Mashabiki wa Ronaldo na Messi msimu 2017/2018 mjiandae kisaklojia tuzo ya Ballon d’Or

Ladder 49

JF-Expert Member
Dec 19, 2017
7,416
18,856
Wakuu habari zenu?

Msimu wa wa 2017/2018 umekuwa msimu mzuri kwa mo salah tofauti na watu walivyodhani.

Ronaldo na Messi Sasa wamepata mpizani wa kweli kwenye tuzo za ballon d’or msimu huu na kuna dalili zote mo salah anakwenda kuchukua hiyo tuzo .

Msimu wa 2017/2018 ulianza mwezi august kwa ligi epl na la liga ulianza September .

Kwa epl mo salah amechukua mchezaji bora wa mwezi mara 3 ,akiweka record kwa mchezaji kuchukua mchezaji bora wa mwezi mara nyingi zaidi katika historia ya epl.

Kwa la liga angalia hapo chini mchezaji bora wa mwezi,la liga msimu wa 2017/2018 ilianza mwezi September tangia ianze hesabia hapo ronaldo na messi wamepata mara ngapi?

Kama ujawaona jiulize kwanini? Mchezaji bora wa mwezi wanajumuisha performance ya wachezaji wote wa ligi kwa walichokifanya.


IMG_2577.JPG



UEFA Champions League msimu wa 2017/2018

Ronaldo kachukua mara 3 mchezaji bora wa wiki

Messi mara 1

Salah mara 3

Kuna watu watasema bado kwanza mpaka world cup tuone atafanya nini,

Niwakumbushe tu msimu wa 2009/2010 kulikuwa na FIFA World Cup nchini South Africa .

Messi alichukua ballon d’or ,Messi hakufunga hata goli moja mpaka wanatolewa World Cup .

Niwakumbushe msimu wa 2009/2010 Sneijder mchezaji wa inter Milan huo msimu ulikuwa na World Cup.

alichukua makombe yote ya ligi ya Italy na makombe mengine nje ya Italy ikiwapo klabu bingwa dunia na UEFA Champions League.

Wadau wa soka mtakuwa mnaikumbuka ile inter milan ya Mourinho.

World cup Sneijder aliisaidia uholanzi kufika fainali na alilingana magoli na mfungaji bora wa World Cup 2010(world cup wanaesabia na assists ulizokuwa nazo mkilingana magoli,mwenye assist nyingi ndio mfungaji bora)

messi mimi nimemtafuta kwenye list ya wachezaji waliofunga na hata waliojifunga World Cup 2010 nchini South Africa hayupo .

Hapo chini nimeweka record ya Sneijder .

IMG_2576.JPG


Kura zinapigwa na makocha na macaptain wa timu za taifa

Anachaguliwa baada ya World Cup kuisha tu mwezi wa saba

Kuna dalili zote mo salah akachukua hiyo tuzo

Kwenye UEFA Champions League msimu huu wa 2017/2018 kwenye kugombea mchezaji bora wa week aliwagalagaza ronaldo na messi na kuibuka mchezaji bora wa week .

ikitokea ameingia kwenye nomininee lazima ashinde hiyo tuzo aijalishi yupo na nani.hii inaonesha jinsi gani anakubalika na watu wanaona uwezo wake.

IMG_2560.JPG


Mchezaji ambaye aliobahatika kuingia kwenye tuzo ya ballon d’or na kuwashinda Ronaldo na Messi ni ricardo kaka pekee ilikuwa mwaka 2007.

Mimi binafsi sijaona sifa ya kupewa ballon d’or ronaldo Au messi msimu wa 2017/2018 yakumzidi mpinzani wao.

Kama unavigezo tililika hapo chini.

Najua Messi na ronaldo ni bora lakini hiyo ni history tunazungumzia msimu wa 2017/2018.sasa usituletee Messi na ronaldo wa miaka ya nyuma hiyo imebaki story.

