Ryzen
JF-Expert Member
- Dec 6, 2012
- 7,301
- 8,693
Jina la beki wa kati wa Real Madrid na nahodha wa timu hiyo Sergio Ramos bado linazidi kugonga headlines katika mitandao ya kijamii, Ramos bado amekuwa akijadiliwa na mashabiki wa soka kuhusiana na kadi yake nyekundu aliyooneshwa wakati wa mchezo wa El Clasico dhidi ya FC Barcelona.
Sergio Ramos alioneshwa kadi nyekundu dakika ya 77 ya mchezo baada ya kumchezea faulo Lionel Messi inayoaminika kuwa ni mbaya kwa mashabiki wa Barcelona, licha ya kuoneshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja walitamani kuona Ramos akikosa mchezo zaidi ya mmoja kwa kosa hilo.
Beki huyo kwa sasa ataukosa mchezo mmoja wa Real Madrid wa siku ya Jumatano dhidi ya Deportivo utakaochezwa katika uwanja wa Municipal Riazor, kitendo ambacho hakijawafurahisha mashabiki wa Barcelona na kulaumu mitandaoni wakiamini Ramos anastahili kukosa mchezo zaidi mmoja kwa faulo aliyomchezea Lionel Messi