Masha awaeleze Watanzania juu ya Dual Citizenship | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Masha awaeleze Watanzania juu ya Dual Citizenship

Discussion in 'Jamii Intelligence' started by MLEKWA, Apr 28, 2010.

 1. M

  MLEKWA Senior Member

  #1
  Apr 28, 2010
  Joined: Aug 18, 2007
  Messages: 138
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Hili inabidi watanzania tumuulize mheshimiwa Rais na Waziri wa mambo ya ndani vipi Wana Msumbiji wasio Raia wa Tanzania waweze kupiga kura Visiwani Zanzibar huku Wapemba wakinyimwa vitambulisho vya Kupiga kura jee CCM haiwaamini tena Watanzania ndio ikaanza kuokokota okota wageni ?

  Haya ndio aliofanya Moi kuchukua waganda wa mpakani kumpigia kura na mwishowe wakenya kuisambaratisha KANU naona strategy hii ndio itakayoimaliza CCM kwa kuuuza uraia wa Tanzania kwa wageni.

  Inakuaje Mkimbizi apige kura Tanzania kweli huyu ni mkimbizi au mkimbizi mzawa , hapa idara ya uhamiaji iwaeke sawa Watanzania.

  For more informoation see images below.

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]

  [​IMG]
   
 2. Ruge Opinion

  Ruge Opinion JF-Expert Member

  #2
  Apr 29, 2010
  Joined: Mar 22, 2006
  Messages: 1,696
  Likes Received: 305
  Trophy Points: 180
  Huu ni ushahidi wa jinsi chaguzi zinavyoibwa huko visiwani. Mbali na hao wageni wapo wanajeshi na mapolisi wanaopelekwa huko kutoka bara kila uchaguzi ukikaribia. Wanaandikishwa kwa ubabe na kukipigia kura CCM. Cha kushangaza ni kuwa CUF huwa wanaishuhudia hali hiyo lakini uchaguzi ukiisha na wao kulizwa huwa hawalifuatilii tena.
   
 3. Z

  Zhule JF-Expert Member

  #3
  Apr 29, 2010
  Joined: May 22, 2008
  Messages: 354
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mkuu kitambulisho hicho cha kwanza pia ungeweka ukurasa yenye picha yake au jina lake kama lilivyo hicho cha Tanzania. hapo tungekuelewa vizuri. lakini kwa jinsi ilivyokaa lol!
   
 4. M

  Mbopo JF-Expert Member

  #4
  May 5, 2010
  Joined: Jan 29, 2008
  Messages: 2,532
  Likes Received: 8
  Trophy Points: 0
  Makubwa na siamini kwamba yanatokea katika nchi yetu! I hope vyombo vyetu vya ulinzi na usalama havijalala maana hii ndiyo hatari ya watu hawa baadae kujipenyeza hadi katika ngazi za utawala na baadae ukawa na kiongozi mkimbizi.
   
 5. N

  Nanu JF-Expert Member

  #5
  May 5, 2010
  Joined: May 29, 2009
  Messages: 1,224
  Likes Received: 5
  Trophy Points: 135
  Mh. Masha hapa huwezi kukaa kimya, tafadhali tupe ufafanuzi!!!!!
   
 6. w

  wasp JF-Expert Member

  #6
  May 5, 2010
  Joined: Aug 19, 2009
  Messages: 206
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  Masikini Mh. Masha ataeleza nini? Yeye hausiki na vitambulisho vya huko Zenji. SMZ ndio imeumbuka vilivyo.
   
Loading...