Nawasilisha.
 
Salah anadaiwa taji tu..
Abebe Uefa afunge hesabu kabisa
Cr7 fan ila Mo Sarah Farao waache wizi Jamaa yuko moto na ninaenda nae Russia mi ni Egypt fan
 
Makombe ya mashindano makubwa yana pointi nyingi kwenye kushinda hiyo tuzo. MO akiweza kuchukua angalau makombe makubwa mawili anaweza kupata point nyingi na kubeba hiyo tuzo kwani CR7 na Messi watakuwa na point chache. Mesi hakuchuklua World cup lakini ukifuatilia alikuwa na makombe mengine makubwa angalau mbili na zaidi. CR7 mwaka jana alichukua kwa saabu alishinda ligi na UEFA

MO anatakiwa Liverpool ichukue UEFA halafu Misri ishinde worldcup??
 
Ni makosa makubwa kuwafananisha Messi na Ronaldo kwa huyu Salah ambaye tumemwona msimu mmoja tu
 
Ronaldo kaifungia madrid mechi 12 mfululizo kwa idadi ya goli 22,ronaldo kaifungia madrid mechi 15 mfululizo za UCL, ronaldo mpk sasa ndie anaongoza kwa magoli kuliko mchezaji yeyote ktk ligi kubwa tano barani ulaya, yani England, Spain, Italy, Germany na France

Nipe record za salah alizomzidi ronaldo
 
Nikweli Ni mwafrika mwenzetu Lazima tumsapoti ila bado mapema kumfananisha na Ronaldo Au Messi bado hajifikia Kiwango cha hao watu
 
Nikweli Ni mwafrika mwenzetu Lazima tumsapoti ila bado mapema kumfananisha na Ronaldo Au Messi bado hajifikia Kiwango cha hao watu
 
Mo atasubiri sana. Mechi ya Egypt vs Portugal friendly ilionyesha nini maana ya specialist na consultant. Mo katupia moja CR7 akazima furaha hiyo kwa mbili. Pia mo hana wadhamini wenye ushawishi kama Messi na CR7. Mpira pia in biashara na matangazo. Akina messi wanachukua kwasababu ya makampuni yanao wadhamini. Mo kama chadema na Ccm uchaguzi kinondoni......hahahaaaa!
 
Hii tuzo anapewa kulingana na mchango wako katika timu ndiomana hata makipa wana kuepo pia timu ya huyo mchezaj inatakiwa iwe imechukua vikombe muhimu na wanaangali huyo mchezaj akiwepo na asipo kuepo mchango wake unakua na impact kiasigani pia uwezo wa kuamua matokeo pia hizi kura wanapiga makocha wachambuzi nguli na elites wa mpira. .....salah ni mzuri ila timu yake itamuangusha labda wakichukua uefa na wajitahidi timu ya taifa ila binafsi bila naona Messi ana nafasi kubwa mno kwasab anaongoza kwa kufunga kuasist na ku create chance na amekua akiamua matokeo katika mechi ambazo barca imetaitiwa hata Argentina bila Messi tusinge waona kwenye world cup
 
Ronaldo kaifungia madrid mechi 12 mfululizo kwa idadi ya goli 22,ronaldo kaifungia madrid mechi 15 mfululizo za UCL, ronaldo mpk sasa ndie anaongoza kwa magoli kuliko mchezaji yeyote ktk ligi kubwa tano barani ulaya, yani England, Spain, Italy, Germany na France

Nipe record za salah alizomzidi ronaldo
Hapa hatuangalii record ukitaka tutashusha za Messi ukimbie
 
We unafikiri Argentina wakichukua world cup kunaatakae chukua hyo tuzo tofauti na messi?
 
Salah akichukua UEFA ndio anaweza sumbua kwenye hicho kinyang'anyiro. Ila vinginevyo vyovyote Mess na Ronaldo mmoja wapo atachukua.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom