Kurzweil
JF-Expert Member
- May 25, 2011
- 6,622
- 8,397
Mwenyekiti Mtendaji Fastjet Tanzania, Lawrence Masha amesema ni kweli shirika hilo lilikuwa na madeni lakini Mamlaka zingeshirikiana naye angehakikisha fedha hizo zinalipwa
Waziri huyo wa zamani wa Mambo ya Ndani nchini anayemiliki asilimia 68 za hisa kwenye shirikia hilo amesema kuwa Fastjet PLC ilianza kukusanya fedha na wameshakusanya Dola za Kimarekani Milioni 35
Amesema "Fastjet imelipa baadhi ya madeni yake, mengine yanalipwa na Fastjet PLC. Fedha nyingine tumekodi ndege na kulipia vibali, Mamlaka zinatakiwa kuniruhusu kufanya kazi ili nipate fedha za kulipa madeni mengine."
Masha ambaye amesema anaiheshimu Serikali na nchi kwa ujumla amesema yupo tayari kufanya kazi na TCAA, Wizara husika na Serikali yote kwa kipindi chake chote cha biashara