Nini kilimsukuma kuingia kwenye siasa,
nini msimamo wake kutokana na ccm kutokuwa na msimamo, inasubiri wapinzani ndio iige, mfano mkutano wa jangwani walioiga kwa chadema - mpiga simu
Amesema mwanasiasa mzuri ni yule anayekubali kushindwa kama vile yeye alivyokubali kushindwa! Ni kweli hii?
Masha tangu mwanzo hakuwa tayari kushindwa. Angalia hapa:
1. Aliamrisha maafisa wa Uhamiaji (idara iliyokuwa chini ya wizara yake) wachunguze uraia wa mpinzani wake Wenje, na hatimaye Mkurugenzi wa halmashauri ya jiji la Mza (returning Officer) alimuondoa katika kinyang'anyiro baada ya kumwekea pingamizi. NEC ilimrudisha Wenje. Habari pia zilizagaa kwamba Masha alimuofer Wenje Sh 350 milioni ili ajitoe.
2. Wakati wa kampeni kuna gari moja lililoibiwa Kenya lilikutwa Mwanza limebandikwa picha za Masha za kampeni. Sijui hii ishu iliishia vipi.
3.Ilimchukuwa Returning Officer siku mbili kutangaza matokeo, ucheleweshaji ambao ulitaka kuzua ghasia kubwa. Zilikuwa zinatafutwa namna ya kumpa ushindi asiostahili.
Anapenda misifa tu huyo. Juzi juzi tu alikuwa katika kipindi cha mikasi cha ITV akihojiwa na yule Salama wa Bongo Star Search akiongea vitu kama hivyo hivyo!
Masha anatafuta namna ya kurudi kwenye siasa...anatafuta daraja. Angekaa kimya tungemheshimu. Huwa nawashangaa sana ccm wanapokuwa madarakani wanakuwa wanakula tu, wakitoka wanaanza kuzungumza kana kwamba wao ni wema sana!
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.