombe hili tu
a4f648298f29f33606fadbb6e08ab526.jpg
 
Back
Top Bottom